Ramani mpya ya Afrika Mashariki haioneshi Zanzibar, Inabidi kuwe na masahisho

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264


Upande wa kwanza Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika ikapatikana Tanzania, katika huu muungano Zanzibar inabidi iwe na raisi au makamu wa raisi wa Tanzania, Pia Wazanzibari katika huu muungano wapo Mawaziri, mabalozi, wakuu wa taasisi, wabunge, Idara za ulinzi, waajiriwa, n.k.

Lakini kwa upande mwengine Zanzibar ina serikali yake ambayo haiingiliani na Tanganyika, Kwa mfano kwenye Ajira za serikali ya Zanzibar inabidi muombaji awe mzanzibari, Wana rais wao Mzanzibari, Wana katiba yao, Wana mahakamu wa raisi Mzanzibari, wama bunge lao la wazanzibari, Wana taasisi zao za mpira, umeme, mapato, n.k. Huku Mtanganyika hakumuhusu.

Sasa kama eneo linalooneshwa kwenye ramani ni upande wa Tanganyika pekeyake utasemaje ni ramani ya Tanzania?
 
Mimi naona ibakie hivyo hivyo tu! Nchi gani watu wake hawana hata vichogo! Yaani wote vichwa vyao ni flat screen! 😬😁😁😁😁
Ndjo wenye nchi hao kwa sasa 😁😁

Mama ndie anaepanga flani aje hapa, huyu aende pale, yule stop.

Meli zikinunuliwa ni pasu kwa pasu.

Misaada kutoka nje ni pasu kwa pasu

Ndege zikija ni pasu kwa pasu
 
wamekosea hapo. hakuna haja ya maelezo marefu
 
Hii hoja niliiona akiishupalia Zitto kule twitani
As long as bendera ya tz ipo hapo sioni shida sana.
Ni juhudi za Zitto tu kujipendekeza kwa rais kwa vile anajua ni mzanzibari.
 
Hii kitu ingine nahis mm ndiye MTz pekee niliye gundua

Kivipi Sudan kusini upande wa Magharibi ipakwe rangi ya DRC??

Kwamba walio andaa hio Ramani walikuwa careless hivo??
Hapana mkuu hiyo ni moja kati ya rangi za bendera ya sudani kusini pia ina nyota kama ilivyoonekana hapo,, pitia kwenye key ya ramani utagundua.
 
Ipo mzee ila ni dot ndogo sana huwezi kuiona kwa macho baada ya kuweka DRC. Inadi uzoom sana ili kuweza kuiona.
 

Hilo ni nchi wanachama wa EAC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…