Ramadhani Kipalamoto: Kanifanya niikumbuke Golden Generation toka Simba B

Ramadhani Kipalamoto: Kanifanya niikumbuke Golden Generation toka Simba B

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Kuna "kiumbe" anawasumbua vilivyo mabeki wa ligi daraja la kwanza [SDL] na Kombe la Shirikisho kwa sasa.. Yaani jamaa anatupia anapojisikia tu.. Hakuna wa kumzuia.. Kiumbe huyu si mwingine bali ni Ramadhani Kipalamoto.

Mpaka sasa katupia goli 4 katika mechi 1 tu ya Kombe la Shirikisho.. Pia katupia goli 1 katika mechi 1 ya ligi daraja la kwanza.. Hivyo katika mechi 2 tu alizocheza msimu huu.. ana wastani wa goli 3 [hat-trick] kwa kila mechi.. Maajabu yaliyoje..😳😳

Ramadhani Kipalamoto ni nani Haswaa??

1. Kipaji chake kiliibuliwa mnamo mwaka 2011.. na jopo la makocha bora kabisa wa Simba B.. Na katika mwaka huo huo aliisaidia Simba B kuchukua ubingwa wa Uhai Cup

2. Mwaka 2012, Ramadhani Kipalamoto alikua katika kiwango bora kabisa.. Ambapo aliiwezesha Simba B kuwa mshindi wa 3 wa Uhai Cup.. huku yeye akiwa mfungaji bora

3. Mwaka 2013 Ramadhani Kipalamoto alisajiliwa rasmi na kua mchezaji wa Kikosi cha Kwanza.. na hii ilikua ni katika dirisha dogo la usajili.

4. Mwaka huo huo, Ramadhani Kipalamoto alipata nafasi ya kucheza Kikosi cha kwanza.. Na katika mechi ya kwanza aliyoingia uwanjani.. alitupia kambani goli 1.. na hii ilikua dhidi ya Toto jijini Mwanza.

5. Msimu wa 2014/2015 haukua mzuri kwake, na ikapelekewa kujiweka pembeni Simba S.C.

6. Mwaka 2015 vijana wa Abajalo F.C toka mitaa ya Sinza.. Wakaona kwanini hii "almasi" inazagaa zagaa mchangani.. tena mchanga wenyewe wa pembeni ya barabara ya lami?? Wakampa mkataba fasta.
Sasa Jamaa Anatupia Tu.

Baada ya performance ya kiwango cha dunia anayoonesha Ramadhani Kipalamoto kwa sasa, imenifanya niwakumbuke "washikaji" zake aliokua nao Simba B kuanzia miaka ya 2011 kama vile....

Manyika Jr.. Edward Christopher.. Hassan Isihaka.. Jonas Mkude.. Rashid Ismail.. Said Ndemla.. Abuu Hashim.. William Lucian "Gallas".. Hassan Hatibu.. Haroun Chanongo.. Ramadhan Singano.. Ibrahim Ajibu.. Miraj Athuman.. Rahimu Juma Abdalah n.k

Nachokiona.. kuna kabati la ziada lazima lingeongezwa pale Msimbazi kwa ajili ya kuhifadhi makombe ya Kimataifa.. kama hawa vijana wangeendelea kuwa pamoja.

Wahenguzi walishanena .. Ukijua.. Umejua tu.. Pia wakaenda mbali.. Kupotea njia.. Ndo kujua njia.

Naamini Kocha Mtalaamu wa Simba B.. "Fundi" Kiondo.. atakua..
...Kashaoneshwa shamba tunalolitumia kuwavuna kina Ramadhani Kipalamoto.. Na sasa yupo anavuna.
...Pia atakua makini na njia atakapokua anarudi toka Shambani.. Ili asije akapotea.
 
sembo sidhani kama manyika jr alikuwapo ktk hiyo generation... Nakumbuka kipa alikua dogo flan hivi anaitwa hashim
 
Last edited by a moderator:
Hiki kizazi si ndicho kimeipoteza Simba katika ramani ya soka kwa miaka minne sasa!
 
sembo sidhani kama manyika jr alikuwapo ktk hiyo generation... Nakumbuka kipa alikua dogo flan hivi anaitwa hashim

Uko sahihi kabisa.. Kumbukumbu zangu zinaonesha Manyika Jr.. kajiunga mwaka 2014 Simba S.C kama memba wa Simba B.. ambapo kile "kizazi cha dhahabu" kilikua kikiishia.
Na hapa Mkuu nazungumzia Generation ya Simba B toka mwaka 2010.
 
Last edited by a moderator:
Hiki kizazi si ndicho kimeipoteza Simba katika ramani ya soka kwa miaka minne sasa!

Hapana Mkuu.. Sababu za Simba kupotea katika ramani, zipo nyingi ila hii ya kizazi hiki cha dhahabu.. HAIPO.

Kosa lililofanyika ni jinsi ya walivyokua wakiwa integrate katika 1st eleven.. Haiwezekani uingize U-20 zaidi ya 5 katika 1st eleven.. Huku wengine wakitokea benchi.

Hapa wa kumlaumu ni Kocha na si hawa Golden Boyz.
 
Kuna dogo flani hivi anaitwa Athumani miraji a.k.a shevchenko yupo toto africans... Dogo hatari sana inabidi simba imrudishe kundini nayeye alikua simba B
 
Hapana Mkuu.. Sababu za Simba kupotea katika ramani, zipo nyingi ila hii ya kizazi hiki cha dhahabu.. HAIPO.

