Ramadhani Singano huru kutimkia popote

Hilo lilitakiwa kuwa limefanyiwa kazi kitambo........
 
Katika uamuzi huu, kuna upande umesitiriwa kwa kuwa na mkataba wa kufoji. Siasa za mpira Bongo.
 
Mkataba umevunjwa kwa Simba kupeleka vielelezo dhaifu kuhusu madai ya kutotimzwa kwa bima ya afya na pango la nyumba, ndio kusema kabla haujavunjwa mkataba ulikuwepo.

Mkataba unavunjika pale upande mmoja unashindwa kutimiza vipengele vya makubaliano (contract recision due to non-performance of agreement). Kwa kuwa Simba walishindwa kutimiza vipengele hivyo vya bima na pango la nyumba, kwa upande wao TFF walitangaza tu kuwa Messi hana mkataba tena na Simba.

Maamuzi hayo hayo yalimpeleka mchezaji Emmanuel Okwi katika klabu ya Simba ikidaiwa kuwa Yanga ilishindwa kutekeleza kipengele cha kumlipa fedha yake ya usajili hivyo TFF ika-declare tu kuwa Okwi hakuwa na mkataba tena na Yanga. Uamuzi wa TFF wa Okwi kwenda Simba ulipongezwa sana na wanachama, wapenzi na wadau wa mikia. Kwa kuwa uamuzi wa kumuweka huru Messi umechukuliwa katika mazingira yale yale yaliyomnyofoa Okwi kutoka Yanga kwenda Simba, ni matumaini yangu kuwa uamuzi huu unastahili kupongezwa pia na wadau wa Simba; maana ni uamuzi wa haki.
 

Mimi ni mmoja kati ya wanaopongeza haki kutawala mahali popote. Kwa kuwa Simba wameshindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba maana yake mkataba umekufa rasmi. Japokuwa wadau baadhi hawakuubali uamuzi ule wa Okwi kwenda Simba, itashangaza kama wanaweza kushangilia leo maamuzi haya ambayo ni ktk mazingira yaleyale.
Itawalazimu kukubali kwanza mazingira yale ya mkataba wa Okwi na Yanga kuvunjika ili wawe na 'guts' za kupongeza hili la Messi na Simba. Huu ndio uungwana na busara.

Lkn dogo huyu kabla alisema mkataba umefojiwa, kitu ambacho Simba walipinga vikali. Hadi sasa TFF haijasema upi ulikuwa ni mkataba halali, lkn kwa kusema kuwa mkataba umevunjika ina maana kumbe ulikuwepo in the first place. Sijajua ni kwa nini hili la ni upi mkataba uliovunjwa, wa miaka 2 au 3 halijafumbuliwa na TFF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…