Divele Dikalame
Member
- May 4, 2010
- 77
- 12
RASIMU YA KATIBA MPYA
MAONI NA MSIMAMO BINAFSI WA AWALI KUHUSU RASIMU
- Rasimu haijibu kero za mungano na wala ki mantiki haiimarishi muungano. Ni njia ya kisayansi ya kuua Muungano na sijui atakeye wanadganya wa Tanzania kuwa kuimarisha muungano ni kuwa na serikali tatu ni nani na anatupa insurance gani? Watanzania hawakuwa na lengo la kudai serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Rasimu hii, lakini tatizo kubwa la muungano lilikuwa utata wa utekelezaji wa mambo makuu ya kimsingi ya muungano.
- Kuna kila dalili kuwa Tume inayoongozwa na Mh. Jaji Warioba imezidiwa ujanja na makundi maalum ambayo ni hatari katika jamii yetu ya watanzania. Itakumbukwa kuwa kabla ya serikali kuamua kuunda tume tayari genge la wasomi wakiongozwa na Issa Shivji wa Kigoda cha Mwalimu, Kitila Mkumbo aliyekuwa makamu mwenyekiti UDASA na wengine wanaojiita waumuni wa Azimio la Arusha walikwisha anza kutu brainwash wakitumia mijadala ya kisomi iliyoonyeshwa moja kwa moja kwa wananchi kupitia TV, mijadala iliyofanyika kwenye ukumbi maarufu wa Nkrumah, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (live coverage pale Nkurumah Hall). Mambo yote waliyokuwa wanaropoka pale yameingia kwenye hii rasimu. Swali kwa nini yameingia kirahisi bila hata kuchujwa? Kweli mabilioni ya pesa yaliyotengwa kwa tume kufanya kazi ndo yameishia kunakili taarifa zilizokuwapo na kutuletea wananchi tuzijadili?
- Rasimu haijatimiza kiu ya wananchi wa Tanzania. Rasimu hii imetimiza kiu ya makundi ya watu wachache hususan Kigoda cha mwalim, CHADEMA, LHRC, Haki Elimu, MCT na MTF na Tanganyika Law Society. Kwa uhakika zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania hawajasikika na wamepigwa butwaa na matokeo ya Rasimu.
6. Tume hii ilipewa takribanshilingi bilioni 50 ili kufanya kazi, kuhoji watu na kutafsiri maoni yaokisayansi. Haitegemewi maoni yakeyatokane na taarifa ambazo ziliwahi kuandikwa hapo Zamani mfano NyalaliCommission au Kisanga Commission au Warioba Commission au Tanganyika LawSociety au Midahalo ya Katiba iliyokuwa ikiandaliwa pale Nkrumah Hall chuokikuu cha Dar-es-Salaam. Kufanya hivyo ni kuwanyima wa Tanzania waliowengikusikika. Kwa mshangao Tume imekiri kuwakuna wa Tanzania walitaka serikali mbili wengine nne wengine tatu. Lakiniyenyewe ikaamua kuchukua serikali tatu. Hii ni kosa kisayansi. Ilibidi kwanzaiainishe ni watu wangapi walisema tatu wangapi walisema nne wangapi walisemambili. Kamani kweli wanayotushauri basi wawe na ujasiri huo huo wa kunakiri maoni ya tumeya NYALALI NA KISANGA NA WARIOBA CORRUPTION COMMISSION WATUELEZE KWA NINI HAYOMAWAZO HAYAKUCHUKULIWA. Mbona hawatuelezi yaliyojiri wakati wa Jumbe na NjeruKasaka maana ilikuwa ni suala nyeti sana kama hilowaliloleta juu ya serikali tatu. Si busara kutumia taarifa ambazo zilitolewa na serikali hiyo hiyozikakataliwa hii ni kuleta kiburi cha kutaka kuilazimisha serikali mambo ambayoina sababu za msingi kuyakataa wakati huo ilipopewa hizo taarifa za Nyalali naKiasanga. SEHEMU YA PILI: · SERIKALIYA TANGANYIKA NA SUALA NYETI LA MUUNDO WA MUUNGANO WA SERIKALI TATU HAYAYANATOKEA WAPI?Tumeilisheheni wataalamu wengi wanaoheshimiwa sana nchinikutokana na umilisi wao mkubwa katika maeneo ya elimu waliyobobea. Lakini inaelekea hawakujisumbuakufanya utafiti wa kina juu ya sehemu hii iliohusu serikaliya Tanganyika na muundo mpya wa serikali tatu walioupendekeza. Hii inaonyesha wamekujana mawazo yao na mawazo ya vikundi ambavyo vimetajwa hapo mwanzo na kutaka kutulazimisha jamii yote ya wa Tanzania tuyaamini. Kwamfano;
- Suala nyeti la muungano. Inabainishwa katika tafiti mbali mbali ambazo tulitegemea Tume inayoongozwa na Jaji Warioba wazisome na kutupa mwongozo wa nini tujadili. Kwa watanzania wengi ambao hawakuwapo wakati muungano ukiasisiwa wangeweza kuelewa kuwa kuna kitu kinaitwa Article IV ambacho kwenye machapisho mbalimbali kinasema;
