Elimu bora kabisa hiiUjenzi una hatua zake, na hatua zingine zinatakiwa zitangulie kabla ya zingine. Ukivuruga mpangilio ujue lazima utaingia gharama ya ziada huko mbeleni
Mfano unakuta mtu ameanza kupigilia mbao za dari wakati bado hajapachika bomba za umeme ukutani, baadae akitaka kuweka hizo bomba anaanza kufumua mbao za pembeni ili apitishe bomba.
Ikumbukwe kwamba fundi ukimuita site, yeye atafanya kazi yake husika na hawezi kukuambia kwamba inabidi fundi wa tasnia flani ndio anatakiwa aanze kabla yake kwa kuhofia kuzungukwa na fundi mwenzake na kukosa hiyo kazi kwahivyo wewe mwenye kazi (boss) ndio unatakiwa ujue ikitoka hatua hii inafuata hatua gani
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
sawa lakini siyo sahihi unaweza kufanya nyumba iwe ndefu na madirisha makubwa kwhaiyo mzunguko wa hewa ukawa poa kabisa , pia siku hizi mamikanda ni old fashion ni mwendo wa plan tu. bytheway mie siku nashauri FLAT ROOFING .Hizo kazi yake ni kuruhusu mzunguko wa hewa ambapo kama usipoweka, lile joto la hewa iliyopo kati ya paa na dari kipindi jua linawaka inasababisha hewa kuwa na pressure ambayo inaenda kusukuma mikanda ya pembeni ya dari na gympsum board na kusababisha mipasuko ktk maungio
Sio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko juusawa lakini siyo sahihi unaweza kufanya nyumba iwe ndefu na madirisha makubwa kwhaiyo mzunguko wa hewa ukawa poa kabisa , pia siku hizi mamikanda ni old fashion ni mwendo wa plan tu. bytheway mie siku nashauri FLAT ROOFING .
Sio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko ju
Oooh hilo sasa siyo issue maana mafundi umeme siku hizi wako vizuri wakipita juu ya dari wamepita pia nikuweka ventillation tuSio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko juu
Mwisho wa siku uamuzi utabaki kwa mwenye nyumba, aweke ama asiweke. Hiyo sijasema kwamba inawekwa kwa ajili ya mafundi umeme, nilitolea mfano wa mtu wa kumuuliza hali ya joto iliyopo huko juuOooh hilo sasa siyo issue maana mafundi umeme siku hizi wako vizuri wakipita juu ya dari wamepita pia nikuweka ventillation tu
Slope inayowekwa hapo ni ndogo mno kiasi kwamba huwezi kuiona kwa macho, hata wakati wa kuset inatakiwa ile bubble ya pima maji isitoke yote ktk chumba chake cha kati. Inatakiwa ivuke mstari kidogo sanaHivi sakafu tambarale ama sakafu mwinamo kidogo ipi ni Bora? Kwa maana baadhi ya mafundi seremala husema sakafu mwinamo husababisha mlango uburuze sakafuni.
Mlango kuburuza sakafuni chanzo ni sakafu mwinamo ama ni nini?
Upo sahihi kabisaUlinzi wa nyumba kupitia madirisha unaimarishwa na pattern ya grill zako. Dirisha za aluminium (vioo) zinazuia tu baridi na vumbi, kwa sababu kama mtu amedhamiria kabisa kuiba anaweza akapasua kioo kwa nyundo au jiwe.
Hakikisha pattern ya grill zako utakayochagua iwe ni complex kidogo, sio mtu akipachua point mbili tu tayari ameshapata upenyo wa kuingia ndani.
Mwizi kawaida huwa anacheza na hesabu za muda, akiona dirisha lako ni rahisi kupachua let say atatumia labda dakika moja au mbili kupachua, basi ni rahisi kufanya maamuzi ya kupachua na kuingia tofauti na angekutana na dirisha lenye pattern ngumu ambapo atahofia kutumia muda mwingi na kukutwa akiwa bado hajafanikisha dhamira yake.
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ushauli mzuri kabisa huu ubalikiwe sanaNi bora ukajenga nyumba ya vyumba vitatu ambayo ina sebule na jiko bila dinning room kuliko kuwa na nyumba ya vyumba viwili yenye sebule, jiko na dinning.
Dinning ni sehemu ambayo inatumika muda mchache sana, kwahivyo kama uchumi hauruhusu sio lazima kuwa na dinning (kwa hizo situation mbili hapo juu, ni heri ukaongeza chumba cha kulala ukaskip dining, watu wanaweza wakala hata sebleni).
Wageni kula chakula sebleni na usiku wakapata chumba cha kulala ni bora kuliko wageni wakala chakula dinning lakini usiku wakalala sebleni kutokana na kukosa chumba cha wao kulala.
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Habari pichaUķipita site nyingi, utakutana na hili tatizo la mkanda wa msingi kuwa na level moja nyumba nzima.
Mkanda wa msingi unaopita sehemu ya kibaraza unatakiwa uwe chini kwa kozi moja mfano kama msingi wako umejenga kozi 7, basi sehemu ya kibaraza jenga kozi 6 tu.
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane