Ramsey Noah amlilia Kanumba

Ramsey Noah amlilia Kanumba

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
ramsey-noah.jpg

Dar es Salaam.
Nyota wa filamu wa Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Noah amemkumbuka msanii mwenzake Steven Kanumba akisema ndiye aliyejenga daraja la ushirikiano kati yao.

Amesema Kanumba ndiye aliyewezesha ushirikiano kati ya Nollywood na Bongo Movie nchini Tanzania. Walicheza filamu mbili pamoja za Moses na Devil’s Kingdom.

"Nimemkumbuka Kanumba aliyekuwa wa kwanza kunileta Tanzania na kushirikiana katika filamu. Sitamsahau alikua mtu mzuri mwenye kupenda udadisi, kujifunza kuthubutu," amesema Ramsey leo Alhamisi Desemba 14,2017.

Ramsey yupo nchini ambako ameshiriki kongamano la kutambua fursa kwa vijana chini kwa mwaliko wa kampuni ya Sahara Tanzania.

Amesema atakwenda kuwasha mshumaa na kuweka maua kwenye kaburi la Kanumba Jumamosi Desemba 16,2017.

"Nawaomba Watanzania muungane nami katika kuweka mshumaa kwenye kaburi la Kanumba pamoja na maua," amesema.

Kanumba alifariki dunia Aprili 7,2012 baada ya kutokea mzozo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam na rafiki yake Elizabert Michael maarufu Lulu.

Lulu ambaye pia ni msanii wa filamu kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani kwa kumuua bila kukusudia Kanumba.

Mwananchi:
 
Ila watu wauaji aiseee kuna siku flan hivi niliona youtube na kichw kilisema Ramsey Noah has passed away source of death car accident sikutaka kuendelea kujua nin kilichomo ndan kwa uchungu niliojihis afu leo naona kitu tofaut aiseee watu hatupndan hivi
 
Huyu jamaa ndo alinifanya nizipende Nigerian movies! Enzi za True Love, My Love, Honey, Real Love, enzi hizo bado barobaro...daah! Very nice guy!

Halafu wakijezaga na mzee Peter Edouche, ni balaa!

Ngoja nidaunilodi movie yake, nikimalizana na wagonjwa nikaiangalie...
 
kwakweli huwa patamu sana hapo, jamaa anakua masikini anampenda mtoto wa Peter, afu mdingi hataki binti awe nae
 
Huyu jamaa ndo alinifanya nizipende Nigerian movies! Enzi za True Love, My Love, Honey, Real Love, enzi hizo bado barobaro...daah! Very nice guy!

Halafu wakijezaga na mzee Peter Edouche, ni balaa!

Ngoja nidaunilodi movie yake, nikimalizana na wagonjwa nikaiangalie...
Hasa.. my love .. ilipendwa sana hii movies
 
ndio anajua sana jamaa, afu naona wanawake wengi wanampenda kama walivokua wanampenda kanumba
 
Back
Top Bottom