Ranga Chivaviro yeye ni Yanga tu

Hawana ubavu labda ahiari mwenyewe. Hawana hela.
Huko aliko mshahara wake dola 150,000 kwa mwezi, watalipa hawa makolokolo hawa?
Acha ujinga ww hakuna mchezaji wa kulipwa dola 150k pale!! Yule mshahara haufiki dola 50k .

Mnatamka hovyo hovyo pesa bila heshima!! Unaijua dola?
 
Ni usajili wa kimhemko( kama kweli atakuja), kwanini wasiletwe mawinga na fullbacks wazuri sababu hayo ndio maeneo yenye mapungufu makubwa.

Yanga hatuna haja na mshambuliaji.
Mshambuliaji anahitajika, ili Mayele apate nafasi ya kupumzika baadhi ya mechi. Mayele huyo kila mechi mpaka inafika time anakuwa ha perform kutokana na fatique ya mechi za mfululizo.
 
Mshambuliaji anahitajika, ili Mayele apate nafasi ya kupumzika baadhi ya mechi. Mayele huyo kila mechi mpaka inafika time anakuwa ha perform kutokana na fatique ya mechi za mfululizo.
Mayele haanzi kila mechi halafu huyo chivaviro ni mchezaji wa kuanza sio bench.
 
Mayele haanzi kila mechi halafu huyo chivaviro ni mchezaji wa kuanza sio bench.
Sijasema kuanza, ni kucheza.
Na sababu ni hiyo, hakuna wa kaliba yake. Wenzake wanaweza kukaa hata mechi mbili bila kupangwa, wanafanya rotation. Yeye hata kama kocha anampango wa kumpumzisha, basi lazima amuweke standby, timu ikichelewa kupata matokeo aingizwe.
Sio Chiva tu, hata Mayele sio mchezaji wa kukaa benchi lakini wale sio marobot, wanahitaji muda wa kutosha wa kureserve nguvu ili wa perform vizuri zaidi na njia bora zaidi ni hiyo rotation.
 
Mtu mwengine ni dogo mmoja anaitwa KATLEGO OTLADISA hajaonekana akifunga sana ila Yuko poa sana ni maelekezo(coaching) tu yanahitajika na tulimuona Kwa mkapa alivosumbua na Umri26 wake kijana unafaa.
Ranga chivaviro, Ranga amekua na Umri mkubwa kulinganisha na dogo huyu kwani ameifungia sana team yake hasa mabao ya ushindi, umri30 SI mbaya sana.

Kwangu Mimi naona Otladisa anafaa kuja Kati ya Simba,yanga, ama Azam. SI lazima mtu awe ameifungia mabao mengi Cha msingi ni uwezo tu na makocha tunao.
 
Suala la uchovu unalikuza sana kuliko uhalisia. Ligi yetu ina vilabu 16 tu hivyo kwa msimu Yanga Fc inacheza mechi 32 ambazo ni chache kufananisha na ligi kubwa duniani.

Kuwa na mastriker wanaotofautiana uwezo ni jambo la kawaida tu kwenye mpira na kwa ligi yetu hapa Musonda na Mzize wanatosha kabisa.

Mimi sioni ni vipi Chivaviro anaweza kucheza na Mayele.
 
Ni usajili wa kimhemko( kama kweli atakuja), kwanini wasiletwe mawinga na fullbacks wazuri sababu hayo ndio maeneo yenye mapungufu makubwa.

Yanga hatuna haja na mshambuliaji.
Usijiongopee mkuu, timu ya mataji inatakiwa iwe na watu yani kwenye namba inatakiwa wawe wawili wawili wenye uwezo unaolingana na sio anaumia Mayele alafu nje back up yake Mzize ni uongo huo, Mzize mzr ila bado anajifunza, na ilipofika Yanga kwa sasa inahitaji kuwe na watu mana tumeonesha ubabe msimu huu msimu ujao tutakamiwa sana, hizo nafasi ulizosema zizibwe na fowadi pia ya kiwango iongezwe, kama man city vilee..
 
Ni usajili wa kimhemko( kama kweli atakuja), kwanini wasiletwe mawinga na fullbacks wazuri sababu hayo ndio maeneo yenye mapungufu makubwa.

Yanga hatuna haja na mshambuliaji.
Kuna hati tati ya mayele kuondoka
 
Angalia kwa mapana mkuu, ligi ina timu 16 lkn kwa ss mashindano ni mengi kuna azam confederation, kuna ligi, kuna mapinduzi alafu kuna caf, siku hizi timu zetu hazitoki mapema huko CAF, ukiwa na kikosi chembamba unakata moto mapema.
 
Simba hawana pesa za kumtoa mchezaji south
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…