Jumatano, Jan 25, 2023.
Shinyanga mjini, Shinyanga.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Cde Ramadhani Mwishehe Mlao (MNEC) amezungumza na wanachama wa CCM mkoa wa Shinyanga kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika wilaya ya Shinyanga mjini mkoani Shinyanga.
Katika ziara hiyo ya kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM MNEC Mlao ameungana na viongozi wa Uvccm Mkoa wa Shinyanga na wanachama wa chama cha mapinduzi ambapo amepokelewa kwa kishindo kikubwa katika muendelezo wa ziara yake Kanda ya ziwa akitokea Mkoa wa Kagera alipowasili katika ofisi ya CCM Mkoa.
Aidha MNEC MLAO ameshiriki zoezi la upandaji wa miti na kuwaasa wanachama wa CCM na wanashinyanga juu ya utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na hali ya hewa. MNEC MLAO akiwa katika viwanja vya CCM Shinyanga mjini amewasisitiza Vijana kujibu kwa hoja juu ya upotoshaji wowote unaofanywa katika Mambo makubwa yanayofanywa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. SAMIA SULUHU HASSAN Pia MNEC MLAO amewahimiza Vijana kujikita katika kubuni miradi ya kiuchumi hususani kwenye Kilimo ambapo amesema "Mh. Rais anatambua juhudi za vijana wa Mkoa wa Shinyanga na Vijana wa Tanzania kwa Ujumla na kupitia wizara ya Kilimo Rais ametoa fedha ili Vijana wakanufaike na mradi wa BBT-YIA (Building Better Tommorow-Youth Initiative Agribusiness) Kama mradi mahususi wa kuwaingiza Vijana kwenye fursa ya Kilimo chenye tija".
Pia MNEC MLAO amewatembelea watoto wenye uhitaji Maalumu katika shule ya Buhangija na kuwapatia mahitaji mbalimbali na amehahidi kuendelea kufanya hivyo kwani Taifa linawategemea na wao ni sehemu ya Jamii yetu.
MNEC Mlao pia ameweza kutembelea Mashina ya mabalozi, na kupandisha bendera na kuzindua Madarasa ya MAKADA Mkoa wa Kagera, kwa kuzungumza na Maelfu ya Vijana waliofurika katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi na kusisitiza wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwa kinara kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan maana kazi anayoifanya ya kuhakikisha watanzania wote wanapata maendeleo kwenye kila maeneo ni kubwa sana.
Sambamba na hivyo Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na mwenyekiti Cde Clement Madinda umempongeza sana MNEC Mlao kwa kwa kufanya ziara mkoani Shinyanga kwani imeongeza hali na hamasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika kukitumikia na kujitolea husuani katikaJumuiya ya vijana.
#MimiNiNyinyi
Imetolewa na:
NYANDI KABAGASHA
KATIBU WA UVCCM MKOA WA SHINYANGA.