Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kwa sehemu zenye asili ya maji maji, unaweza ukatumia zege kavu kudhibiti maji kupanda juu. Katika hiyo zege unaweka maji kidogo sana (wengine hawaweki kabisa) na kwenda kulimwaga sehemu husika, zege litakuwa linafyonza maji kidogo kidogo kwa sababu halina maji ya kutosha na baadae litaanza kukomaa taratibu taratibu, kadri maji yanavyopanda ndio itakuwa inaikomaza zaidi (inakuwa kama mtu anayemwagilia, CONCRETE CURING).

Hapo maji hayatopanda tena juu labda itokee mahali kwenye hiyo zege kukawa na nyufa au kitobo, kama utaweka zile expansion joint basi hakikisha unaziba na zile gundi maalum ambazo water proof

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
 
Moja ya mbinu za kupunguza gharama katika ujengaji wa msingi ni kutumia tofali za nchi 6 badala ya tofali za nchi 5

Kwa kuwa katika msingi tofali zake huwa zinalazwa hivyo ukitumia tofali za nchi 6 utajenga mistari michache tofauti na ukitumia tofali za nchi 5

Tuchukulie mfano msingi wako una mita 1.4 (beam excluded) (nimechukua 1.4m kwa sababu inagawanyika kwa 175mm na 200mm bila kubaki, kiuhalisia nyumba za kawaida msingi huwa ni futi 2 mpaka 3 au na zaidi kutegemeana na slope ya eneo)

Kama utatumia tofali za nchi 6 utajenga mistari 7 (150mm ya tofali + 50mm ya udongo =200mm)

Na kama utatumia tofali za nchi 5 utajenga mistari 8 (125mm ya tofali + 50mm ya udongo= 175mm)

Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 6 itakuwa 50x7×1100 = Tsh 385,000/=

Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 5 itakuwa 50x8×1000 = Tsh 400,000/=

NB: Unene wa udongo nimechukua 50mm ili mahesabu yawe rahisi

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa tuwasiliane
Madini haya
 
Speed ya kazi hutegemea na vitu vingi, leo nitaelezea kitu kimoja (mpangilio/upangaji wa material ktk site)

1. Tofali
Kama site inafikika vizuri bila shida, basi tofali zako zishushe pande zote nne za site. Hii itasaidia mbebaji asitembee umbali mrefu kufata tofali mahali zilipo na kupeleka upande ambao hamna tofali (hazikushushwa).

2. Mchanga na Kokoto
Hivi vinatakiwa vishushwe karibu sana na mahali ambapo utakuwa unachanganyia udongo ama zege, hii itapunguza ule muda wa wabebaji kutembea kufata hayo material na kuleta sehemu ya kuchanganyia.

Sehemu ya kuchanganyia (sahani) iwe angalau mita 3 kutokea mahali jengo liliposetiwa...itafanya idadi ya trip za kupeleka udongo/zege ziongezeke kutokana na umbali mfupi

Kingine material yote ambayo yanatakiwa yatumike kesho, inabidi yawe yamefika site siku ya leo ili kesho asubuhi na mapema kazi ziendelee kuepuka delay ya kusubiri material/vifaa
 
Udongo wa mfinyazi haufai kabisa katika ujenzi, katika vitu vya kuzingatia ktk ununuzi wa kiwanja ni pamoja na kujua aina ya udongo ktk hicho kiwanja vinginevyo utaingia gharama zingine ktk kukabiliana na udongo huo. Mfinyazi una tabia ya kukatika pindi maji yanapokauka hivyo kama ulijenga tu hivi hivi juu ya mfinyazi, tegemea kuta kupata nyufa za kutosha
 
Kama msingi wako ni mrefu, ni vyema ukafunga mikanda miwili. Mfano kama msingi umejenga kozi 8, unaweza ukafunga mkanda baada ya kozi ya 5 na baada ya kozi ya 8 (ya mwisho)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
 
Mafundi wengi wanatumia pipe level kwenye kozi ya mwisho (mfano kama msingi una kozi 7, basi ile kozi ya 7 ndio wanaitafutia level). Sasa kuna muda inatokea upande mmoja unadai udongo mwingi (mortar thickness) ili kufikia level ya upande mwingine hivyo inashauriwa utumie pipe level angalau katika kozi mbili kabla ya kuifikia ile kozi ya mwisho ili in case kama kuna upande utadai udongo mwingi uweze kubalance katika hizo kozi kuliko kurundika udongo sehemu moja katika kozi ya mwisho

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
 
Katika ufungaji wa bomba za umeme, ni vizuri ukatumia gundi (tangit) kati ya maungio ya kifaa kimoja na kifaa kingine mfano round box na pipe, au pipe na elbow n.k. Hii itafanya mfumo wako wa umeme kuwa salama zaidi hasa kwa wanyama kama Panya ambayo huwa wanazaliana huko kwenye dari.

