Rambo kulikoni kelele zote hizo......????

Rambo kulikoni kelele zote hizo......????

basha unguja

Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
83
Reaction score
77
Nawasalimu waungwana!

Poleni sana na mihangaiko ya siku nzima!

Tulio wengi itakuwa tunakumbuka vizuri baada ya kuangalia movie za kikomando kwenye vibanda vya kuangalia video, kama tuliowengi wetu tuliopitia mambo haya tutakuwa tunaelewa vizuri sana kwa wale wakishua kidogo wanaweza wasielewe. Sasa kuna matukio yanaambatana baada ya kuangalia movie hizo za kikomando , tulikiwa tunajigawa katika makundi na kujivika majina ya waigizaji nguli na majina mengine tuliyokuwa tunaona yana swaga, kama vile Rambo, Van dame, chaknorisi, Anorld shwaziniga, boloyang, komando kipenzi, Solo, tamineta, n.k baada ya kupeana majina hayo huwa tunagawana majambazi na masteringi then watu tunaingia msituni kwa swaga zile zile za kikomando kama tulivyoona kwenye muvi, tukiwa na bunduki zetu za miti na kujifanya na sisi tunauana kwa kupigana risasi, baada ya hapo tunatoka msituni na kupongezana kulingana na nafasi tulizocheza na kama jina ulilolichukua umelitendea haki.

Siku moja nikiwa na wenzangu akina Ndeleka, Mujiku, Tupe, Side, na wengine ambao siwakumbuki tulitoka kuangalia movi moja matata saaana ya kivita ambayo ilimshirikisha nguli wa filamu wa enzi zileeee Rambo baada ya muvi ile bwana Side akabeba uhusika wa Rambo katika mchezo wetu wa kila siku baaada ya kungalia muvi, tukajichagulia majina pale tukaona sasa tuingie msituni tayari kwa mchezo wa kivita.....

Bwana side kwa uhodari mkubwa sana aliweza kuruka mithiri ya nyani ,aliweza kupotelea msituni huku wengine tukistaajabu uwezo wa bwana Side kuruka kwa jinsi alivyoruka, tukasema labda mzuka wa Rambo kweli umemuingia. Basi na wengine tukaingia msituni huku tukianza kusakana....Bwana side ambaye sasa ni Rambo nikamuona kwa mbaaaali ana tambaa mithiri ya chatu nikasema leo kazi ipo, Gafla tulishtushwa na kelele za kugumia kwa sauti ya juu ikilalama "MAMAA WEEEEEEEEEE MAMA WEEEEEEEE MAMA WEEEEEEE" Makomandoo wote tulikurupuka kutoka msituni huku tukimshuhudia Rambo akitokomea kama kishada....Bila kujiuliza mara mbilimbili makomndoo wote tulimfuata kwa nyuma japo kwa speedi aliyokuwa akienda nayo ilikuwa ni ngumu kumkaribia.....

Rambo alipofika sehemu akasimama, nasisi tulipofika tulimkuta Rambo akitweta ile mbaya tukamuuliza nini kimetokea pale msituni , akasema alipokuwa anatambaa alikuwa haangalii mbele sasa alipoinua macho kuangalia wapi anaenda ndiyo akakutana uso kwa uso na Nyoka aina ya kobra wakawa wanatazamana.....Kwa kumbukumbu yangu toka siku hiyo tukaacha kucheza msituni na ndiyo ukawa mwisho wa ukomandoo wetu wa utotoni.........

michezo ya utotoni bwana
 
Hahaha Rambo....
Muda ukifika atatweta tu, ngoja tuendelee kuntazama.
 
Back
Top Bottom