Rangi ya jezi Taifa Stars?

Hii timu imekua kama Changudoa, kila mtu anapiga bao tu. Yaani atujawahi kufurahia football kwenye nchi hii. Kila siku majonzi tu, dah!
itakua we mpenzi mpya wa kandanda..wakati tnamfunga moroko 3 ulikua unachunga kondoo,tulipompga bukinabe nje ndani ulikua wapi
 
Bashite na babaye wapeleke timu Russia??!!
Labda ya wasiojulikana!
 
Wacha wavae tu rangi yoyote.. tutachagua rangi tukipata timu muafaka.
 
Kuna ujuha wa kukwepa rangi za Yanga kwenye bendera ya Taifa. Basi watumie rangi ya blue complete

Sibonike, wewe ni memba mzoefu tu hapa JF hivyo nina imani una exposure ya kutosha.
Kama ulivyosema Jezi za Taifa sio lazima ziendane na bendera ya Taifa lakini kusema kuna ujuha wa kukwepa rangi za Yanga nafikiri hautoi suluhu ya msingi ama mawazo chanya.

Mi nilifikiri kwa kuwa hatuna rangi rasmi za nyumbani wala za ugenini basi tungekuwa na mjadala mpana kuhusu Jezi rasmi ya timu ya Taifa.

Angalia hata timu yako ya Yanga ni kwamba hawajitambui Jezi yao ya nyumbani ni ipi wala ya ugenini ni ipi. Yanga wana rangi tatu Njano, Kijani na less used nyeusi. Miaka ya nyuma na tulivyokuwa tukikua Yanga walikuwa wakivaa jezi za njano kama rangi kuu kwa nyumbani na kwa proportion kwamba fulana njano bukta kijani au fulana njano with green stripes. Ila miaka kama saba sasa Yanga wanavaa kijani kama rangi kuu na njano ni nadra na mechi nyingi Taifa wanavaa rangi za kijani. Msimu huu sasa mechi mbili ile na Ndanda na ile na Mtibwa wanavaa nyeusi kama rangi za nyumbani. Hadi hapo naamini hata wewe mwana Yanga umechanganyikiwa hujui jezi ya nyumbani ni ipi na ya away ni ipi.

Simba pia last week wameleta kituko Shinyanga kwa kuvaa jezi nyekundu ilhali jezi za ugenini ni nyeupe.

So ukiangalia kwa muktadha huu kama Taifa kuna tatizo la rangi za jezi kwa vilabu na timu yetu ya Taifa. Tuendelee kuelimishana iki kila mdau atambue jezi ipi ni sahihi na kwa mazingira yepi.
 
itakua we mpenzi mpya wa kandanda..wakati tnamfunga moroko 3 ulikua unachunga kondoo,tulipompga bukinabe nje ndani ulikua wapi


By the way nimezaliwa Dar es salaam, na naishi mbele, usifikiri wote tumekuja kama wewe
 
Kawaida kwenye timu ya taifa lazima kuwe na basis ya rangi ya jezi kwa timu ya Taifa. Mjadala uanzie hapo. Mengine yatakuwa madoido tu na utekelezaji zaidi.
Rangi iwe based kwenye kitu gani hasa?
 
Hapo ndipo tunapoanzia kushindwa,maana hatujitambui.

1980 -kurudi nyuma timu ilikuwa inavaa jezi za njano na bukta nyeusi. Jezi ikiwa na mistari mieusi miwili kifuani toka kulia kwenda kushoto timu ikiwa na wachezaji hawa:

1- Juma pondamali mensah
2-Daud salum bruce lee
3- Hassan Zitto/Mohamed kajole
4-Salum Amir
5-Jellah Mtagwa
6-Mohamed Adolf Richard
7-Omar Hussein Keegan
8-Hussein Ngulungu
9- Peter Tino
10- Mohammed Salim
11- Thuwen Allii
Haina chenga soka la maana Mashabiki hawaangalii jezi ni kushangilia tu.
 
jezi zetu huamuliwa na makuhani kutegemea na ugumu wa mechi
 
kama jezi zinasaidia kufuzu kwenye mashindano mbalimbali basi endeleeni kujadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…