Kosa lililofanyika ni jinsi ya walivyokua wakiwa integrate katika 1st eleven.. Haiwezekani uingize U-20 zaidi ya 5 katika 1st eleven.. Huku wengine wakitokea benchi.

Hapa wa kumlaumu ni Kocha na si hawa Golden Boyz.

Sawa Mkuu.
 
Kwa kukuongezea tu wengine ambao hujawataja ni pamoja na: Abdallah Seseme kiungo bora kabisa, Frank Sekule, Miraji Adam.
 
Kweli Mbumbumbu FC aliewaroga kafa,timu ya wakubwa Jahazi linazama badala ya kufanya juhudi kuiokoa mnajadili timu B,kweli Yanga wacha iitwe Yanga tuu.
 
Kweli Mbumbumbu FC aliewaroga kafa,timu ya wakubwa Jahazi linazama badala ya kufanya juhudi kuiokoa mnajadili timu B,kweli Yanga wacha iitwe Yanga tuu.

Kichwa cha Habari... Ramadhan Kipalamoto: Kanifanya niikumbuke Golden Generation toka Simba B

Main Body... Nimemzungumzia Mtalamu Rama Kipalamoto, historia yake kwa ufupi.. Wachezaji aliowahi kucheza nao kipindi yupo Simba B

Nimemamaliza kwa kusema... Wahenguzi walishanena .. Ukijua.. Umejua tu.. Naamini Kocha Mtalaamu wa Simba B, "Fundi" Kiondo.. atakua kashaoneshwa shamba tunalolitumia kuwavuna kina Ramadhani Kipalamoto.. Na sasa yupo anavuna.

Labda Mkuu nikusaidie tu, maana nadhani uwezo wako wa kuelewa vitu hauendani na kasi ya timu yako ikiwa uwanjani.. Nilichokimaanisha katika bandiko langu ni;
1. Kuonesha ni wapi Rama Kipalamoto katokea.. Hadi hapo alipo.
2. Ni mchango gani aliuleta katika timu yangu ya vijana, ambayo ulikua ni chachu kubwa kwa wachezaji wenzake kukaza ili kusogelea kiwango alichokua nacho.
3. Japo tulipotea.. Naamini Kocha mpya wa timu ya vijana aliyekabidhiwa majukumu mwaka huu.. Atafuata nyayo za kina Matola, katika kutuletea kina Rama Kipalamoto wengi zaidi.
 
Watanzania uwa tunajidanganya sana eti golden generation ya mtu kama MKUDE kila siku analewa chakali tabata.
 
Hivi unaweza kuwaita Golden Generation wakati hawajawahi kuipa ubingwa wa ligi ya vodacom ata kuwa wapili washiriki mashindano ya kimataifa acheni kujidanganya na kutumia maneno mazito kwenye hizo takataka zenu.
 
Golden Generation haina mchezaji ata mmoja anacheza kikosi cha kwanza cha national team tena national mbovu mbovu....nyambafuuuuuu.
 
Hapo ndio ameniacha hoi,eti team B ina Golden Generation halafu team ya wakubwa ina Uozo Generation. Ukihoji anakwambia uwepo wako wa akili ni mdogo.
 
Duh!golden generation!maneno mazito mnawabebesha vijana mpaka mpira unawashinda.
 
Watanzania uwa tunajidanganya sana eti golden generation ya mtu kama MKUDE kila siku analewa chakali tabata.

Hivi unaweza kuwaita Golden Generation wakati hawajawahi kuipa ubingwa wa ligi ya vodacom ata kuwa wapili washiriki mashindano ya kimataifa acheni kujidanganya na kutumia maneno mazito kwenye hizo takataka zenu.

Golden Generation haina mchezaji ata mmoja anacheza kikosi cha kwanza cha national team tena national mbovu mbovu....nyambafuuuuuu.

Duh!golden generation!maneno mazito mnawabebesha vijana mpaka mpira unawashinda.

Kwanini ninewaita Golden Generation ya Simba B?

1. Ili kua mchezaji wa timu ya Simba B, ni lazima uwe na umri chini ya miaka 20.. ingawa Mara chache hutokea wenye umri zaidi kuwepo.

2. Tangu Simba ianzishwe haijawahi kua na Kikosi imara.. Narudia tena Kikosi imara cha vijana kama nilichokizungumzia hapo juu.. Hivyo wanadeserve kuitwa Golden Generation ya Simba B.

NOTE: hapa nazungumzia Golden Generation ya Simba B na si timu ya wakubwa.

Nakala: Frank Wanjiru
 
Last edited by a moderator:
Alafu kufanikiwa katika soka la vijana ni jambo moja.. Kuwa successful katika soka la wakubwa au professional ni jambo jingine.

cc Frank Wanjiru guasa MKALIKENYA
 
Last edited by a moderator:
Kwanini ninewaita Golden Generation ya Simba B?

1. Ili kua mchezaji wa timu ya Simba B, ni lazima uwe na umri chini ya miaka 20.. ingawa Mara chache hutokea wenye umri zaidi kuwepo.

2. Tangu Simba ianzishwe haijawahi kua na Kikosi imara.. Narudia tena Kikosi imara cha vijana kama nilichokizungumzia hapo juu.. Hivyo wanadeserve kuitwa Golden Generation ya Simba B.

NOTE: hapa nazungumzia Golden Generation ya Simba B na si timu ya wakubwa.

Nakala: Frank Wanjiru

Baadae hao Golden Generation walienda wapi au walitoweka kwenye ile Ndege ya Malaysia?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom