Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Hiyo inakuwa changamoto ndg yangu
Kiufupi mimi nadesign kulingana na uhalisia ulivyo, nyie huko kwenye utekelezaji ndio mtaamua mfanye vipi ili hata likitokea la kutokea mkamatane mashati wenyewe kwa wenyewe🙂🙂.
Ni vizuri ukafuata muongozo unavyokuongoza ili kuepukana na risk za kudondoka kwa majengo, kitu ambacho kitaleta hasara kubwa na hata kusababisha vifo vya watu
 
Sawa hunaga baya Engineer wetu Mungu akulinde acha nikusanye nguvu then soon nakutafuta
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=ArqQnJe_1L0
Mkuu kama maji ni changamoto naamini wahandisi mtakuwa mmeipatia majibu hii changamoto kwa kuja na board sizisopitisha maji. Naanza kufikiria kufanya partion ya board pekee kwa juu badala ya blocks


View: https://www.youtube.com/watch?v=t4T619wzP-w
 
Boards ambazo haziathiriwi na maji ni PVC boards (mara nyingi huwa zinatumika hata kwenye milango ya chooni na kufunikia dari nje ya nyumba). Lakini pia kuna glass japo hii sikushauri kuitumia, maana inaweza ikaleta shida in case kama mtu amejigonga bahati mbaya
 
Nimekuelewa mkuu. Nitatumia pvc maana matumizi yangu sio makubwa sana ni kama mita 8 tu hivi. Nachopunguza ni uzito na sio gharama
 
Nimekuelewa mkuu. Nitatumia pvc maana matumizi yangu sio makubwa sana ni kama mita 8 tu hivi. Nachopunguza ni uzito na sio gharama
Hivi zile ceiling board za kizamani haziwezi tumika pia? kuna nyumba naifahamu wamefanya partioning ya hizo board tokea miaka ya 70 zipo vile vile au ndo moto ukitokea zitashika moto faster and so proposed solution ni kutumia gypsum board ambazo mafundi husema hazishiki moto Hechy Essy msaada wa mawazo hapa tafadhali

Nadhani OKW BOBAN SUNZU hapa ni kutumia kitu chenye uzito mdogo kadiri iwezekanavyo kitaalam
 
Nimekuelewa mkuu. Nitatumia pvc maana matumizi yangu sio makubwa sana ni kama mita 8 tu hivi. Nachopunguza ni uzito na sio gharama
Slab yako ni hii ya kawaida ya vichanja vya nondo na zege ama ni ile ya kutumia pre casted slab zinapangwa then unaweka wire mesh na kumwaga zege?
 
Slab yako ni hii ya kawaida ya vichanja vya nondo na zege ama ni ile ya kutumia pre casted slab zinapangwa then unaweka wire mesh na kumwaga zege?
Itakuwa kichanja, Bado ipo kwenye makaratasi. Nachofanya hapa ni kujiongeza maana mtalaamu wangu sio wa kumtegemea kila kitu
 
Itakuwa kichanja, Bado ipo kwenye makaratasi. Nachofanya hapa ni kujiongeza maana mtalaamu wangu sio wa kumtegemea kila kitu
Ok poa naja PM kuna vitu nataka nijifunze kwako maana angalau kuna stages wewe ushavuka. Nitakuwa na project ya kujenga kighorofa hapo baadae so sio mbaya nikajifunza kutokea kwako pia.
 
Vilevile nimewaza inawezekana kwenye 1st floor ukatumia yale matofali yenye uwazi ndani, na pengine sijajua kitaalam inawezekana ule uwazi ukaongezwa zaidi kwa maana ya kumodify mold kuwa nyembamba zaidi ambapo wembamba utakuwa compesated na plaster kama ambayo umesema lengo hapa ni kupunguza uzito kwa kadiri iwezekanavyo kitaalamu.

Vilevivile kuna yale maplastic ( Expanded Polystyrene blocks) siku hizi yanatumika nayo pia ni option nzuri ya kupunguza costs check ujionee.
nimeona Dar mtaa wa uhuru kuna maghorofa siku za karibuni wametumia yana uzito mdongo Expanded Polystyrene in Nairobi, Kenya
 
Kila chenye hasara, kwa upande mwingine kinakuwaga na faida zake pia japo ni chache

Kumlipa fundi kwa siku kunakupa option ya kubadilisha fundi siku yoyote hasa pale unapokuwa huridhishwi na kazi yake tofauti na kumlipa fundi kwa kazi yote na humjui

Vuta picha umeshamlipa fundi advance na mmekubaliana afanye kazi ya kujenga boma, lakini kazi yake anavyoifanya huielewi...hapo utachukua hatua gani?!

NOTE
Usimpe fundi kazi ya muda mrefu ikiwa hujui kazi zake zipoje, wapo wengi walioingia hasara ya kuanza upya baada ya kuharibiwa kazi zao. Na hii ni kwa sababu maboss wengi wanakosa ujasiri wa kumfukuza fundi, hivyo anasubiri fundi amalize kazi yake ili abomoe aanze upya.

Mchunguze vizuri fundi jinsi anavyosoma futikamba yake, jinsi anavyotumia vifaa kama kobilo, square, spirit level n.k, hivi vyote vitakupa majibu ya awali kuhusu umahiri na ubora wa kazi zake kabla hata hajafika mbali

Kama haujui vizuri kazi zake, ni vyema ukaanza nae malipo kwa siku, ukiona kazi yake ni nzuri ndipo mkae tena mezani kwa makubaliano ya kazi ya muda mrefu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Pale unapoanza na ripu (plaster) kisha ukafuata na floor (rough floor). Plaster ya kuta inatakiwa isimame juu ya rough floor kwa hivyo unatakiwa uanze na floor kisha ndio upige plaster

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ni vizuri gympsum boards zote katika chumba husika zikawa na uelekeo mmoja ili fibre tape itakapowekwa kwenye maungio ya board na board ifike mpaka mwisho wa kuta, isikatiwe njiani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Bati za Ando mbona hazivumi lakini naskia wanabati imara sana je nikweli?
 
Bati za Ando mbona hazivumi lakini naskia wanabati imara sana je nikweli?
Inawezekana ikawa ni kweli lakini mpaka kuja kusikika inaweza ikachukua muda, ushindani kwa sasa ni mkubwa...kampuni zimekuwa nyingi mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…