Kwanza siku hizi ule mfumo wa kuweka bomba za umeme juu ya dari umepitwa na wakati, mfumo wa siku hizi bomba zinapita kwenye kuta tu hivyo matatizo kama Panya kula waya na kesi zingine kama hizo huwezi ukakutana nazo tena

Kama utafunga bomba zako juu ya dari na mfuko wako upo vizuri tumia bomba za class B, zenyewe ni ngumu na imara zaidi ukilinganisha na bomba za class A ambazo ukiminya hata kwa mkono bila kutumia nguvu nyingi zinabonyea
 
Katika hizi nyumba za contemporary,ikitokea umejenga eneo lililoko mbali kiasi na mitaro ya maji taka,yale maji yanayoshuka chini na bomba huwa tunazielekeza wapi?

Na pia naomba uongelee finishing ya kuta za nje kwa kutumia CONMIX hasa gharama,ubora na madhaifu yake ukilinganisha na finishing ya rangi za kawaida
Asante mkuu Hechy Essy
 
Katika hizi nyumba za contemporary,ikitokea umejenga eneo lililoko mbali kiasi na mitaro ya maji taka,yale maji yanayoshuka chini na bomba huwa tunazielekeza wapi?

Na pia naomba uongelee finishing ya kuta za nje kwa kutumia CONMIX hasa gharama,ubora na madhaifu yake ukilinganisha na finishing ya rangi za kawaida
Asante mkuu Hechy Essy
Weka slope mahali yanapomwagikia maji ili yaende kwenye barabara za mitaa. Barabara huwa ina muinuko kati kati (camber) kwa hivyo maji yatakuwa yanatembea humo humo mahali ambapo palitakiwa pawekwe mitaro lakini haijawekwa
 
Katika udongo, huwa kuna nafasi kati ya punje moja na punje nyingine (voids). Wakati wa kujaza kifusi, maji huwa yanawekwa katika kifusi ili ile hewa (yaani void) iondoke katika udongo kwa sababu maji yana uzito (density) mkubwa kuliko hewa kwa hivyo hewa haiwezi kubaki chini kama juu yake kuna maji.

Kila udongo una kiwango chake cha hiyo nafasi ya hewa kati ya punje na punje, sasa inapotokea maji yaliyowekwa kwenye kifusi yamezidi kipimo, hayo maji yaliyozidi yanaanza kutengeneza msukumo (hydrostatic pressure) katika kuta ili kutafuta sehemu ya kutokea wakati unashindilia huo udongo (kifuisi)

Pressure hiyo ndio huwa inayosababisha nyufa katika kuta za msingi hasa hasa kwa udongo ambao una tabia ya kuhifadhi maji kwa wingi.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
4 bedroom house
  • Master 1 yenye kibaraza chake, unaweza ukaingia ama kutokea mlango huo (ramani nzuri sana kwa wadaiwa sugu)
  • Self 1
  • Single 2
  • Jiko
  • Dining
  • Store
  • Library/Pray room
  • Public toilet 2

Chumba cha master kipo mbali sana na vyumba vingine, hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyoteView attachment 2898139
Nasisitiza Tena, "hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyote".

Sio mko kwenye shughuli zenu za "kubovusha" kitanda Watoto au family members wengine wanawasikia.
 
Katika ujenzi wa tofali, hakikisha ile mortar ya kusimama (perpend) haikai kati kati ya tofali la juu ama la chini (inatakiwa ikae pembeni ya center ya tofali la juu na la chini)
Mmmhh,
Somo bado teacher, tunaomba urudie.
 
Mmmhh,
Somo bado teacher, tunaomba urudie.
Uzito wa tofali la juu ubebwe na tofali mbili za chini, na huo uzito usiegemee kati kati ya tofali kwani tofali ni rahisi kukatika sehemu ya kati kuliko sehemu ya pembeni. Kiufupi tofali la chini libebe 75% ya uzito wa tofali moja na 25% ya uzito wa tofali lingine, lisibebe 50% kwa 50% ya uzito wa kila tofali
 
Hakikisha vifaa vya umeme utakavyoweka nje ya nyumba mfano socket za nje, taa za garden n.k viwe vina uwezo wa kutoruhusu maji ya mvua/umande kuingia ndani ya hivyo vifaa.

Zipo socket maalum ambazo zina mifuniko yake ambayo inazuia maji kutoingia, hutumika hata sehemu za kuoshea magari pia.

Socket za nje jitahidi ziwe na switch yake ndani ya kuruhusu umeme kutoka nje ili uwe una uwezo wa kuwasha na kuzima kwa usalama zaidi kwani wezi wanaweza wakatumia hizo hizo socket kutumia machine za kukatia grill (vyuma), wakakata dirisha kirahisi na kuiba
 
Back
Top Bottom