Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Shangazi amesema kuwa alimuandikia Dewji barua ya kumuomba kujiondoa kwenye bodi hiyo tangu Juni 2 mwaka huu, hii ni kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Simba.
"Kati ya mambo yaliyonifanya nijiuzulu ni kupisha mwekezaji kutengeneza safu mpya ya bodi itakayoisaidia klabu yetu, kwani hatukuwa na matokeo mazuri kwa kipindi cha misimu miwili hivyo nimefanya hivi kama sehemu ya uwajibikaji wangu," amesema Shangazi.
Amesema kuwa mwenendo mbaya wa timu hiyo umemfanya kupisha mwekezaji kutafuta watu wengine watakaoifikisha sehemu nzuri kama awali. Shangazi amewataka wanachama na mashabiki kuwa karibu zaidi na uongozi haswa katika kipindi hiki cha mapito.
Pia soma: Tetesi: - Boom: Wajumbe wote wa Bodi ya Simba upande wa Mo Dewji wajiuzulu