Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Dada kuna watu "fii quluubihim maradh fazaada humu llah maradhwaa...."ilaa akhiril aya...
Sasa iyo profile picture itawaharibia swaumu dear...[emoji1]
Hahaha kipenzii,nduguu,dada angu[emoji23]sote tu ,tubadili Mimi na ww.mimi naitoa Sasa ivi isijeniharibia saum yngu na ya wengine[emoji3][emoji28]
 
Mambo Yaliyopendekezwa Kwa Mwenye Kufunga

Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo;


1. Kula daku
Amehadithia Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) amesema:

‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.” [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah].
Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’

[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2945 imeripotiwa na Ibn Hibbaan].

Pia Imependekezwa kuchelewesha kula daku. Amehadithiya Anas kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema:

‘’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikula daku kisha akatoka kwenda kuswali. Anas akamuuliza “Kulikuwa na muda gani baina chakula cha daku na adhaana?” Akajibu: “Ilikuwa kiasi cha kusoma Aayah khamsini za Qur-aan".
[Imeripotiwa na Imam Al-Bukhaariy na Muslim].
Pia ameruhusiwa amalize chakula chake anaposikia Adhaana ya Fajr. Abu Hurayrah amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

“Endapo mmoja wenu atasikiya adhaana na mkononi mwake ana kinywaji, asirudishe kinywaji hicho mpaka aridhike nacho.

’’[yaani anywe mpaka amalize haja yake]. [Imesahihishwa na Shaykh al-Albaaniy katika al-Jami' as-Swaghiyr na.607].
Barakallahu fyka Kumbe Nyoka Mzee ni Bonge la Sheikh Nmepitia post zako naona zmejaa Nusus tupu MashaAllah...!!!
 
Dada kuna watu "fii quluubihim maradh fazaada humu llah maradhwaa...."ilaa akhiril aya...
Sasa iyo profile picture itawaharibia swaumu dear...[emoji1]
Allah Akubaliki ila Akhy wanachuoni wetu wa kiislam wamekataza kuandika Quran kwa lugha nyingine yaani Transliteration hili hali fai na linaitoa Quran kutoka ktk Asli yke
Ushauri wangu kwa ndugu zangu ktk Imani ni kuwa, tujitahidi kujipinda na ibada zaidi ktk mwezi huu wa Ramadhan

1. Tuhakikishe tunaswali swala zote kwa wakati bila ya kukosa.

2. Tunajisomea Qur'an kwa wingi na ikiwezekana kumaliza Juzuu 30 zote.

3. Kupata darsa za kuzihuisha nyoyo zetu ili ziweze kudumu na ibada pamoja na kufanya yale yenye kheri

4. Kupata darsa za Tafsiri za Qur'an ili kuweza kutambua maamrisho kama yalivyo ktk Qur'an. Ukishindwa basi Hata kusikiliza Audio kutoka kwa masheikh wetu zinazopatikana ktk web tofauti tofauti kama Alhidaaya, wanachuoni, east africa Quran and Sunna Society. Google ni rafiki muhimu. Ukiweza pia kuna web za kiingereza nitawawekea nikiwa ktk computer.

5. Ramadhan si mfungo wa chakula draft, bali ikiwezekana tuwatafute wasio na uwezo tuwape sadaka ya vyakula ambavyo wengi wetu hufanya israfu.

6. Taraweh na Sala za usiku ziwe katika malengo yetu na hakikisha unahudhuria misikiti ambayo ina visomo virefu ili ku maximize muda wetu kwenye ibada.

7. Tujiepushe na laghwi zozote. Mfano frequenting ktk websites za kuchat tu, miziki na mengineyo yasiyomfurahisha Muumba. Games kwa munasaba wa kupoteza muda si mahala muafaka ktk Ramadhan bali yatupasa tuipambe ramadha kwa Nyiradi, visomo na kusikiliza Quran.

8. Tuombe maghf'iraa kwa wingi sana, ikiwezekana lia na nafsi yako, toa machozi kujisuta kwa madhambi tuliyowahi kuyafanya na tuazimie kutorejea tena ktk madhambi hayo mfano wa Riba, utesi, zinaa, wizi, kusengenya, shiriki, kula mali za yatima, dhulma, liwatwi, kuacha kusali, kuacha kuhiji kwa wenye uwezo na mengi ktk madhambi ambayo Iblis mwenye laana ametupambia nayo.

