Ranger Cookies - karibuni jikoni

Ranger Cookies - karibuni jikoni

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,328
Reaction score
23,909
Wapendwa tunawasalimu wote,

Mimi na mwenza wangu Evelyn Salt salt tunawakaribisha jikoni kwetu. Leo tutatengeneza 'ranger cookies' sijui kwa kiswahili tutaziitaje...biskuti za ???

IMG_20161214_023400.jpg



Njia rahisi ya kupika ambayo alinifundisha mke wangu (hasa kwenye baking) ni kutoa kila utakachokihitaji na kukiweka mezani kisha kila ukishakiweka kwenye chombo cha kuchanganyia unakirudisha kabatini.

Screenshot_20161214-080919.png


Pichani: sukari nyeupe, unga, mayai, mixer,...andaa mahitaji yako yote kabla hujaanza kuchanganya.


Kwa njia hii hutosahau kuweka kitu na pia wakati unamaliza kupika hutokuwa na kazi kubwa ya kusafisha jiko lako.

Kwa mapishi haya hakikisha una jiko la oven, trays kulingana na jiko lako, kijiko cha chai, scoop ya icecream (kile kijiko cha kuchotea ice cream-si lazima sana ila tunakitumia ili kuzipa round shape), mixer au hata mkono unaweza kuchanganyia na kikombe cha kupimia.

Changanya hivi kwenye mixer yako au bakuli kama unatumia mikono kuchanganyia.


- margarine/siagi - robo kilo
- kikombe kimoja cha sukari ya kawaida
- kikombe kimoja cha sukari nyeupe
- mayai mawili
- vijiko viwili vya chai vya vanilla
- vikombe viwili vya unga wa ngano
- kijiko kimoja cha chai cha 'baking powder'
- wakati huu washa jiko lako liendelee kupata moto
- kijiko kimoja cha chai cha chumvi
- kijiko kimoja cha chai cha 'soda'
- vikombe viwili vya nazi (nazi iliyokunwa..sio tui la nazi, ile nazi yenyewe iliyokunwa)
- vikombe viwili vya cornflakes au oatmeal

Screenshot_20161214-080828.png


- baada ya kuchanganya pamoja unaweza kuongeza kama vijiko vinne au vitano vya chakula vya olive oil (unaweza kuongeza mafuta mengine yoyote ya kupikia ili kulainisha mchanganyiko wako zaidi lakini tunapenda olive maana haina harufu kama mafuta ya kupikia say ya alizeti)
- hakikisha mchanganyiko wako umechanganyikana vyema kabisa.

Kwa kutumia 'ice cream scoop' toa 'scoops' za mchanganyiko wako na uziweke kwenye sinia ukizipa nafasi ili zisishikane. Ingawa wakati unaviweka vinakuwa kana vimduara lakini vikiiva vinakuwa flat kama cookies/biskuti.

Screenshot_20161214-080509.png



Weka kwenye oven sinia zako kulingana na ukubwa wa jiko.

Oka kwa dakika 10 katika moto usiozidi digrii 350 - 375.

baada ya hapo toa cookies zako na ziache zipoe kwa muda kidogo kisha ziweke kwenye chombo tayari kwa kuliwa.

*** Usisahau kusafisha jiko lako baada ya kupika

Screenshot_20161214-081026.png



Muhimu zaidi: Usisahau kuonja baada ya kupika.

Sisi hupenda kuweka ice cream katikati (kama sandwich)...soooo yummy..


Karibuni wapendwa,

IMG_20161214_023735.jpg


Evelyn Salt & Mentor !
 

Attachments

  • IMG_20161214_023735.jpg
    IMG_20161214_023735.jpg
    100.4 KB · Views: 121
Karibu sana mkuu!

Ukioa utalazimika tu...
Mkuu unaonaje ukanitumia hizo biskuti zako kwa bus nizipeleke TFDA? Huenda kuna vitu umeviongeza hasa Sukari.

Alafu nivile nikupe Credits!
 
Mkuu unaonaje ukanitumia hizo biskuti zako kwa bus nizipeleke TFDA? Huenda kuna vitu umeviongeza hasa Sukari.

Alafu nivile nikupe Credits!


Nitumie address yako bado tumebakiza kadhaa...
 
ukhuty tushamaliza kachumbari sasa tupo kwenye dessert! Karibu sana..
 
Back
Top Bottom