Ramli: Lady Jaydee kuolewa mara ya pili

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Msanii nguli wa bongo fleva, ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini , Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jaydee, hivi karibuni ametabiriwa kuolewa tena mwaka 2017 na mpiga ramli aliyekwenda nyumbani kwa super star huyo Masaki jijini Dar es salaam.

Akizungumza kupitia kipindi cha msanii huyo, diary ya Lady Jaydee, mpiga ramli huyo alienda mbali zaidi kwa kumtabiria mwanaume atakayemuoa staa huyo, kuwa ni maarufu, mtu mwenye pesa zake na mwenye hadhi kwenye jamii, kitendo ambacho msanii huyo alionekana kukifuraia huku akisema kuwa mwaka 2017 sio mbali hali inayoonyesha msanii huyo kukubaliaba na utabiri huo.

Mbali na kumtabiria maisha yake ya kimapenzi, mpiga ramli huyo aliendelea kutiririka kuwa mwaka huu utakuwa mwaka wa mavuno na mafanikio kwa staa huyo, na ni mwaka ambao akitoa album, basi itafanya vizuri sana sokoni.
 
Hahahaaa,kumbe ni maneno ya mpiga ramli? Huyo mtu maarufu, mwenye pesa zake na mwenye heshima ni nani?Au ni mwanasiasa?
Uwiiii ngoja nifunge bakuli sina mamilioni mie!
 
Hahahaaa,kumbe ni maneno ya mpiga ramli? Huyo mtu maarufu, mwenye pesa zake na mwenye heshima ni nani?Au ni mwanasiasa?
Uwiiii ngoja nifunge bakuli sina mamilioni mie!

Mwenzangu sijui bonge la bwana gani hlo, ila jide nae mshirikina, kwa hiyo huyo muhindi ndio mungu wake? Mmh kweli kazi anayo, anaacha kumuomba mungu anahangaika na waganga
 
Mwenzangu sijui bonge la bwana gani hlo, ila jide nae mshirikina, kwa hiyo huyo muhindi ndio mungu wake? Mmh kweli kazi anayo, anaacha kumuomba mungu anahangaika na waganga

Ndio team jide mlivyo wanga kwelii
 
Angetabiriwa kupata Mario mwingine tena angenuna

Kafuraia mwenyewe kusikia anapata mwanaume mwenye pesa, anasema kabisa mwaka 2017 sio mbali sana, kweli pesa mwana haramu
 
Huyo mpiga ramli yeye ana mafanikio gani?
 
Hahahaaa,kumbe ni maneno ya mpiga ramli? Huyo mtu maarufu, mwenye pesa zake na mwenye heshima ni nani?Au ni mwanasiasa?
Uwiiii ngoja nifunge bakuli sina mamilioni mie!

Atakuwa mh.....ngi
 
Dah watu mna mahaba balaa.. JD naye siku hizi kawa mfanyabiashara maarufu nchini? Duh hii ndo nimeisikia kwa mara ya kwanza... anafanya biashara gani?
 
Anatafuta namna ya kupata fedha kwa ledy jeydii anajikomba
 
Jide ni mmoja wa watu wanao changia mauaji ya Albino.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…