Sibonike, wewe ni memba mzoefu tu hapa JF hivyo nina imani una exposure ya kutosha.
Kama ulivyosema Jezi za Taifa sio lazima ziendane na bendera ya Taifa lakini kusema kuna ujuha wa kukwepa rangi za Yanga nafikiri hautoi suluhu ya msingi ama mawazo chanya.
Mi nilifikiri kwa kuwa hatuna rangi rasmi za nyumbani wala za ugenini basi tungekuwa na mjadala mpana kuhusu Jezi rasmi ya timu ya Taifa.
Angalia hata timu yako ya Yanga ni kwamba hawajitambui Jezi yao ya nyumbani ni ipi wala ya ugenini ni ipi. Yanga wana rangi tatu Njano, Kijani na less used nyeusi. Miaka ya nyuma na tulivyokuwa tukikua Yanga walikuwa wakivaa jezi za njano kama rangi kuu kwa nyumbani na kwa proportion kwamba fulana njano bukta kijani au fulana njano with green stripes. Ila miaka kama saba sasa Yanga wanavaa kijani kama rangi kuu na njano ni nadra na mechi nyingi Taifa wanavaa rangi za kijani. Msimu huu sasa mechi mbili ile na Ndanda na ile na Mtibwa wanavaa nyeusi kama rangi za nyumbani. Hadi hapo naamini hata wewe mwana Yanga umechanganyikiwa hujui jezi ya nyumbani ni ipi na ya away ni ipi.
Simba pia last week wameleta kituko Shinyanga kwa kuvaa jezi nyekundu ilhali jezi za ugenini ni nyeupe.
So ukiangalia kwa muktadha huu kama Taifa kuna tatizo la rangi za jezi kwa vilabu na timu yetu ya Taifa. Tuendelee kuelimishana iki kila mdau atambue jezi ipi ni sahihi na kwa mazingira yepi.