Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #301
Madini hayaMoja ya mbinu za kupunguza gharama katika ujengaji wa msingi ni kutumia tofali za nchi 6 badala ya tofali za nchi 5
Kwa kuwa katika msingi tofali zake huwa zinalazwa hivyo ukitumia tofali za nchi 6 utajenga mistari michache tofauti na ukitumia tofali za nchi 5
Tuchukulie mfano msingi wako una mita 1.4 (beam excluded) (nimechukua 1.4m kwa sababu inagawanyika kwa 175mm na 200mm bila kubaki, kiuhalisia nyumba za kawaida msingi huwa ni futi 2 mpaka 3 au na zaidi kutegemeana na slope ya eneo)
Kama utatumia tofali za nchi 6 utajenga mistari 7 (150mm ya tofali + 50mm ya udongo =200mm)
Na kama utatumia tofali za nchi 5 utajenga mistari 8 (125mm ya tofali + 50mm ya udongo= 175mm)
Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 6 itakuwa 50x7×1100 = Tsh 385,000/=
Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 5 itakuwa 50x8×1000 = Tsh 400,000/=
NB: Unene wa udongo nimechukua 50mm ili mahesabu yawe rahisi
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa tuwasiliane
Subscribe kabisa uwe unapata notificationsNitarudi
Weka slope mahali yanapomwagikia maji ili yaende kwenye barabara za mitaa. Barabara huwa ina muinuko kati kati (camber) kwa hivyo maji yatakuwa yanatembea humo humo mahali ambapo palitakiwa pawekwe mitaro lakini haijawekwaKatika hizi nyumba za contemporary,ikitokea umejenga eneo lililoko mbali kiasi na mitaro ya maji taka,yale maji yanayoshuka chini na bomba huwa tunazielekeza wapi?
Na pia naomba uongelee finishing ya kuta za nje kwa kutumia CONMIX hasa gharama,ubora na madhaifu yake ukilinganisha na finishing ya rangi za kawaida
Asante mkuu Hechy Essy
hii sijaelewaKatika ujenzi wa tofali, hakikisha ile mortar ya kusimama (perpend) haikai kati kati ya tofali la juu ama la chini (inatakiwa ikae pembeni ya center ya tofali la juu na la chini)
Nasisitiza Tena, "hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyote".4 bedroom house
- Master 1 yenye kibaraza chake, unaweza ukaingia ama kutokea mlango huo (ramani nzuri sana kwa wadaiwa sugu)
- Self 1
- Single 2
- Jiko
- Dining
- Store
- Library/Pray room
- Public toilet 2
Chumba cha master kipo mbali sana na vyumba vingine, hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyoteView attachment 2898139
Mmmhh,Katika ujenzi wa tofali, hakikisha ile mortar ya kusimama (perpend) haikai kati kati ya tofali la juu ama la chini (inatakiwa ikae pembeni ya center ya tofali la juu na la chini)
Uzito wa tofali la juu ubebwe na tofali mbili za chini, na huo uzito usiegemee kati kati ya tofali kwani tofali ni rahisi kukatika sehemu ya kati kuliko sehemu ya pembeni. Kiufupi tofali la chini libebe 75% ya uzito wa tofali moja na 25% ya uzito wa tofali lingine, lisibebe 50% kwa 50% ya uzito wa kila tofaliMmmhh,
Somo bado teacher, tunaomba urudie.