Range Rover Velar VS Land Cruiser Prado

Rich people problems
 
Labda ajue anahitaji nini, maana kila gari hapo lina specialization
 
Tatizo lao wamekariri, wao kutoa vocha tu basi masimango mji mzima hawaamini km kuna watu wananunua range kwa ajili ya wake zao
 
Mkuu Isanga family naweza kupata mawasiliano yako (hata private message).

Kama nilivokueleza, juzi, kuna jamaa yangu anahitaji msaada wako kuhusu kuagiza gari kutoka S.A.

Nakutegemea sana boss

Nisaidie mawasiliano yako.

Point yangu ni kuwa nataka nimpe mawasiliano yako atakucheki moja kwa moja, kuliko hivi nauliza maswali , unanipa jibu, anauliza tena swali.
 
OK karibu PM mkuu nikupe namba wiki mbili hizi nashinda kwenye minada ya magari ni rahisi kupata majibu sahihi.
 
Kwamba wanaume wote wenye 40+ wametununulia ist hivi mnaishigi kwenye dunia ipi? Huku mtaani hiyo foleni si ingekuwa balaa,
Niliandika hivi kama trick.. hali ya uchumi sio rafiki, ila naamini wanaume wengi wanapenda sana kuwapa raha wake zao kwa vitu vizuri.. sema mifuko sasa imeroboka
 
Waambie jibu rahisi tu, kuwa na pesa sio kuwa na ufahamu wa kila kitu au kujitenga na jamii.

Binafsi sioni shida mtu mwenye hela nyingi kuja kuuliza jambo la kawaida au ushauri hapa, JF ni jamii.

Kuna matajiri ni wanyenyekevu sana, achana na ambao akiwa na milioni mifukoni anaona kila mtu mjinga.

Mimi nimekuelewa sana Mkuu
 
Watu hawajui hayo matokeo yake wamenikwaza mpaka nimetoa maneno yasiofaa.

Kosa lilikua kuuliza Range na Prado, ningekua nauliza Passo au IST wasingeongea yote hayo.

Ndiyo binadamu na kila mtu na malezi yake tunavumiliana.
 
Hivi umeongea nini yaani Mercedes Benz G wagon ufananishe na Land Cruiser hizi gari mnazozizungumzia mnazijua kweli au mimi sijaelewa Mercedes G wagon ufananishe na LC tena unasema imezidiwa?.
G wagon naijua pengine hata unavyoifahamu! Usiangalie kwamba gari maarufu au kisa inatumika na celebrities ndio ukamilishe kwamba itakua bora! Land cruiser ni gari ile haswa tena au pengine kwavile zipo nyingi ndio unazionea jau
 
Jana tumekaa kijiweni nikaona jamaa kafungua hii thread kamwaga upupu kwa mtoa uzi alafu zikapita karanga kamuomba muuzaji za kuonja

nipo hapa naangalia comment yake
 
Wewe kachangie kwenye nyuzi ya kuliwa kimasihara, huku umekua kituko
 
Mimi nimemtema huyo jamaa yaani G Wagon ambayo inaweza kununua hizo Land Cruiser mpya 4 harafu anafananisha ubora na mapumziko kwenye hizo gari na anatumia nguvu kweli Watanzania wengi hawayajui magari aisee hii mambo huwezi kumkuta Mzambia/Mkongo DRC akilinganisha haya magari hata awe wa kijijini ila Mtanzania wa mjini kabisa anaongea hiki kitu..
 
Wewe ndie unaliwa kimasihara chakula cha mwenye gari! Kwa comments zako nimeona kabisa hujui kuhusu magari ila unafosi tu,
 
Umenikimbia kwakua huna hoja usikute hata hizo g wagon hujaziona live unatishia kuona kwa ma celebrities, usiangalie bei ya kitu ndio ubjtimishe kwamba itakua kimara kuliko ziingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…