Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na aliyefoji mkataba kutoka miaka 2 kuwa 3 kapewa adhabu gani?
Funika kombe mwanaharamu apite.
Mkataba umevunjwa kwa Simba kupeleka vielelezo dhaifu kuhusu madai ya kutotimzwa kwa bima ya afya na pango la nyumba, ndio kusema kabla haujavunjwa mkataba ulikuwepo.
Mkataba unavunjika pale upande mmoja unashindwa kutimiza vipengele vya makubaliano (contract recision due to non-performance of agreement). Kwa kuwa Simba walishindwa kutimiza vipengele hivyo vya bima na pango la nyumba, kwa upande wao TFF walitangaza tu kuwa Messi hana mkataba tena na Simba.
Maamuzi hayo hayo yalimpeleka mchezaji Emmanuel Okwi katika klabu ya Simba ikidaiwa kuwa Yanga ilishindwa kutekeleza kipengele cha kumlipa fedha yake ya usajili hivyo TFF ika-declare tu kuwa Okwi hakuwa na mkataba tena na Yanga. Uamuzi wa TFF wa Okwi kwenda Simba ulipongezwa sana na wanachama, wapenzi na wadau wa mikia. Kwa kuwa uamuzi wa kumuweka huru Messi umechukuliwa katika mazingira yale yale yaliyomnyofoa Okwi kutoka Yanga kwenda Simba, ni matumaini yangu kuwa uamuzi huu unastahili kupongezwa pia na wadau wa Simba; maana ni uamuzi wa haki.