Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Hapa sijaelewa mkuu. Huu ufa unakata na grenda? Je unakata mpaka unatokea upande wa pili? Ukikata kila sehemu yenye dirisha hupunguzi uimara wa nyumba?
Je huu ufa unafanyaje kazi ya kuzuia hizo nyufa za zigzag?
 
Huu Uzi nilikuwa nimeusave tangu mwaka jana nafikiri ni mda na mm niombe ushauri haka ka ramani
 

Attachments

  • f04fef4b1a6b44e4cb80185acf661639_1.jpg
    219.4 KB · Views: 57
Hatimaye nimemaliza kusoma Uzi wote.
Hongera sana fundi ushauri huu ungeuandikia kitabu halafu uweke Kila kitu ndani hakika pesa yangu pia ningeitoa
 
ujenzi upi ni bora kwa fensi yenye kimo mita 2.8 na mzingo mita 270 kati ya hizi mbili katika picha
 
Nahitaji kujenga fremu kubwa 12M Kwa 12m ya biashara ya duka na stoo mixers hardware na vyakula naomba cautation kuanzia msingi wa mawe,tofali za broku, mchanga,semint,mbao,bati,misumar,ufundi nk kwa ramani pia unaweza nishauri ramani nzuri eneo ni tambalale mkoa wa Tanga.
 

Attachments

  • IMG_20250923_133803_HDR.jpg
    468.3 KB · Views: 49
  • IMG_20250923_133755_HDR.jpg
    480.8 KB · Views: 47
Naomba fully cautation kwa ramani hii ya fremu ya biashara kuanzia mchanga,sement,nondo,mbao,bati,ufundi nk
 

Attachments

  • IMG_20251001_125905.jpg
    405.8 KB · Views: 50
 
Ukimaliza kujenga pagale/boma lako, kama unapumzika kuendelea na ujenzi kwa muda, basi ziba madirisha na milango ya nje kwa kupanga tofali ili nyumba yako isigeuzwe kuwa guest house au choo na wahuni.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wakuu, anayehitaji nyumba ya kununua maeneo ya Kibamba anicheki. Nyumba bado kupauwa.
Kama unahitaji njoo nikupe maelezo zaidi, mimi ndo mmiliki mwenyewe.
 
Ili jengo lifanane moja kwa moja na ramani kama inavyoonekana katika karatasi, inatakiwa umakini katika zoezi la kuset jengo. Vipimo vikiyumbishwa kidogo, muonekano wa jengo na paa kwa ujumla hubadilika.

Athari kubwa huwa inakuja kwenye paa, kwa kuwa paa huwa linafata kuta za nje zinavyozunguka kwa hivyo mpishano wa kuta ambazo zilitakiwa ziwe katika grid moja huzalisha vipaa vingine vidogo vidogo ili kuziba nafasi zilizo wazi, kitu ambacho kinaongeza gharama katika hatua ya upauaji.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Mkuu naomba Raman ya vyumba vi 3
Kimoja masters na varanda yake
Ondoa dinning, kitchen, public toilet
 
Hata kama eneo lako halina asili ya maji maji, hakikisha kuta zako za vyoo unatandika nailon (DPC) kabla hujaanza kupandisha kuta za boma kwa sababu vyooni ni sehemu ambazo zinakuwa na maji maji muda mwingi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Rekebisha hizo vent za huko kwenye paa, hazina kazi yoyote zaidi ya kuozesha ceiling board
Ni kweli. Ila zinasaidia kupunguza madhara ya ceiling kufumuka pia kutokana na wind pressure... Ingawa hii ina minor effect...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…