Rashid Chilumba: Jitahada za kutaka watu wasikumbuke matukio ya October 29, mara zote haiponyi bali huongeza Machungu

Rashid Chilumba: Jitahada za kutaka watu wasikumbuke matukio ya October 29, mara zote haiponyi bali huongeza Machungu

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mwaka mmoja uliopita watu zaidi ya 500 waliuawa nchini Tanzania, wengi kwa kupigwa risasi za moto zilizofyatuliwa na wale ambao manusura, mashuhuda, vyama vya upinzani na mashirika ya haki za binadamu yanasema ni maafisa wa usalama waliodhamiria kuua.

Kwa yeyote aliyetazama video za siku ya Oktoba 29, 2025 atakiri matukio yake yalikuwa doa kubwa sana katika historia ya Tanzania – nchi iliyojijengea jina kwa utulivu wa kisiasa licha ya malalamiko makubwa yaliyokuwepo kwenye mifumo yake ya uchaguzi.

Haikuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kukumbwa na vurugu za uchaguzi, zilikwishatokea mara kadhaa hususani visiwani Zanzibar, lakini kile upinzania umekitaja kuwa “ukatili wa vyombo vya dola” uliofanywa mwaka uliopita, ulikuwa cha kilele cha kutoridhika kwa wananchi
 
Back
Top Bottom