Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 873
- 3,307
- Thread starter
-
- #1,341
Kiongozi kwa makadilio ya vyumba viwili na sebure sehemu tambalale inaweza chukua tofali ngap hadi kukamilikaNi vyema dirisha zako ukaziweka kati kati ili mkanda wako juu ya dirisha uwe na support za kuta zinazolingana (support width, kushoto na kulia)
Mfano kama ukuta wako una urefu/upana wa mita 3.6 ndani kwa ndani na dirisha lako lina upana wa mita 1.5 basi dirisha lako inabidi lianzie umbali wa mita 1.05 sawa na sentimita 105 kutokea katika kona ya chumba
X = (3.6 - 1.5)/2 = 1.05m kutokea kwenye kona ya chumba
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Mkuu mbona unapotea sana tuna miss madini kama hayaUkienda kununua kiwanja mahali hasa hivi vya bei kubwa, pendelea kutumia mfumo wa malipo ya awamu hata kama unaweza kulipia pesa yote kwa pamoja.
Hii itamfanya hata muuzaji (na watu wengine kama madalali nk) wajue kwamba pesa yako ni ya kuunga unga (ifanye hali yako ya kiuchumi kuwa ni siri hasa kwa watu usiowajua)
Ukiwa unamiliki kitu ambacho wengi hawana na wanakitafuta kwa nguvu zote basi ujue kwako hiyo ni risk hivyo epuka kujionesha au kutaka kuonekana kuwa unacho.
Sasa ukiacha nondo kavu niulizie nondo gan hizo zingine? Nondo mbichi au?Nondo kavu
Ukienda hardware kununua nondo, kuwa makini...fanya field test hapo hapo kabla ya kulipia na kuondoka na mzigo (mchukue fundi abebe na bender yake, uongozane nae hardware).
Nondo kavu ukiikunja huwa inakatika, ni kama mti uliokauka sana.
Nondo inayofaa katika ujenzi haitakiwi kukatika pale inapokunjwa.
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3544797
Nauliza juu ya matumizi ya DPM kwenye hatua ya jamvi. Mfano baada ya kujaza kifusi na mawe kisha ukasuka nondo ( mf. Kwenye jamvi la ghorofa) na kufunika kwa DPM kisha ukamwaga zege. Swali langu ni juu ya kuzifunika nondo kwa DPM haiwezi kuleta shida kwenye mambo ya stability ukizingatia kwamba zege linatakiwa lishikane na nondo moja kwa moja ili kupata mshikamano uliokusudiwa?.Nyumba za paa la kuficha kupendeza kwake ni kule kupishana kwa kuta za juu ya mkanda.
Changamoto iliyopo ni mafundi kulazimisha kuta zote zilingane urefu hata kama hakuna ulazima.
Kule juu ya mkanda, kuna kuta zingine kazi yake ni kusimama kama kingo tu za mifereji ya maji kwa hivyo hakuna ulazima wa kujenga kozi nyingi wakati unaweza ukajenga kozi mbili au tatu tu na ukaokoa idadi kubwa ya tofali.
Mbali na kuokoa tofali, pia inapunguza mzigo wa jengo katika ardhi
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
DPM haiwekwi juu ya nondo ndg, nondo zinalazwa juu ya DPM.Nauliza juu ya matumizi ya DPM kwenye hatua ya jamvi. Mfano baada ya kujaza kifusi na mawe kisha ukasuka nondo ( mf. Kwenye jamvi la ghorofa) na kufunika kwa DPM kisha ukamwaga zege. Swali langu ni juu ya kuzifunika nondo kwa DPM haiwezi kuleta shida kwenye mambo ya stability ukizingatia kwamba zege linatakiwa lishikane na nondo moja kwa moja ili kupata mshikamano uliokusudiwa?.
Shukrani kwa ufafanuzi. Kuna picha niliiona kwenye page ya NHC, huenda labda sikuangalia vizuri mpangilio wa mawe, DPM na nondo.DPM haiwekwi juu ya nondo ndg, nondo zinalazwa juu ya DPM.
Nondo unalaza juu ya DPM, kwa maana hata nondo pia zinatakiwa zilindwe na unyevu ili zisipate kutu ambapo hiyo kazi inafanywa DPM
Kiufupi DPM inatenganisha tabaka la mawe (hardcore) na zege (jamvi)
DPM haiwekwi juu ya nondo ndg, nondo zinalazwa juu ya DPM.
Nondo unalaza juu ya DPM, kwa maana hata nondo pia zinatakiwa zilindwe na unyevu ili zisipate kutu ambapo hiyo kazi inafanywa DPM
Kiufupi DPM inatenganisha tabaka la mawe (hardcore) na zege (jamvi)
Hapo safi, kazi imenyookaView attachment 3550156
Picha niliiangalia kwa haraka. Maelezo yako ni sahihi kwa mujibu wa picha.