sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Kuna "kiumbe" anawasumbua vilivyo mabeki wa ligi daraja la kwanza [SDL] na Kombe la Shirikisho kwa sasa.. Yaani jamaa anatupia anapojisikia tu.. Hakuna wa kumzuia.. Kiumbe huyu si mwingine bali ni Ramadhani Kipalamoto.
Mpaka sasa katupia goli 4 katika mechi 1 tu ya Kombe la Shirikisho.. Pia katupia goli 1 katika mechi 1 ya ligi daraja la kwanza.. Hivyo katika mechi 2 tu alizocheza msimu huu.. ana wastani wa goli 3 [hat-trick] kwa kila mechi.. Maajabu yaliyoje..😳😳
Ramadhani Kipalamoto ni nani Haswaa??
1. Kipaji chake kiliibuliwa mnamo mwaka 2011.. na jopo la makocha bora kabisa wa Simba B.. Na katika mwaka huo huo aliisaidia Simba B kuchukua ubingwa wa Uhai Cup
2. Mwaka 2012, Ramadhani Kipalamoto alikua katika kiwango bora kabisa.. Ambapo aliiwezesha Simba B kuwa mshindi wa 3 wa Uhai Cup.. huku yeye akiwa mfungaji bora
3. Mwaka 2013 Ramadhani Kipalamoto alisajiliwa rasmi na kua mchezaji wa Kikosi cha Kwanza.. na hii ilikua ni katika dirisha dogo la usajili.
4. Mwaka huo huo, Ramadhani Kipalamoto alipata nafasi ya kucheza Kikosi cha kwanza.. Na katika mechi ya kwanza aliyoingia uwanjani.. alitupia kambani goli 1.. na hii ilikua dhidi ya Toto jijini Mwanza.
5. Msimu wa 2014/2015 haukua mzuri kwake, na ikapelekewa kujiweka pembeni Simba S.C.
6. Mwaka 2015 vijana wa Abajalo F.C toka mitaa ya Sinza.. Wakaona kwanini hii "almasi" inazagaa zagaa mchangani.. tena mchanga wenyewe wa pembeni ya barabara ya lami?? Wakampa mkataba fasta.
Sasa Jamaa Anatupia Tu.
Baada ya performance ya kiwango cha dunia anayoonesha Ramadhani Kipalamoto kwa sasa, imenifanya niwakumbuke "washikaji" zake aliokua nao Simba B kuanzia miaka ya 2011 kama vile....
Manyika Jr.. Edward Christopher.. Hassan Isihaka.. Jonas Mkude.. Rashid Ismail.. Said Ndemla.. Abuu Hashim.. William Lucian "Gallas".. Hassan Hatibu.. Haroun Chanongo.. Ramadhan Singano.. Ibrahim Ajibu.. Miraj Athuman.. Rahimu Juma Abdalah n.k
Nachokiona.. kuna kabati la ziada lazima lingeongezwa pale Msimbazi kwa ajili ya kuhifadhi makombe ya Kimataifa.. kama hawa vijana wangeendelea kuwa pamoja.
Wahenguzi walishanena .. Ukijua.. Umejua tu.. Pia wakaenda mbali.. Kupotea njia.. Ndo kujua njia.
Naamini Kocha Mtalaamu wa Simba B.. "Fundi" Kiondo.. atakua..
...Kashaoneshwa shamba tunalolitumia kuwavuna kina Ramadhani Kipalamoto.. Na sasa yupo anavuna.
...Pia atakua makini na njia atakapokua anarudi toka Shambani.. Ili asije akapotea.