Rashid ''Afisa'' Sisso

Rashid ''Afisa'' Sisso

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
RASHID ''AFISA'' SISSO

Nimemfahamu Rashid Sisso toka udogo wangu na nikimjua kama mmoja kati ya wanachama wakubwa wa TANU.

Nilipoanza utafiti wa historia ya TANU katika miaka ya 1980 ndipo nikaanza kumtafiti Rashid Sisso kwa undani zaidi.

Leo nimebahatika kupata picha yake ya ujana ya miaka ya 1950 ambayo inamuonyesha haiba yake kwa ukamilifu.

Lakini katika historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru Rashid Sisso humkuti popote.

Nimeangalia kwenye kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere kilichoandikwa na Prof. Shivji na jopo lake, Rashid Sisso hayumo.

Katika kitabu cha Abdul Sykes jina la Rashid Sisso linatokea mara 10.

Nimemtaja Rashid Sisso mara 10 na kueleza mchango wake akiwa kijana mpiganaji katika Bantu Group, vijana wahamasihaji na walinzi wa viongozi wa TANU.

Si haba.

Mara ya kwanza Rashid Sisso anatokea kwenye kurasa za kitabu cha Abdul Sykes, Rashidi Sisso yupo kwenye jukwaa la mkutano wa TANU Mnazi Mmoja mwaka wa 1955 kasimama nyuma ya Julius Nyerere Rais wa TANU.

Hebu msome Rashid Sisso katika wakati na ubora wake:

''Mmoja kati ya wazalendo walioanzisha Bantu Group alikuwa Rashid Sisso.

Wakati wa harakati za kudai uhuru alikuja kuwa karibu sana na Nyerere; na Nyerere akambandika jina la utani ''Afisa.''

Katika mikutano ya hadhara Sisso alikuwa akisimama nyuma kabisa ya Nyerere kama mpambe wake.

Nyerere alipotaka kusisitiza nukta fulani katika hotuba yake alikuwa akinyamaza kusema kwa muda na kumgeukia Sisso.

Kisha atamuuliza Sisso, ''Je siyo hivyo ofisa?''

Jibu la Sisso lilikuwa kupiga ukelele katika kipaza sauti.

Wasikilizaji hawakuwa wanaweza kujizuia.
Kwa pamoja walipiga vifijo na kushangilia.

Vibweka hivi vya Nyerere na Sisso vilikuwa havishindwi kuamsha morali za wasikilizaji.''

Leo mwanae kaniletea picha ya Rashid Sisso katika ujana wake labda ana miaka 30.

Rashid Sisso ni mmoja wa wanachama wa TANU waliomsindikiza Julius Nyerere Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza UNO 1955.

1659723715551.png

Rashid Sisso
 
Back
Top Bottom