Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,719
- 40,739
Alafu kufanikiwa katika soka la vijana ni jambo moja.. Kuwa successful katika soka la wakubwa au professional ni jambo jingine.
cc Frank Wanjiru guasa MKALIKENYA
Baadae hao Golden Generation walienda wapi au walitoweka kwenye ile Ndege ya Malaysia?
Kwa hiyo nyie Mbumbumbu fc a.k.a wa mchangani kazi yenu ni kutwanga maji kwenye kinu?
Kwanini ninewaita Golden Generation ya Simba B?
1. Ili kua mchezaji wa timu ya Simba B, ni lazima uwe na umri chini ya miaka 20.. ingawa Mara chache hutokea wenye umri zaidi kuwepo.
2. Tangu Simba ianzishwe haijawahi kua na Kikosi imara.. Narudia tena Kikosi imara cha vijana kama nilichokizungumzia hapo juu.. Hivyo wanadeserve kuitwa Golden Generation ya Simba B.
NOTE: hapa nazungumzia Golden Generation ya Simba B na si timu ya wakubwa.
Nakala: Frank Wanjiru
Na mimi nachokuchallenge kama hiyo ilikuwa golden generation ya Simba B mbona walipopandishwa kwenye timu ya wakubwa hawakupata mafanikio na ata kupata mafanikio binafsi.
Ndo mana nikasema..
Alafu kufanikiwa katika soka la vijana ni jambo moja.. Kuwa successful katika soka la wakubwa au professional ni jambo jingine.
Mfano mmojawapo ni Bojan Krkik.. Alikaa Barcelona B kwa muda wa mwaka mmoja tu.. The moja kwa moja akatupwa 1st eleven iliyojaa mastaa kibao.
Kilichotokea baada ya hapo hakuna anachojua.. Na sasa jamaa yupo Stoke City.. Timu ambayo haishiriki si UEFA wala Europe League.
Mbona unajichanganya aisee sasa ugolden unatokea wapi kama hakuna ata mmoja amepata mafanikio ya kutangazwa kama walipopandishwa hawajafanya chochote cha maana.
Unajua Mkuu unawaaibisha mashabiki wenzako wa Kandambili? Na hii ni kutokana na kuwa mgumu sana kuelewa.
Hapa nazungumzia Kikosi bora kuwahi kutokea katika Simba B.. Sasa hayo ya walipo sasa yanatokea wapi?
Sisi kazi yetu ni kutwanga maji kwenye kinu.
Nyinyi hua mnatwanga nini?
Baadhi ya waliopandishwa toka Golden Generation hadi 1st eleven ya Mnyama ni hawa hapa chini.. Na timu zao wanazocheza kwa sasa katika VPL.
1. Hassan Isihaka - Simba S.C
2. Jonas Mkude - Simba S.C
3. Said Ndemla - Simba S.C
4. Ibrahim Ajibu - Simba S.C
5. Edward Christopher - Toto African
6. William Lucian - Ndanda F.C
7. Haruna Chanongo - Stand United
8. Ramadhan Singano - Azam
9. Miraji Athuman - Toto African
10. Abuu Hashimu - Kagera Sugar
11. Ramadhan Kipalamoto - Abajalo F.C
Ambao walitua Simba B, Golden Generation ikiwa inaishia ishia.. Na timu zao wanazocheza kwa sasa katika VPL.
1. Manyika Jr - Simba S.C
2. Said Issa - Simba S.C
3. Boniphace Maganga - Simba S.C
4. Mubarak Yusuph "Boban" - Kagera Sugar kwa Mkopo
5. Rahim Juma Abdallah Kibaden "zenden" - African Sports
Ukitaka kujua wamefanya nini tangu walipohitimu Simba B... Wanafanya nini hivi sasa.. Mchango wao katika soka la Tanzania.. Je ni wangapi wapo national timu.. Mnaweza mkapitia https://www.google.co.tz/
Nakala: Frank Wanjiru MKALIKENYA
Baadhi ya waliopandishwa toka Golden Generation hadi 1st eleven ya Mnyama ni hawa hapa chini.. Na timu zao wanazocheza kwa sasa katika VPL.
1. Hassan Isihaka - Simba S.C
2. Jonas Mkude - Simba S.C
3. Said Ndemla - Simba S.C
4. Ibrahim Ajibu - Simba S.C
5. Edward Christopher - Toto African
6. William Lucian - Ndanda F.C
7. Haruna Chanongo - Stand United
8. Ramadhan Singano - Azam
9. Miraji Athuman - Toto African
10. Abuu Hashimu - Kagera Sugar
11. Ramadhan Kipalamoto - Abajalo F.C
Ambao walitua Simba B, Golden Generation ikiwa inaishia ishia.. Na timu zao wanazocheza kwa sasa katika VPL.
1. Manyika Jr - Simba S.C
2. Said Issa - Simba S.C
3. Boniphace Maganga - Simba S.C
4. Mubarak Yusuph "Boban" - Kagera Sugar kwa Mkopo
5. Rahim Juma Abdallah Kibaden "zenden" - African Sports
Ukitaka kujua wamefanya nini tangu walipohitimu Simba B... Wanafanya nini hivi sasa.. Mchango wao katika soka la Tanzania.. Je ni wangapi wapo national timu.. Mnaweza mkapitia https://www.google.co.tz/
Nakala: Frank Wanjiru MKALIKENYA
Kaka tumia neno Generation peke yake hivi unajua maana ya neno Golden.
Sembo hakuna mtu anataka kubishana pasipo sababu ya msingi watu wanahitaji uwaambie achievements za hicho kizazi maana dhahabu inajulikana ubora na thamani yake.Barcelona ya kina Messi xavi na iniesta wamekutana wana miaka 12mpaka leo ukiulizwa mafanikio yao utayasema.Sasa hii dhahabu yako ya msimbazi watu wamevutwa na kichwa cha khabari ila maelezo yako ndo maana wana ku challenge.
Haha.. Mkuu tatizo lililopo "raia" wanataka kufananisha Golden Generation ya kama Barcelona au Ajax na hii ya Simba S.C wanasahau kua kufananisha hivi vitu viwili ni sawa, na kufananisha Mbingu na Ardhi.
Kibongo Bongo hii Generation inadeserve kuitwa "Golden one" na huu ni muono wangu.. Siwezi nikawalazimisha waamini nachoamini.
Mkuu Sembo kubali kuwa umeshindwa kutetea hiyo Golden Generation yako ya Kichina,maana hatuyaoni matunda yake kwa Simba.
Sembo watu wanaona umetia chumvi nyingi kukipamba kizazi hicho hilo ndo waungwana wanalikataa kuhusu ubora wanao kiasi chake ila si kwa kiwango unachotaka kuuaminisha mwisho najua weye ni msimbazi damu so mtu kupenda chake sio dhambi ila kumbuka mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo.Ila pamoja sana sembo.