9. Tuunge udugu kwa kutembeleana na kufuturishana.

10. Tutoleane salamu na tujiweke mbali na mikusanyiko ambayo kwayo maasia yanapatikana.

Allaah atufanyie wepesi sote na tuiombee nchi yetu na viongozi wetu ili Wasiipoteze hii nchi na kuiharibu.

Ameen

74c9bac6419eb62c3881e0fe2a411645.jpg
 
Ahsante sana kwa ukumbusho, itabd niset my phone keyboard in Arabic fonts.
Naam Fanya hivyo maana kuna watu wakiyasoma hayo maneno wataya tamka tofauti hili linapelekea maana ya Quran kubalika

ﺍﻟﻠﻪ ﻳﺒﺎﺭﻙ ﻓﻴﻚ
Ahsante sana kwa ukumbusho, itabd niset my phone keyboard in Arabic fonts.
 
JE FUNGA INASWIHI IKIWA MTU HASWALI?

Uzuri ni kwamba dini ya kiislamu imekamilika kila kitu kiko wazi katika quran na sunnah

Na Mtume( s.w.a ) alisema hivyo ametuacha mahali peupe kabisa, ambapo haina haja ya kutafuta tochi kuanza kumulika jambo fulan kuhusu dini yetu tukaacha quran na sunnah

Jambo la kwanza tutakaloulizwa siku ya kiyama ni swala!!
hivyo kama swala haipo sawa basi amali zako zingine zinazofata zaweza zikawa povu lilopotea tujitahidi na kusimamisha swala ndugu zangu!!

Mtume (s.a.w ) anasema ''kinachotenganisha uislamu na kufru ni kuacha sala''

swala ndiyo nguzo kubwa ya dini hayo mengine yanafuatia, tofauti yetu sisi na wao ni swala hayo mengine hata wao wanafanya kufunga kuhiji n.k

KUFUNGA NA KUACHA SWALA NI DALILI YA UNAFKI SABABU UNACHAGUA KIPI UFANYE KIPI UACHE

Mara ya kwanza Mtume (s.a.w)anapewa swala alipewa vipindi 50
Na falsafa iliyopo hapo ni ili kutuonyesha, Allah(s.w.) ametuleta duniani si kwa jambo lingine lolote isipokuwa IBADA
IBADA ndiyo njia pekee alotuwekea Allah(s.w) kufikia mafanikio ustawi na furaha

Mtume(saw)alikuwa akiswali mpaka miguu inavimba mimi na wewe kujihalalishia kufunga na tunaacha sala ni kujidanganya

(Q 2.283) ''enyi mlioamini mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachamungu''
''ILI MUWE WACHAMUNGU'' sasa mwisho wa ramadhani jifanyie mwenyewe self assessment je ramadhani imenisaidia kuwa Mchamungu? nimeacha uwongo? nimeacha wizi? Nimeacha zinaa? Nimeacha pombe? Nimeacha riba?

Japokuwa kuna changamoto tele kutokana na mazingira ya makazini kwetu, vyuoni kwetu majumbani kwetu, ndugu zetu marafiki zetu n.k ila wakati sasa wa kupambana kuisimamisha haki, usiyumbishwe na chochote UISLAMU NDIYO DINI YA HAKI FUATA MAFUNDISHO YAKE NA MAAMRISHO YAKE ILI UPATE MWISHO MWEMA HAPA DUNIANI. HUJUI KIFO CHAKO KIPO LEO KESHO AU YAWEZEKANA RAMADHANI IJAYO IKAKUKUTA KABURINI.

Imani haiombwi imani inatafutwa kisha uhifadhiwa moyoni na huimarika kwa kufanya vitendo vizuri vya kumridhisha Allah (s.w)

Kama mimi na wewe tulikuwa hatusimamishi swala ndio mda muafaka wa kuamka usiku kuomba ''taubatan nasuha '' il mungu atusamehe na kisha tuweke nia ya kuendelea na yale mazuri yote ya kumpendeza Allah(s.w) ambayo tunayaanza mda huu kuelekea Ramadhan, na tuanze leo ndugu yangu wala tusisubiri kesho,wakati ni sasa
Mtume(s.w) anatushauri tuwe na pupa/haraka katika kuyaendea mambo ya kheri na subra katika mitihani/kuyaendea maovu

