Ramadhan Special Thread

Assalamu Alaykum ndugu zangu katika iimani na wanaJf.

Ni matumaini yangu mpo wazima wa afya na ni wenye hamu na mahaba yamewajaa kwa huyu mgeni wetu Ramadhani. Alhamdulillah! nina uwezo wa kuishi pasipo na Jf na bila shaka wapo humu miongini mwao tunaokutana kwenye majukwaa tofauti tofauti: Nia na madhumuni ya huu ujumbe wangu ni kwamba hatutoonana kwenye Jf kuanzia sasa mpaka Ramadhani itakapokwisha inshaallah.

Binafsi ni mwenye furaha pia kuhusu mwezi wa Ramadhani. Mungu atukubalie swaumu zetu na atujaalie lengo haswa la swaumu tulipate, nalo ni uchamungu. Kwa wale tuliyo kwaruzana hapa na pale kwenye majukwaa tofauti tofauti naomba mnisamehe. Kwangu hakuna aliyenikwaza, mmekuwa wema zaidi kwangu kuliko nilivyokuwa kwenu. Naombeni mnisamehe. Nawatakia Ramadhan Mubaarakah.
 
Karibu sana
Ni kuelimishana tu kwani watu wanakosea tu
Kuna wengi wanatumia neno Juma'a Kareem lakini nalo ni kosa pia Kareem ni Allah na inatakiwa iwe Ijumaa (Juma'a) Mubarak
(Kwa manufaa ya wote Dada)
Nazidi kujifunza Mkuu natumai wengi wamekuelewa maana hata mie nilikuwa miongoni mwa watumiaji wa hilo neno na nilikuwa naona sawia tu.
 
Naomba uniambie maana ya misamiati kareem

Karimu ni jina lenye asili ya kiarabu,ambalo kwa Kiswahili,hutafasiriwa kwa tamko "Ukarimu", lenye maana :

ukarimu

NOMINO wingi ukarimu



  • 1
    utoaji vitu au mali kwa kukaribisha watu au kuwasaidia wanaohitaji msaada bila ya malipo.

    Visawe
    fadhila, hisani

    Maana hiyo kilugha haikai sambamba na mwezi ikaleta maana.
 
Ili mradi tu sio mke wako wa halili basi sio jambo lenye kupendeza.
Uislamu unatafsiri mtu kuwa mke na mume ikiwa tu mmefunga ndoa.

Ni mambo yasipendeza hata kama sio wakati wa ramadan, ila kama una nia kweli ya kumuoa basi jitahidi ufanye hivyo.

Ila kuhusu kuharibu swaum sina ilmu nalo ila jitahidi bwana kuoa kwani ndoa ni nusu ya dini na jambo lenye kupendeza mbele ya allah.



Wallahu a'aalam
 
Kuna katazo gani la kutumia emoji ya mikono ?

Kuaema halina asili peke yake haitoshi kuonesha haifai.

Kuna katazo gani kutumia emoji za mikono mkuu?
Uislam unakwenda kwa hoja ya ayat na hadith za mtume.

Alete hoja iliyowazi ama fatawa ya wanachuoni kuonyesha uharamu wa neno hili "ramadan kareem"

Kuhusu emoji hakuna, hakuna mahali popote imekatazwa kwenye uislamu ni sawa na mtu akuambie leta dalili ya kutumia watsup.
 
Rejea hadithi ya mtume amani ya Allah iwe juu yake isemayo "Mwenye kujifananiza na kaumu fulani,basi na yeye ni miongoni mwao"
Ndugu yangu hadithi hii ni sahih kabisa ila hapa kwenye emoji huwezi itumia hii.

Emoji ni katika maendeleo tu ya sayansi na technlojia na uislam unakubaliana na hali hii.

Hakuna uharamu wowote iwe kutoka kwenye qur an, hadith wala fatawa za ahlul ilmu
 
Naaam sasa kusema ramadhan kareem (si nikusema ni heri ya kutakiana ukarimu/wema/huruma ndani ya mwezi huu)
 
Hata ulicho pinga sielewi naona umekubali comment yangu kwenye mwenzi Mtukufu tunakumbushwa kutoa Swadaka hapo Umeandika kwenye comment yako nilijua neno Karim ni lugha chafu kama ni hivyo acha nilitumie RAMADHAN KAREEM
 
Aje kutuelewesha vizuri kwanza mimi hili neno Karim sijamuelewa iweje iwe halitakiwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…