Rashid Shangazi: Nimejiuzulu Simba kama sehemu ya uwajibikaji

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
Your browser is not able to display this video.
Mbunge wa Jimbo la Mlalo na Mjumbe Kamati ya Bodi ya Uwekezaji wa Simba kupitia upande wa mwekezaji Mohamed Dewji, Rashid Abdallah Shangazi ameeleza sababu ya kujiuzulu kwake kwenye nafasi hiyo.

Shangazi amesema kuwa alimuandikia Dewji barua ya kumuomba kujiondoa kwenye bodi hiyo tangu Juni 2 mwaka huu, hii ni kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Simba.

"Kati ya mambo yaliyonifanya nijiuzulu ni kupisha mwekezaji kutengeneza safu mpya ya bodi itakayoisaidia klabu yetu, kwani hatukuwa na matokeo mazuri kwa kipindi cha misimu miwili hivyo nimefanya hivi kama sehemu ya uwajibikaji wangu," amesema Shangazi.

Amesema kuwa mwenendo mbaya wa timu hiyo umemfanya kupisha mwekezaji kutafuta watu wengine watakaoifikisha sehemu nzuri kama awali. Shangazi amewataka wanachama na mashabiki kuwa karibu zaidi na uongozi haswa katika kipindi hiki cha mapito.

Pia soma: Tetesi: - Boom: Wajumbe wote wa Bodi ya Simba upande wa Mo Dewji wajiuzulu
 
Hoyee
 

Attachments

  • FB_IMG_17177695544176742.jpg
    413.3 KB · Views: 6
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…