Na unapoamua kuyafanya ya Mungu (s.w) tegemea mitihan yakila aina ila cha muhimu uwe na msimamo KWANI NI BORA YAHARIBIKE YAKO ILA USIYAHARIBU(AMRI) YA MUNGU(S.W) NA IKIWA HUTAYAHARIBU YA MUNGU(S.W) JUA YA KWAMBA YAKWAKO PIA KAMWE HAYATAHARIBIKA

''Kumbusha hakika ukumbusho huwafaa wenye kuamini'' (51:5)
Wabillah tawfiq
 
SWALI



nilimskia sheikh mmoja katika kipindi cha televisheni anasema kwamba haiwezekani watu wote duniani kupata sikukuu siku moja kwa sababu kuna nchi zimepishana kwa takribani masaa 24,na kutoa mfano kwamba, Honolulu Marekani jumamosi saa 3 asubuhi, New Zealand ni saa 2 asubuhi Ijumaa. je hii ni kweli na kweli inawezekana ikawa ni sababu ya kutowezekana kufunga na kufungua siku moja dunia nzima??



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Ni kweli kuwa zipo sehemu ambazo zimetofautiana kwa masaa takriban 23 kama ulivyosikia lakini huyo shekhe kachanganya baina ya sehemu. Jua linachomoza Wellington, New Zealand mwanzo kabla ya Hawaii – Honolulu, USA, yaani ikiwa New Zealand ni saa mbili siku ya Ijumaa, Honolulu itakuwa Alkhamisi saa tatu asubuhi. Hata hivyo tofauti hiyo si sababu kabisa kwa Waislamu duniani kutofunga na kutofungua pamoja.

Ni hakika isiyopingika kabisa kuwa kuanzia wakati ambao mawasiliano yamekuwa ni sahali kupatikana kote duniani mwezi umekuwa ukionekana Mashariki ya kati. Na kwa sasa kama katika nchi ya Tanzania na Kenya baada ya Waislamu kuchukua umuhimu mkubwa wa kuangalia mwezi ukawa mwandamo wa sehemu hii unakwenda sambamba na ule wa Mashariki ya Kati. Tufahamu kuwa tofauti baina ya sehemu hiyo na sehemu za Mashariki na magharibi ya ulimwengu haizidi masaa 12. Hakika mazungumzo hayo ni watu tu kutafuta vizisababu visivyokuwa na msingi wowote wa kidini.



Ni ajabu kuwa mashekhe hao wamejikita kuzungumza kuhusu mwezi wa kimataifa pekee wala huwasikii kuzungumza matatizo ya rai kama:

1. Kuzingatia mipaka ya kila nchi.

2. Kuzingatia umbali wa farsakh 24.

3. Kuzingatia masafa ya qasri.

4. Kuzingatia tofauti za matlai.

5. Kuzingatia usawa wa bahari (sea level).

6. Kuzingatia maeneo ya mashariki na magharibi.

7. Kuzingatia kusadifu.



Kila moja katika hizo ni rai ya wanazuoni kuhusu kufuatwa kwa mwezi lakini rai kama hizi huwa tunafichwa. Hata inapozungumziwa rai ya mwandamo wa kitaifa huwa haiwekwi katika mizani kupimwa kama inavyopimwa rai ya kimataifa. Swali la kujiuliza kila Muislamu kwa kirahisi kabisa: “Je, katika ulimwengu wetu huu tuna miezi (wingi wa mwezi - moon) mingapi?”

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:



Kuandama Mwezi – Afuate Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?

Kuonekana Kwa Mwezi Mwandamo Sehemu Tofauti Na Kuanza Funga

Kufuata Mwezi Wa Kitaifa Au Wa Kimataifa; Kupishana Masaa; Wazee Zamani Walikuwa Wanapataje Habari Kuhusu Mwezi Wa Kimataifa

Utata wa Kufunga Swawm na Kufungua Kutokana Na Kutofautiana Kuhusu Mwandamo Wa Mwezi

Ni Sawa Kumfuata Mume Kwa Msimamo Wa Mwezi Wa Kitaifa Japokuwa Alikuwa Akifuata Unapoonekana Popote Duniani?

