Rangi ya ngozi ya Adam ilikuwa reddish-brown (kama mfinyanzi wa reddish-brown)

Leo baada ya kumaliza shughuli zangu za hapa na pale mchana nikaamua kupitia maktaba. Nilikuwa nasoma kuhusu mchango wa Afrika kwenye maendeleo ya dunia yetu, maana kuna chapisho na semina naandaa. Nikajikuta namsoma Mwanazuoni Cheikh Anta Diop na kuna maneno yake yalinigusa sana:

"When they explain their own historical past . . . that seems normal. Yet, when an African does likewise to help reconstruct the national personality of his people, distorted by colonialism that is considered backward or alarming. We contend that such a study is the point of departure for the cultural revolution properly understood."

Unapozungumzia historia ya mtu mweusi watu wa kwanza kabisa kukushambulia ni watu weusi. Kibaya zaidi mambo nyeti kama haya ya kihistoria tumeamua kufundishwa na jamii nyingine. Leo hii waandishi wakubwa wa historia ya Afrika wanatoka Oxford, Cambridge, Vatican, Harvard, Georgetown, nk.

When it comes to African History and Identity our intellectuals are in a state of despondency.
 
Bado siamini Kama watu wa kwanza kuishi duiani ni hawa watwao Adam na Eva! Huo utakuwa ni uleule utapeli wa mzungu.
Maswali kama haya ni mazito sana na yanahitaji majibu yenye kueleweka ambayo taasisi nyingi za kidini zinakataza watu wasihoji. Kama wakihoji basi majibu yanayoeleweka huwa hayatolewi: Dunia ni sayari kongwe mno na ina mamilioni ya miaka. Sehemu kubwa ya historia ya huu ulimwengu hatuifahamu vizuri.

Kuna ushahidi mwingi wa kihistoria unaoneesha kwamba sisi binadamu wa leo homo-sapiens siyo wenyeji pekee wa hii sayari. Kuna jamii nyingine zilishawahi kuwepo kabla yetu: Kuanzia mimea hadi wanyama. Hivyo majibu ya maswali ya nini kilitokea hadi tukafika hapa ndiyo nadharia mbalimbali zinaingia kujibu. Kuna nadharia za kidini (Creationist Theory) na Kisayansi (The Big-Bang, Tidal Gaseous and Evolution Theories).

Jamii nyingi za dunia hii, tena ambazo hazikuwa na muingiliano mkubwa kabisa zimekuwa zikiamini katika The Creationist Theory. Japo maudhui yametofautiana katika kuelezea hii nadharia, lakini mambo mengi sana yamefanana kama uwepo wa nguvu ya ulimwengu wa roho (The Supernatural ) katika kutawala ulimwengu wa mwili (The natural world): Uwepo wa Mungu na miungu (Theism): Uwepo wa maisha baada ya kifo (The Afterlife/Reincarnation/Purgatory/ Paradise).

Mfano mzuri ukiangalia dini za kale za Kimisri, kuna mambo mengi sana yameshabihiana na maelezo ya dini ya Kiislamu na Kikristo. Mfano uwepo wa siku za hukumu (Kiama/Judgement Day) na mambo yatakoyofanyika zimefanana sana. Ukisoma zaidi historia inasemekana taswira ya kuzimu ya Waislamu (Moslem Inferno), imefanana sana na taswira ya kuzimu ya wamisri ambayo iliandikwa kwenye kaburi la Mfalme Set wa kwanza (Set I) ambaye alitawala miaka 1700 kabla ya kuandikwa kwa Kurani.

Binafsi mimi ni muumini wa The Creationist Theory kama ilivyoandikwa kwenye Biblia: Ambacho huwa nakikataa ni kutafsiri Biblia kimapokeo kama ambavyo wanadini wengi wanafanya. Mapokeo ya kidini ndiyo yametuletea matatizo lukuki ambayo dunia inayashuhudia mpaka leo. Hivyo hata wewe unavyohoji vitu kama hivi, nadhani uko sawa kabisa: Hoji kabla ya kuamua kuamini chochote kile.

Nadhani pia uko sawa kuhoji kwasababu kama wazungu walikudanganya kwenye mambo mengi, kwanini usiwahoji kwenye hili suala la dini ??? Nini kinatufanya tuamini kwamba kwenye dini ndiyo hawajatudanganya?

Ukifuatilia mazungumzo ya LAWINO na mumewe OCOL utafahamu jinsi ambavyo Waafrika tunatakiwa kuhoji mambo mengi sana ambayo yalikuja kwa mashua na ngamia.

Develop a sense of Health Skepticism.
 
Umenena sawia kiongozi.
 
Mkuu, mimi ninaamini kabisa kwanza kuna pre Adamic world Kisha kukawa ulimwengu huu tulio nao. Na hata huu tulio nao nadhani before Adam walikuwepo wanadamu wengine waliokwisha kuwepo isipokuwa Mungu alimuumba Adam as a special Priestly race kwa ajili ya kupata race ya makuhani wa kusimamia ibada za kumwabudu yeye Mungu duniani.

