Assalaam Alaykum
Ndugu zangu Waislam
Allah awabaarik sana popote mlipo
TANBIH FUPI
Mwezi huu wa Rajab,ni Katika Miezi Mitukufu
Ila Baadhi ya Watu wanaojiita ni Masheikh,Wanawafundisha Watu na kuwasisitiza kuhusu kufanya Ibada mbalimbali katika miongoni mwa Ibada za Sunna
Jambo ambalo si sahihi kisheria
Hakuna Ibada Maalum ndani ya mwezi huu(Rajab),ambayo Mtume wa Allah Sala na Salamu ziwe juu yake ametufundisha
Bali
Ibada nyingi watu wamezua ndani ya Mwezi huu
Kuna Watu
Wanafanya Umra ndani ya mwezi huu(Rajab)Wakidhani kufanya hivi,wanapata Ujira zaidi
Kuna Watu
Wanaswali swala maalum( صلاة الرغائب)ambayo haina asili katika Dini yetu
Kuna watu
Wanafanya Ibada maalum usiku wa Nusu Rajab( صلاة النصف من رجب ),Hili nalo halina asili katika Sheria yetu tukufu
Kuna Watu
Wanaswali tarehe 27,na kusema ndio siku ya Miiraaj( صلاة ليلة المعراج ),Hili nalo halipo katika Dini
Kiujumla
Meengi yamezushwa na Watu kwa ujinga au kwalengo ambalo wao wanajua zaidi
Ikhwah
Tuwe makini sana ndani ya Miezi hii
Tusomeni Dini yetu,ili tujue yaliyosahihi kisheria
Shukran sana
جزاكم الله خيرا
Sent using
Jamii Forums mobile app