Mwanakijiji nakubaliana nawe majukumu iliyoyataja ya usalama wa raia, lakini sidhani ya kuwa hata hao wanaofanya kazi katika taasisi hiyo wanajua majukumu ya taasisi hiyo.Ukichunguza taasisi hii kama ilivyo ni kulinda wakubwa yaani rais na na viongozi wengine na mali zao kuandamana na viongozi katika safari zao za nje na ndani ya nchi.
Nina imani ya kuwa watanzania wengi wanaamini hivyo kua kazi ya taasisi hiyo ni hiyo. Kwani kama ingelikuwa inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za uwanzishaji wa taassisi hiyo matatizo mengi ya mikataba mibovu na mambo mengine yanayohatarisha usalama wa taifa yasingekuepo.
Sitashangaa ya kuwa moja ya majukumu yao wakiwa safarini na viongozi wetu ni kutumwa kuwawekea viongozi wetu mafisadi-WEZI-maana ufisadi sasa nikama sifa fedha katika akaunti zao na kuwanunulia mashangingi.
Kwa upande mwingine viongozi wa juu katika taassisi hii wanateuliwa na Rais itakua kichekesho kwa ofisa wa taasisi hiyo kutoa taarifa kwa Rais ya kua Mh.Rais wewe na marafiki zako Mafisadi-WEZI-Mnahatarisha usalama wa taifa.
Hivyo Mwanakijiji kitendo cha mkuu wa taasisi hiyo kujiuzulu ni sawa na kutoa kondoo wa kafara au kujaribu kujiliwadha si zaidi. Hapa chakufanya kwanza taasisi hinapashwa kua uhuru na iwe chini ya bunge na viongozi wake kuchujwa katika bunge na kulindwa na bunge. Kitu ambacho vile vile nakiofia kama kinaweza kutoa matunda yoyote. Kwani tatizo letu ni mfumo wa uongozi katika nchi yetu ,na katika mfumo huu wakati viongozi wengi kuanzia ngazi za juu rais ni mafisadi huu ni mduara au circle ambayo kuivunja ni vigumu.
Hapa matumaini pekee ni kelele za walalahoi,shinikizo la wafadhiri ndiyo njia pekee itakaowalazimisha viongozi wetu kufanya uchunguzi kwa kashfa nyingi zilizo tokea na kuendelea kutokea Mwanakijiji katika hali ilivyo hata ukiwekwa wewe katika nafasi hiyo utofanya chochote Lowassa, Karamangi, Rostam, chenge na wezi wengine wengi wamechukuliwa hatua zipi? Inauma ninapowaona watua hawa wamekaa katika viti vya bunge ni aibu!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Advocate Jasha