Rangi gani nzuri kupaka nje ya nyumba?

Rangi gani nzuri kupaka nje ya nyumba?

Skimming ni tofauti na binder, skimming ni ile powder inayochanganywa na maji na kusongwa kupata kitu kama ugali halafu inapakazwa kwenye ukuta uliokwisha chapiwa, ndio foundation ya mwanzo kabisa kwenye maandalizi ya kuelekea rangi...kwenye gari unaweza ifananisha na 'puti'

Baada ya kufanya skimming, ukuta utapigwa msasa mlaini, then utapigwa white emulsion, then binder halafu mwisho rangi
Kwenye ujenzi, inabidi maranyingi we mwenyewe uwe na maarifa ya ujanzi.

Mafundi wengi hawa akina fundi Dula wengi wanajua kuskimu, kupaka white emulsion mwisho rangi. Hawatumii sadle binder mpaka umshtue na hajui kazi akkle
 
Binder ni muhimu endapo ume skim ikuta.
Hii ni kuua vumbi...kwani binder ni aina ya gundi.
Anaweza kutumia hata billion binder au sado binder

Pia inasaidia kupunguza tatizo la fangas za ukuta
Hawa akina fundi Roja,fundi Dula wanaswma eti bider ni mbwembwe, eti sio lazima kwasababu tu ukuta haukatai.
Kuna mtu hapo juu kamwambia mwenzake eti ndoo moja ya weatherguard anapiga nyumba nzima na wala hamwambii kuwa kitaalam rangi inapigwa coa 3 baada ya coat moja kukauka.

Mwingine anasimplify eti binder sio lazima[emoji3][emoji3]
 
Binder muhimu jamani

Sema kupiga coat 3 inategemea na Rangi yenyewe

Ila zisipungue mbili
 
Hawa akina fundi Roja,fundi Dula wanaswma eti bider ni mbwembwe, eti sio lazima kwasababu tu ukuta haukatai.
Kuna mtu hapo juu kamwambia mwenzake eti ndoo moja ya weatherguard anapiga nyumba nzima na wala hamwambii kuwa kitaalam rangi inapigwa coa 3 baada ya coat moja kukauka.

Mwingine anasimplify eti binder sio lazima[emoji3][emoji3]
Coat 3!?? Jamani mbona hatari
 
Hii bei yake mkasi, kopo moja la liter 4 tu huku kwetu tunanunua kwa 90,
Sema hii kampuni wamekuja kivingine ni inter pure

Naomba nikueleze kwa uwezo wangu na uzoefu wangu wa ufundi mwaka wa 9 sasa nipo kwenye ufundi finishing,

Kwa upande wa nje ili upake rangi na idumu kwa miaka mingi kama plaster yako ulifuata vipimo sahihi nikiwa na maana haukuibania cement,
Basi unaweza kuskim kwa kutumia michanganyo ifuatayo,
Gundi+white cement
Gundi +Cement ya kawaida,
Gundi +Jk wall putt
Emmusion + cement ya kawaida
Hapo ukuta wako utakuwa imara zaidi na hauta jutia,

Upakaji rangi,
Viwanda vizuri vinavyo ongoza kwa kudumu mda mrefu bira kupauka wala kuonyesha kasoro yoyote ni
1.Jotun
2.plascon
3.Gold ster
Nitaelezea sifa na ubora wa kila kiwanda

1.Jotun,
Hiki kiwanda ni ghari sana kutokana na material yaliyotumika kutengenezea rangi,
kwa rangi hizi huvutika yaani hutengeneza kama karatasi fulani ang'avu, pia unapoipata uziba mashimo ana mikwaruzo ya misasa, hapa hauta iona.

2.plascon
Hiki kiwanda zamani ndo kilikuwa kinaitwa Sadolin, Tunaweza sema hawa ndio waliokuwepo tangu enzi na enzi, ubora wao kwanza rangi zao huwa nzito sana na haipauki hata ipite miaka 10 nyumba utaikuta vile vile,
Hawa walikuza wakazalisha kitu kinaitwa
Binder,_Hii kazi yake hupakwa baada ya kupaka Emmusio rangi yeupe ya kutanguliza kusafisha vumbi ndipo utapaka Binder ili kuzuia fangasi wa nyumba,
Ukiona rangi imepakwa baada ya mda unaona rangi inaanza banduka au kuonyesha kuchoka haraka basi ujue ni fangasi kwenye ukuta, maranyingi huletwa na unyevu nyevu kwenye ukuta wakati wa masika.

2 .Gold ster,
hii huwa ni nzito na inaweza pauka lakini sio haraka kivile pia huwa inang'aa,
𝐍𝐚𝐨𝐦𝐛𝐞𝐧𝐢 𝐧𝐢𝐢𝐬𝐡𝐢𝐞 𝐡𝐚𝐩𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐚𝐦𝐚𝐬𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐧𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢𝐛𝐮 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐧𝐠𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐮𝐞𝐥𝐞𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐧𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐚 𝐟𝐮𝐧𝐝𝐢 𝐦𝐰𝐞𝐧𝐳𝐚𝐠𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐡𝐢𝐬𝐢 𝐤𝐮𝐧𝐚𝐬𝐞𝐡𝐞𝐦𝐮 𝐧𝐢𝐦𝐞𝐬𝐚𝐡𝐚𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐢𝐫𝐞𝐤𝐞𝐛𝐢𝐬𝐡𝐚,
mtaalam unaizungumziaje coral paints?
 
Back
Top Bottom