Nilifunga Na Waliochelewa Kufunga Nikasafiri Kwa Wale Waliwahi Kufunga Nao Kwao Ni Siku Ya ‘Iyd, Je, Niendelee Kufunga?

Tunaambiwa Wanaofuata Mwezi Wa Kimataifa Wamekosea Na Walipe Swawm Je, Ni Sawa?Mwandamo Wa Mwezi, Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?

Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu Je, Tulipe Siku Hiyo?



Na Allaah Anajua zaidi
 
Huwa tunasikia vyeo vya viongozi mbalimbali wa kiislam kwa level za kitaifa, kama kadh/shekh mkuu, ayatollah (supreme leader) nk. Hivi viongozi wakuu wa level ya dunia wapo? Kiongozi wa mashia duniani cheo chake kina jina gani? Au kiongozi mkuu wa dhehebu la sunni duniani yuko na jina la wadhifa wake ni lipi?

Je kuna tofauti kati ya kafir na mshirikina? Unapo futurisha watu gani wanaqualify kufuturisha?

Na washawasha!
 
_Enyi Waislamu, vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume, basi haujafika tu wakati wa kukaa kitako na kuipangia mikakati Ramadhaan iliyopo njiani? Imeshafika mlangoni na inabisha hodi kwa nguvu zote, basi ifungulieni mlango na muitandikie zulia la upendo na ukarimu._

_Huo ndio mwezi wa Ramadhaan ambao ndani yake kuna fadhila nyingi na matunda yake mtakuja kuyaona mbele ya Muumba._

_Kuna mazingatio makubwa katika Swawm hapa duniani kama vile kujua hali za masikini, kulikausha tumbo na kulifanya kuwa na afya zaidi na mengineyo zaidi._

_Halikadhalika, kuna mazingatio ya kwamba tendo hili halijulikani malipo yake hata kwa Malaaikah, kwani Allaah {{سبحانه وتعالى}}_

_Amewahakikishia kwamba ni Yeye tu Ndiye Atayekwenda kuilipa kwa haki inayotakiwa kulipwa. Kwa sababu funga ni ‘ibaadah ya siri kabisa baina ya mja na Mola wake, hakuna mwanaadamu anayeweza kututhibitishia kwamba fulani amefunga au vyenginevyo._

*Amesema Mtume Muhammad صل الله عليه وسلم*

يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: الصَّوْمُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ، يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَأَكْلَهُ وَشُرْبَهُ مِنْ أَجْلِي، وَالصَّوْمُ جُنَّةٌ وَلِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ، فَرْحَةٌ حِينَ يُفْطِرُ وَفَرْحَةٌ حِينَ يَلْقَى رَبَّهُ، وَلَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ {}البخاري و مسلم و مالك والترمذي والنسائي وابن ماجه{}.

*Allah Aliyetukuka na Jalali Anasema:*

_*Swawm ni Yangu na ni Mimi ndiye ninayelipa. {{Mtu}} huacha matamanio yake, chakula chake, kinywaji chake kwa ajili Yangu. Swawm ni ngao, na yule anayefunga ana furaha mbili; Furaha anapofuturu na furaha anapokutana na Mola wake. Mbadiliko wa harufu ya pumzi zake {{kutoka mdomoni}} ni bora kwa Allaah kuliko harufu ya misk.*_

[Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, At-Tirmdihiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

_Tena kwa utaratibu na ustaarabu wake, mgeni huyu hafiki kwako kuigonga milango yenu bila ya kuwaletea taarifa. Daima anawaletea ujumbe wake kwamba atakuja kukutembelea, anazielewa silka na tamaduni za ugeni._

_Ameshaondoka tarishi wake Rajab na karibuni ataondoka mjumbe mwenziwe Sha’abaan, ili kumpisha mgeni Mkarimu Ramadhaan._

_Basi ninawanasihi mumfungulie mlango kwa tabasamu kubwa na huku mioyo yenu ikiwa wazi kwa faraja pamoja na kupokea mafunzo yote atakayokuachia nayo._

_Itakuwa ni hasara kubwa kumkimbia Ramadhaan ukajitia shughuli na uziwi hadi kushindwa hata kumfungulia mlango nyumbani kwako na moyoni mwako._

_Hivyo, jitahidini kwa ukarimu wake Ramadhaan kuwa ni sababu ya kuondolewa katika usajili wa watu wa Motoni._

*Allah {{سبحانه وتعالى}} Atukinge na adhabu hiyo.*

*Aamiyn*
 
Huwa tunasikia vyeo vya viongozi mbalimbali wa kiislam kwa level za kitaifa, kama kadh/shekh mkuu, ayatollah (supreme leader) nk. Hivi viongozi wakuu wa level ya dunia wapo? Kiongozi wa mashia duniani cheo chake kina jina gani? Au kiongozi mkuu wa dhehebu la sunni duniani yuko na jina la wadhifa wake ni lipi?

