Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 873
- 3,307
- Thread starter
-
- #1,221
Kama ulivyopendekeza kwenye comments za nyuma juu ya matumizi ya level pipe. Je, haiwezekani ukatumia mbao ama kamba yenye urefu fulani, mfano kama ukuta umefika futi 7, ukatumia kamba au mbao yenye futi 7 kupimia hiyo level ya ukuta kwa kila upande?.Mara nyingi level huwa inatafutiwa wakati wa kufunga box la mkanda lakini pia unaweza ukatafuta level kozi mbili kabla ya kufikia hatua ya mkanda.
Inawezekana, ila mara nyingi hii tunatumia ktk ujenzi wa msingi hasa sehemu zenye muinuko (msingi kuwa na steps)Kama ulivyopendekeza kwenye comments za nyuma juu ya matumizi ya level pipe. Je, haiwezekani ukatumia mbao ama kamba yenye urefu fulani, mfano kama ukuta umefika futi 7, ukatumia kamba au mbao yenye futi 7 kupimia hiyo level ya ukuta kwa kila upande?.
Mbinu nyingineKatika hatua ya kufanya wiring katika nyumba, kuna mbinu mbali mbali zinazotumika kupunguza gharama za material.
Leo nitaelezea mbinu moja wapo
Ikitokea vyumba viwili vina-share ukuta, basi tafuta point moja katika huo ukuta ambayo itakuwa comfortable kwa vyumba vyote kuweka socket pande zote mbili. Hii inasaidia kupunguza matumizi ya waya na bomba tofauti na kuweka socket katika point tofauti tofauti.
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hakuna Three way switch yaan unawasha mara tatuMara nyingi taa ya koridoni, switch yake huwa inawekwa mwanzoni mwa korido kwa hivyo kama mtu yupo mwishoni mwa korido atalazimika kuifata switch ilipo ili azime/awashe taa kisha arudi tena mwishoni mwa korido huku akiwa anatembea gizani.
Ili kukabiliana na hii changamoto, ni vyema taa ya koridoni ikawa na swichi mbili (two way switch) mwanzoni na mwishoni mwa korido ili mtu aweze kuwasha/kuzima taa akiwa popote
Njia hii inatumika pia na kwenye taa inayomulika ngazi (kwa majengo ya ghorofa) ambapo switch moja inawekwa chini kabla ya kupanda ngazi na switch nyingine inawekwa juu baada ya kumaliza kupanda ngazi
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
Kama unataka kuwe na switch zaidi ya mbili (mfano 3) unaongeza switch ya 4-ways (intermediate switch) katika hizo switch mbili za 2-ways.Hakuna Three way switch yaan unawasha mara tatu
Unaweza ukaongeza switch ya taa/feni pembeni kidogo ya kitanda ili usilazimike kuinuka kitandani kwenda kuzima/kuwasha taa mlangoni.Mara nyingi taa ya koridoni, switch yake huwa inawekwa mwanzoni mwa korido kwa hivyo kama mtu yupo mwishoni mwa korido atalazimika kuifata switch ilipo ili azime/awashe taa kisha arudi tena mwishoni mwa korido huku akiwa anatembea gizani.
Ili kukabiliana na hii changamoto, ni vyema taa ya koridoni ikawa na swichi mbili (two way switch) mwanzoni na mwishoni mwa korido ili mtu aweze kuwasha/kuzima taa akiwa popote
Njia hii inatumika pia na kwenye taa inayomulika ngazi (kwa majengo ya ghorofa) ambapo switch moja inawekwa chini kabla ya kupanda ngazi na switch nyingine inawekwa juu baada ya kumaliza kupanda ngazi
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
Ni nini tofauti ya DPM na Dpc?DPM unaweka kabla ya kumwaga jamvi, ila DPC unaweka wakati wa kuinua kuta za boma (juu ya mkanda wa msingi)
DPC (Damp proof course) inalazwa juu ya mkanda wa chini kabla ya kuanza ujenzi wa tofali za boma, lakini DPM (Damp proof membrane) yenyeye ni pana na inatandikwa kama mkeka chini ya jamvi/floorNi nini tofauti ya DPM na Dpc?
Hii ni Moja ya matumizi mazuri ya pesa, ushauri huu uheshimikeWakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa
Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama
Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
Tuko pamoja ndg, endeleeni kufatilia bila kuchokakwa ushauri mzuri unaotupatia, nimeenda mbali nikawaza nyumba yako itakuwa imenyooka kama rula
Hongera sana mkuu
Siku hizi wanatumia zile single nazo zinaivo vipimo?Katika mfumo wa umeme, hakikisha kila sakiti inatumia size ya waya husika. Mfano sakiti ya socket waya wake ni tofauti na waya unaotumika katika sakiti ya taa/feni.
Katika sakiti ya socket, size ya waya inayotumika ni 2.5mm² na katika sakiti ya taa waya unaotumika ni 1.5mm²
Kwa kuwa waya wa 2.5mm² bei yake ipo juu kulinganisha na bei ya waya wa 1.5mm², mafundi wamekuwa na kawaida ya kutumia waya wa 1.5mm² katika sakiti zote licha ya kwamba katika list ya manunuzi waya wa 2.5mm² uliwanunulia (kwao ni bora ubaki waya wa 2.5mm² kuliko ubaki waya wa 1.5mm² ili wakienda kuuza wapate pesa nyingi)
Huo ni mfano mdogo tu, kuna waya wa 4mm² pia ambao unatumika kwenye sakiti ya jiko la umeme, kuna waya wa 6mm² au 10mm² ambao unaenda kupokelea umeme kwenye mita (hapa watakuambia ununue waya wa urefu flani mfano mita 10, lakini kimatumizi unakuta umetumika waya wa mita 4 kwa hivyo muwe makini msije mkamaliza ujenzi mkiwa hoi bin taaban, mkakosa hata hela ya mchele ya kufungulia nyumba siku ya kuhamia)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane