Ramani za nyumba za kwenye series maarufu kwenye tv

Ramani za nyumba za kwenye series maarufu kwenye tv

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Kwa wale wapenzi wa kuangalia TV Drama/Series za Hollywood, lazima kutakuwa kuna nyumba umeipenda na ungetamani ungeishi humo.

Leo tuangazie baadhi ya ramani hizo
SEHEMU YA KWANZA

1.HOW I MET YOUR MOTHER
20240415_130814.jpg

Wanaoikumbuka sitcom hii,iliyokuwa na akina Tedy Mosby,Marshall,Bernie,Robin na Lily nadhani mnakumbuka ile nyuma maarufu waliyokuwa wakikutan.
Maelezo :
  • Jengo la ghorofa,amabapo hiyo nyumba ni mojawapo ya apartments
  • Ukiingia ndani,mbele unaona upande wa kulia kuna sehemu ya kula
  • Kulia kuna sebure,ambapo Kulia kwa sebure kuna ofisi ya nyumbani
  • Kwenye Ofisi kuna njia za kwenda vyumba vya kulala
  • Huku dinning ndipo jipo lilipo
  • Nafasi kati Jsebure,dinning na Ofisi hakuna kuta ili kuruhusu mzunguko wa hewa,na urahisi wa watu kutembea
  • Madirisha ya nyumba yote yapo upande mmoja
  • Kuta za nje ni Nene kwa ajili kuthibiti baridi.

2.FRIENDS
20240415_134308.jpg

Sitcom nyingine maarufu ambayo ilipendwa sana.Ilikuwa ikuhusu marafiki 6 Rachel,Monica, Phoebe, Ross,Joey na Chandler.
Nyumba maarufu walizokuwa wakiishi hizo hapo juu
Maelezo :
  • Makazi yapo ghorofani na ni apartments
  • Kushoto ni makazi ya Joey na Chandler
  • Ukiingia tu,kulia kwako kuna jiko,kushoto kuna dinning
  • Ukiendelea mbele kuna sebure,ambapo kulia kuna choo cha umma
  • Mbele ya sebure kuna Milango ya vyumba vya kulala.
Kwenye makazi ya Monica na Rachel
  • Ukiingia unafikia jikoni,ukikunja kushoto kuna dinning
  • Mbele kuna sebure,kushoto ya sebure kuna ofisi ya nyumbani na choo cha umma.
  • Mbele ya sebure kuna vyumba
Ramani zote zina
  • Madirisha upande mmoja
  • Kuta za nje Nene,kuzuia baridi
  • Floor plans zisizo na kuta
  • Majiko yako mlango mkuu,ili kuruhusu vyumba muhimu kuwa madirishani.
  • Privacy haijzingatiwa kabisa
 
Kumbe nyumba zao ndio zilivyo.

ASANTE KWA KUTUJUZA MKUU.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
THE BIG BANG THEORY : 3
20240415_130744.jpg


Ni makazi ya wahusika wawili wa kwenye hii Sitcom maarufu,Penny,Leonard na sheldon

1.Makazi ya Sheldon
  • Jengo ni la ghorofa
  • Unapanda ngazi au Lift,kufika floor husika
  • Kuna madirisha mawili kwa ajili mwanga kwenye ngazi
  • Ukifungua mlango,moja kwa moja upo sebureni,
  • Mbele kuna sehemu ya Jikoni,ambapo meza ya kuipulia ya kuweka chakula kilichoiva ndiyo yatenganisha jiko na sebure
  • Kulia kwa sebure kuna,Meza ya ofisi ya nyumbani,halafu Luna mlango wa kwenda chumbani.
  • Dining ipo kushoto mwa mlango wa chumba...
  • Hii Ramani ni maalum kwa mtu aliye single au mwanachuo
MAKAZI YA PENNY
  • Ukiingia ndani,unakuta chumba kikubwa ,ambapo ina sehemu ya sebure mbele yako
  • Mbele Kulia, Kuna sehemu ya kupika na meza ya kulia
  • Mbele kushoto, kuna mini-Library
  • Mbele katikati utaona korido,ambayo ina kupereka choo cha umma
  • Kulia unaenda kwenye vyumba binafsi
Ramani zote
  • Zina eneo kubwa na vyumba vichache
  • Floor plan huru,,yaani Sebure,Jiko,mahala pa kula na kusoma vyoote vipo chumba kikubwa kimoja
  • Privacy siyo kitu muhimu kwao.
  • Idadi ndogo ya madirisha
 
Back
Top Bottom