Je kuna tofauti kati ya kafir na mshirikina? Unapo futurisha watu gani wanaqualify kufuturisha?

Na washawasha!
Kiongozi wa Shia ni, Ayatollah (kiajemi: آيت الله, kiar.: آية الله ayatu 'llah - "alama ya Allah/Mungu") ni cheo cha kiongozi wa kidini katika Uislamu wa Shia hasa nchini Uajemi na pia Iraq.

Kiongozi wa Sunni, baada ya kifo cha Mtume (S.A.W), vifo vya Maswahaba (R.A) na vifo vya Makhalifa, hapajatokea kiongozi mkubwa mwingine zaidi ya Sheikh. (WANAOJUA WATAKUJA KUFAFANUA ZAIDI)
 
Kiongozi wa Shia ni, Ayatollah (kiajemi: آيت الله, kiar.: آية الله ayatu 'llah - "alama ya Allah/Mungu") ni cheo cha kiongozi wa kidini katika Uislamu wa Shia hasa nchini Uajemi na pia Iraq.

Kiongozi wa Sunni, baada ya kifo cha Mtume (S.A.W), vifo vya Maswahaba (R.A) na vifo vya Makhalifa, hapajatokea kiongozi mkubwa mwingine zaidi ya Sheikh. (WANAOJUA WATAKUJA KUFAFANUA ZAIDI)
Ivi kwani Mashia ni Waislamu?
 
Huwa tunasikia vyeo vya viongozi mbalimbali wa kiislam kwa level za kitaifa, kama kadh/shekh mkuu, ayatollah (supreme leader) nk. Hivi viongozi wakuu wa level ya dunia wapo? Kiongozi wa mashia duniani cheo chake kina jina gani? Au kiongozi mkuu wa dhehebu la sunni duniani yuko na jina la wadhifa wake ni lipi?

Je kuna tofauti kati ya kafir na mshirikina? Unapo futurisha watu gani wanaqualify kufuturisha?

Na washawasha!
Tofauti kati ya Kafir na Mshirikina,
Kafir ni yule anayezikufuru neema za Allah,
Mshirikina ni yule anayemshirikisha Allah na viumbe wengine,

kwa haraka haraka unaweza usione tofauti zao watu hawa wawili,
turejee kwenye Qur'an Allah (S.W) anasemaje.

((لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُواْ إِنَّ اللّهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُواْ اللّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ))


((لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُواْ إِنَّ اللّهَ ثَالِثُ ثَلاَثَةٍ وَمَا مِنْ إِلَهٍ إِلاَّ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَإِن لَّمْ يَنتَهُواْ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ))



((Hakika wamekufuru waliosema: Allaah ni Masiyh mwana wa Maryam! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Allaah, Mola wangu na Mola wenu . Kwani anayemshirikisha Allaah, hakika Allaah Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru))



((Kwa hakika wamekufuru waliosema: Allaah ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna muabudiwa wa haki ila Muabudiwa wa Haki Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayoyasema, kwa yakini itawakamata adhabu iumizayo wale wanaokufuru)) [Al-Maaidah: 72-73]

Wote hao wamekufuru kwa kumpa kiumbe mwingine haki ya Mungu, yaani Kafir akisema Mungu ni wa tatu wa utatu maana yake kua Mungu amegawanyika makundi matatu wakati tunajua kua Mungu ni mmoja, hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana mshirika wake.

Mshirikina yeye anaweza kua Muislam lakini akawa mchawi, au mpiga ramli au akenda makaburini kumlilia maiti amsaidie katika jambo lake analoliona yeye yule mfu atamfaa, huo ni ushirikina wa hali ya juu, wa kustahiki kuombwa ni Allah pekee kwani yeye ndio ametuumba na anayajua yote ya siri na ya dhahiri.
 
Back
Top Bottom