Ramli za Shafih Dauda kwenye usajili wa Yanga unaondelea

Ramli za Shafih Dauda kwenye usajili wa Yanga unaondelea

MCHA MBUZI Dauda anaendelea kwa kusema
Ili uweze kushindana na Simba unahitaji wachezaji wa aina ya Chama, Miquissone, Fraga, Kapombe, Manula, Mkude.

Unazungumzia Simba ambayo Nyoni, Miraji, Ndemla, wote hao wapo nje! Nimi naona timu ya kuipa Yanga ubingwa au kushindana na Simba, ipo ndani ya Simba.

Yanga ilibidi waibomoe Simba, kuna wachezaji ambao wapo Simba wanaweza kwenda Yanga halafu wapambane na Simba kwa sababu watataka kuthibitisha wao ni bora lakini Simba hawapati nafasi.

Mimi nategemea viongozi wa Yanga watoke wawaambie mashabiki kwamba wanajenga timu kitu ambacho ndio ukweli. Yanga bado haijatengemaa kupigania ubingwa sasa kuwaambia wanasajili timu ya kushinda ubingwa msimu ujao watakuwa hawawatendei haki mashabiki wao.
Wewe mikia tulia.
 
Ingawa Mimi ni Yanga ila katika hili Shaffii yupo sahihi
 
Mbumbumbu/Mikia FC ni wajanja kweli walita Yanga ibaki na timu ileile mbovu ya kuwasindikiza maadai wafunge magoli hivi kwa akili ndogo tu ile timu ingeweza kuchukua ubingwa?Viongozi nawapongeza kwa kuleta mapinduzi tunataka Yanga ya zamani sio hii ya kufungwa ni vitimu vidogo au hawa wazee wa simba
 
Huyo dauda ni mbumbu tu na mashavu yake kama mifuko ya timbalendi kwani timu za taifa huwa wanakaa kambini miezi saba?
[emoji23][emoji23] mashavu yake kama mifuko ya timbalendi [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwanza nawapongeza Yanga kwa event yao nzuri ya kilele cha Wiki ya Mwananchi, ilikuwa poa sana na wananchi wenye timu waliitika pale kwa Mkapa!

Baada ya yote hayo, Yanga wanahitaji kuwekeza muda na kujikita kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu ujao. Imebaki wiki moja tu kabla ya ligi kuu kuanza.

Yanga inesajili wachezaji wengi wapya baada ya kuachana na wachezaji (16) waliomaliza mikataba. Wapo wachezaji wapya kabisa kwenye ligi na wengine walikuwepo kwenye ligi lakini walikuwa vilabu vingine. Wamechelewa pia kupata makocha watakaoiongoza timu kwa msimu ujao.

Changamoto kubwa kwa Yanga naiona itakuwa kwenye eneo la ufundi, ujio wa kocha mpya siku chache kabla ya ligi kuanza halafu anakutana na kundi kubwa la wachezaji ambao hawakucheza pamoja msimu uliopita inaweza kuwa tatizo.

Kikosi cha Yanga kilichoanza mechi ya jana kilikuwa na wachezaji wanne tu (Metacha, Kaseke, Fei Toto na Nchimbi) waliokuwepo msimu uliopita, wengine walioanza walikuwa wageni.

Kuna wageni ambao watacheza VPL kwa mara ya kwanza, wanaweza kukutana na changamoto ya mazingira.

Ukiangalia kwa washindani wao wakubwa wa ubingwa wa VPL Simba, imesajili pia wachezaji kadhaa lakini kwenye mchezo wa jana ilianza na wachezaji wawili tu ambao hawakuwepo kwenye kikosi cha Simba msimu uliopita (Onyango na Morrison) waliobaki wote walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu uliopita.

Morrison ni mgeni Simba lakini sio mgeni kwenye ligi, Onyango ni mgeni kwenye ligi lakini mazingira ya soka la Kenya na Tanzania hayapishani sana. Yanga pia inawachezaji ambao si wageni kwenye ligi lakini changamoto yao wachezaji wengi ni wageni Yanga.

Dauda
 
Back
Top Bottom