Ramadhani Bakari Iddi ahukumiwa jela maisha kwa kulawiti mtoto

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Mahakama ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imemuhukumu kwenda jela kifungo cha maisha Ramadhani Bakari Iddi (46) mkazi wa Kilapula kata ya Ngomeni Wilayani hapo kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo hii Hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya hiyo Mh. Geofrey Haule amesema kwamba mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo kwakuwa mnamo tarehe 08/11/2023 mshtakiwa alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo pindi alipomlubuni na kisha kwenda naye makaburini kwa lengo la kumtoa mashetani ndipo akafanya kitendo hicho cha kinyama kwa dhamira ovu.

Amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hivyo mahakama imejiridhisha pasi na shaka kuwa mshtakiwa ndio mtenda kosa hilo hivyo Mahakama inamuhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha maisha Jela ili iwe fundisho katika jamii.

Aidha hakimu Haule amesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kifungu cha sheria 154 (1)(a) na 2 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 RE.2022.

Awali baada ya hukumu hiyo kutolewa wakizungumza kwa nyakati tofauti waendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Muheza Inspector Joseph Njama na CPL Michael Msangawale waliishukuru Mahakama kwa kutoa adhabu hiyo kali kwa mtuhumiwa huyo na huku wakiongeza kusema kuwa inaenda kuwa fundisho kwa wale wote wenye nia ovu ya kutenda makosa hayo katika jamii na Taifa kwa Ujumla.

1716528045666.png
 
Sijui huwa ni akil gan inayopelekea mtu kuwaza kulawiti mtoto,too bad indeed!
 
View attachment 2997895
Huyu wangelimrudisha kwa wananchi wakamchana vipande vipapnde. Huko anakwenda kulawiti zaidi
 
Watoto hawako salama hata kidogo, waelimishwe watoto wakiwa wadogo wajue kila kitu.

Hapa mtaani kuna tukio limetokea la kusikitisha sana. Mtoto wa miaka 5 wa kiume siku moja eti mama yake kaona anapita kwa kasi anakimbilia choo ya nje kabla hajafika chooni, choo hiyo imetoka mama yake akamuuliza una shida gani mbona unajinyea mtoto hakuongea ukweli siku hiyo ikapita.

Siku nyingine wakati anamfulia nguo akakuta tena nguo ni chafu.

Siku nyingine akamuita amuogeshe mtoto akawa anagoma mama yake akamlazimisha, mara akastuka kwa nini mtoto hayuko huru kuogeshwa, kumuangalia vizuri mtoto aliishaharibiwa sana piga mtoto pìgaaa akamtaja kijana wa jirani anasoma darasa la 7 kuwa ndo anawafanyia huo ujinga.

Mtoto wakambana akataja na wengine jumla ni watoto 6, police wakaitwa vitoto vyote wakavipekeka kituoni wavihoji vizuri.
Hadi huruma mtoto anaeleza eti huyo wa darasa la 7 alisema wakimtaja atawagaya, eti siku nyingine aliwaambia wakisema atawachoma kisu.

Wakawauliza mnafanyia wapi? Vikajibu eti kutitoka shule tunapitia kule chini kwenye ka kichaka dah.

Mkubwa wa darasa la 7 ana miaka 13 , mwingine ana miaka 8 viwili vina miaka 5, yaani wote 6 wako chini ya miaka 13.

Huruma kimoja kilisema eti kikiwashwa ndo kinalazimika kumfata huyo mkubwa kimbembeleze aki... dah eti wakati mwingine wanafanyia kwao ndani, yaani ni uzuni.
Basi wakavipeleka hospital matibabu yakaanza.
Nasikia huyo mkubwa atachukuliwa hatua.

Wazazi ongea na mwanao akiwa mdogo, hali ni ngumu, muweke wazi.
 
Back
Top Bottom