Katika research zangu ndogo ndogo za fujofujo niliwahi kukumbana na hii ktk quora.com... the story of Adam and Eve doesn’t describe the creation of all humans, but just a specific lineage of humans, namely the lineage that gave rise to the ancient Israelites. Other lineages of people already existed.

Adam and Eden huwa ninaiwazia kuwa it was like maskuira kama inavyoonekana katika movie ya "wonder woman"
 
Mlijuaje haya? Nani alisema!? Mnayapata wapi
 
Aisee jamani MNA data hatari
 
Hivi mmejuaje kama alikua na rangi hiyo? Kitu kama huna uhakikanacho wala andiko katika vitabu ni heri ukae kimya.
 
Kuna baadhi ya wasomi wa Biblia wanaamini kuhusu Pre-Adamites. Mfano marehemu Dr. Finis Jennings Dake alikuwa anaamini kuhusu Pre-Adamites na akafanya tafiti ya zaidi ya miaka 35 na kutoa machapisho(Documentary). Machapisho yake mengi yanapingwa kwasababu wanasema ni uzushi (Heresy).

Lakini kitu kingine ambacho kinaleta utata ni kuhusu uumbaji. Watafiti wa historia ya vitabu vya dini hasa Torati na Biblia wanasema tokea Adamu hadi sisi ni miaka kama 7000-6000 hivi. Lakini tafiti za kisayansi na kihistoria zinaonyesha kwamba dunia ni kongwe zaidi ya miaka 7000-6000: Hivyo haya yamepelekea dunia kuzuka kwa mjadala mkubwa kuhusu uhalali wa vitabu vya dini kama Torati, Biblia, Taldmud, Kurani nk.

Ila wasomi wengine wa Biblia wamekuja na nadharia ya MWANYA (The Gap Theory), ambayo inakubali kabisa kwamba kuna mambo mengi kuhusu dunia na uumbaji hayakufanyiwa nukuu kwenye Biblia. Pia wanakubaliana na sayansi kwamba dunia ni kongwe zaidi ya miaka 7000-6000 na mambo mengi kabla ya Adamu na Hawa hayajaandikwa. Kitu ambacho wanatilia mkazo ni kwamba kutoandikwa kwa haya mambo hakuondoi UUNGU wa JEHOVAH.

Pengine tuseme tu kwamba kitu ambacho ni kibaya kwa hii dunia yetu ni kwamba sehemu kubwa ya maandiko ya Manabii na Mitume yamopotea na kufichwa. Sambamba na hilo, sehemu kubwa ya historia ya dunia imefichwa na kupotoshwa kwa maksudi na makundi ya watu wachache wenye ajenda ovu. Iwe ni vitabu vya dini, falsafa, vifaa vya kale (Ancient Artifacts) na maeneo ambayo yangekuwa ni makumbusho, watu ambao wamejipa ukubwa wa dunia hii wameficha.

Hebu fikiria The Dead Sea Scrolls imegundulika miaka ya hivi karibuni, lakini ukifuatilia kwa undani sehemu kubwa ya Biblia (Agano la Kale) imeandikwa mle. Wanadai kwamba yale maandiko yana siri nyingi mno na mengine yamefichwa.

Kuna mangi sana yanaendelea hapa duniani na sisi hatuyajui, haya mtu kama Marehemu Donald Rumsfeld huita: The Unknown Unknown au Things that we don't know we don't know .
 
Dada wa kiisrael ambae anaujua ukweli kutoka moyoni, ilimshinda akaamua kusema ukweli... Waafrika njooni mchukue nchi yenu Israel, japo aliwatag African Americans.. maana nyinyi ndo wakazi halali. Point yangu ya msingi hapo ni kwamba hata wazungu wenyewe waliojazana Israel wanaojifanya ni waisrael, wanajua kabisa sio kweli. Wao ni wazamiaji tu

Your browser is not able to display this video.
 

Uko sahihi ndugu , mummies wengi hawana pua
 
Hii ni sahihi, maana hata yule kauzu aliyemuua ndugu,yake Kaini..alipofukuzwa na Mungu kwa kosa la kumuua ndugu yake alisema naogopa watu nitakaokutana nao wataniua. Mungu ikabidi amuweke alama usoni ili watu wasimuue..hao watu ni kina nani? Unakuja gundua kulikuwa na watu wengi tu. Adam sio binadamu wa kwanza
 
yes, akina netanyahu ni khazarian mafias from black sea.
 
Vitabu vingi vimeanza kuwekwa wzi hata ktk splay store. Unaweza ukapata The book of enock ambacho kina elezea mambo mengine mazito yaliyobadili dunia kama mwanzo wa uovu,vita uchawi nk pia kuna kitabu cha Yashari-Jasher, Lost Books of the Bible etc ambavyo vingi ni vile vilivyokatika dead sea schroll
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…