Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 873
- 3,307
- Thread starter
-
- #1,081
Huwa tunaongeza asilimia flani kama allowanceMkuu hivi mkikadiria bati kwenye makadirio hua inakua exactly?
Mkuu kwani haiwezekani kumsimamia fundi atumie pipe level kwenye top level pale ili kuweka height sawa kwa nyumba nzima. Kuliko tena kwenda kuitafutia kwenye upigaji wa dari.Katika ujenzi kuna makosa madogo madogo huwa yanafanyika ambayo huwezi ukayanotice kwa haraka, sasa ili hayo makosa yasiendelee kuzaa makosa mengine katika hatua zingine zinazofuata ni vyema katika kila hatua ya ujenzi ukawa unafuata procedure zote bila kutumia/kutegemea hatua iliyotangulia kama reference
Mfano katika ujenzi wa kuta, ule usawa wa juu kabisa wa boma unaweza usiwe level moja kwa nyumba nzima (kuna sehemu zinaweza zikawa zinapishana kidogo), sasa mfano ukisema utumie usawa wa juu wa boma kama reference katika kupima height ya dari, dari pia halitakuwa level (litainama) ndio maana zoezi la kupigilia mbao za dari, lazima pipe level itumike ili kuhakikisha dari linakuwa na usawa mmoja katika nyumba nzima hata kama kulikuwa na makosa katika ujenzi wa kuta. Mifano ni mingi lakini kwa leo, huo mfano mmoja unatosha
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Wakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chiniMkuu kwani haiwezekani kumsimamia fundi atumie pipe level kwenye top level pale ili kuweka height sawa kwa nyumba nzima. Kuliko tena kwenda kuitafutia kwenye upigaji wa dari.
naona wengi wanatafuta level kwenye mkanda ili madirisha yawe sawa wakipigilia zile mbao za button za madirishaWakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chini
Kama wakitumia pipe level kozi mbili kabla ya kufika mwisho, inasaidia kugawanya huo utofauti uliotokea na kuubalance udongo katika kozi zote mbili hivyo udongo unakuwa haurundikwi sehemu moja pekee (katika kozi moja)
Kuna level flani ya kuta ikishafika (mfano kozi ya 6 au ya 7), pipe level inatumika kutafuta level nyumba nzima na kutokea hapo kwenda huko juu, kozi zote zinakuwa zinatumia hiyo level iliyotafutwa kama reference japo pia katika zoezi la kufunga mkanda ni vizuri pia kuhakikisha level kama iko sawa
Mtaalam. Hivi mbao ya msedelea unaweza tumia kjtengeneza milango ya ndani na isiliwe na mchwa au kupinda?Wakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chini
Kama wakitumia pipe level kozi mbili kabla ya kufika mwisho, inasaidia kugawanya huo utofauti uliotokea na kuubalance udongo katika kozi zote mbili hivyo udongo unakuwa haurundikwi sehemu moja pekee (katika kozi moja)
Kuna level flani ya kuta ikishafika (mfano kozi ya 6 au ya 7), pipe level inatumika kutafuta level nyumba nzima na kutokea hapo kwenda huko juu, kozi zote zinakuwa zinatumia hiyo level iliyotafutwa kama reference japo pia katika zoezi la kufunga mkanda ni vizuri pia kuhakikisha level kama iko sawa
Aise ndg yangu huu mti kwangu ni mgeni, ndio leo nausikia kwako kwa hivyo sina experience nao.Mtaalam. Hivi mbao ya msedelea unaweza tumia kjtengeneza milango ya ndani na isiliwe na mchwa au kupinda?
Ila nadhan wapauaji ndio tatizo. Kuna wengine yako safi tu. Kwenye maungio wanapiga FLASH COVER saafi kabisaKuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).
Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
what a solutionKuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).
Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
Bonge Moja la Uzi .....Wakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa
Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama
Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
1. Idadi ya kozi kutoka mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu inategemea na mtu anataka aweke madirisha ya urefu gani.Hivi kuna tofauti gani katika boma fundi anapojenga tofari 10 akafatia lenta akamalizia na 3 za mwisho
Na anayejenga tofari 11 akafatia lenta akamalizia 3 za mwisho
Na pia inawezekana fundi akajenga 10 akaweka lenta juu akamalizia 4 na sio tatu na ipo vixuri au kiufundi sio sahihi
Hata mimi naona kabisa naelekea kuvunja paa la kuficha nipaue upya kawaida. Hata sielewi nilifikaje hukoKuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).
Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
mkuu kongole sana kwa huu uzi I salute you, mm ni mtaalamu wa ujenzi ila sijui kila kitu with due respect nadiriki kusema uzi wako umekuwa shule tosha kwangu. ( huwa nakuja hapa kuongeza nyama nyama kwenye Ile knowledge ndogo ya ujenzi niliyonayo ). keep it up bro nikipata mteja wa ramani ntamrecommend kwako kuonyesha appreciation yangu kwakoHawa ndio mafundi wa chap chap, huwa wanawaza kumaliza kazi tu ili wapate hela yao waondoke.
Picha yenyewe nimepiga kwa kuvizia, ukuta umeinama kiasi kwamba hata ukikaa mbali unauona kabisa kama umeinama
Fundi kupaua asipojiongeza, paa nalo litainama pia. View attachment 3292171
hapa umeinamaje emu elezeaHawa ndio mafundi wa chap chap, huwa wanawaza kumaliza kazi tu ili wapate hela yao waondoke.
Picha yenyewe nimepiga kwa kuvizia, ukuta umeinama kiasi kwamba hata ukikaa mbali unauona kabisa kama umeinama
Fundi kupaua asipojiongeza, paa nalo litainama pia. View attachment 3292171
Nashukuru sana kwa appreciation, tuko pamoja ndugumkuu kongole sana kwa huu uzi I salute you, mm ni mtaalamu wa ujenzi ila sijui kila kitu with due respect nadiriki kusema uzi wako umekuwa shule tosha kwangu. ( huwa nakuja hapa kuongeza nyama nyama kwenye Ile knowledge ndogo ya ujenzi niliyonayo ). keep it up bro nikipata mteja wa ramani ntamrecommend kwako kuonyesha appreciation yangu kwako
Angalia usawa wa juu wa ukuta, utaona ukuta kwa juu kuna slopehapa umeinamaje emu elezea