- Suala nyeti la Muundo wa Muungano: Muungano ni suala nyeti na tukufu ambalo ni lazima lilindwe kwa gharama yeyote ile kwa usalama wan chi yetu tukufu. Kwa kweli na mtu yeyote aneonekana kutaka kutikisa nguzo zake haina budi kumtolea uvivu ili kusambaratisha nguvu zake na kundi lake kwa kutumia rasilimali zenye gharama yeyote ile kwa maslahi ya taifa hili. Kama ilivyotanguliwa kuanishwa kwenye maandiko haya kuwa mifano ya mataifa kadhaa ambayo yamefuata serikali za shirikisho zimeenda na maji kwa kushindwa kusonga mbele kutokana na shida za utawala wa serikali za shirikisho. Hivyo Tume ilitakiwa kuwa ubunifu wa hali ya juu katika kufanya tafiti na uwasilishaji wa wanayoyaota mawazo ya watanzania ya kutaka serikali tatu. Udhaifu mkubwa katika taarifa ya rasimu ya katiba ni kushindwa kuwa wabunifu na kuchambua kwa kina muundo wa serikali. Kwa kiwango kikubwa uamuzi wao hautokani na maoni ya watu waliowahoji. Hii inatokana na ukweli kuwa mara baada ya kuchapisha taarifa kila mtu aliyehojiwa ameshangazwa na serikali tatu. Waliokataa sababu kubwa zaidi ya asilimia 90 ikawa ni kwamba Muungano utavunjika mara moja, ni gharama ambayo watanzania walipa kodi wata twikwa kuendesha serikali tatu badala ya kuelekeza fedha hizo kwenye barabara, shule na hospitali. Onyo hapa kuna wale wakosaji wanasema bora nchi iharibikiwe tukose wote. Hawa wanasaidiwa sana na coverage ya vyombo vya habari na ni hatari kwa usalama wa nchi hii. Wengi ni wapinzani na wana harakati ambao wanaishi hapa Tanzania lakini mishahara yao yote inatoka Ulaya. Hao wanasema bora Tanganyika ije na kwenye huu msafara kuna wanasiasa, kuna maprofessa walioshiwa hoja ambao wamekuwa wakiranda randa kwenye korido za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujikosha kwa vijana wa kizazi kipya wasiowafahamu. Wengi wanatumia kofia ya kumnadi Mwalimu Nyerere. Lakini Nyerere gani angependa serikali tatu? Ni vinara wa makongamano na Majukwaa ya wahariri, katiba nakadharika LHRC kupitia live coverage ya vyombo fulani vya habari.
- Tume haikuzingatia athari za mapendekezo yake: Pamoja kuwa tume ina majaji na wasomi waliobobea na wanafahamu yaliyotokea juu ya Muungano wa Serikali za Shirikisho kama hii ya Warioba Model itakuwa ni sababu kubwa muungano kufa kama ilivyotokea kwenye baadhi ya nchi duniani, hapa kuna mifano michache.
[TR]
[TD="width: 606"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 342"] <!--if (window.adgroupid == undefined) { window.adgroupid = Math.round(Math.random() * 1000);}document.write('<scr'+'ipt language="javascript1.1" src="http://adserver.adtech.de/addyn/3.0/1332/4486816/0/357/ADTECH;loc=100;target=_blank;grp='+window.adgroupid+';misc='+new Date().getTime()+'"></scri'+'pt>');//--> [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 606, bgcolor: transparent"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimekwenda visiwani Zanzibar, kuwapelekea wananchi serikali ya tatu. Kauli hiyo imetolewa jana visiwani humo na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akizungumza na wazee wa jimbo la Uzini kabla ya kuzindua kampeni za kuwania ujumbe wa Baraza la Wakilishi. Alisema CHADEMA inawataka Wanzanzibari waamue aina ya Muungano wanaoutaka tofauti na huu wa sasa ambao umezusha manunguniko makubwa. Aliongeza kuwa chama hicho kinaamini muundo wa serikali tatu yaani ile ya Tanganyika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hapa Tume itusaidie kujibu masuala yafuatayo walihoji watu wangapi, waliwapata vipi, profile zao zikoje na asilimia ngapi walisema nini na kwa nini? SEHEMU YA TATU KASORO NYINGINE ZA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA KATIBA MPYA
- Mfumo wa Utawala wa Serikali: inaonesha kuwa TUME imeshindwa kuweka bayana mfumo gani wa serikali wanataka Tanzania tuufuate Presidential System tunayoifahamu, au Parliamentary system au cocktail?
- Haki za Raia: Ni fikira ya kila mtu kuwa Rasimu hii haijitoshelezi katika eneo hili. Inazungmziwa juu juu tu na haki ni nyingi zingine ni contradictions. Elimu haiwezi kuwa ni haki isiyotafsiriwa. Haya ni mambo ya msingi na kuyaweka kwenye wajibu wa Serikali. Pia hapa tunapata shida maana hii imekuwa ikiimbwa kila mara na Slaa na wana majukwaa eti ohoo watanzania mnahaki ya kuihoji serikali kwa nini hamkupatiwa elimu? Wote tunajua kuwa elimu ya primary school ni ya lazima. Ukiweka kwenye katiba haki kama hizi uwe muangalifu usije ukajikuta unadaiwa kitu ambacho hauna uwezo nacho. Nadhani nivema kutafuta namna ya kuiweka.
- Mgawanyo wa Rasilimali: Kuna mambo ya msingi kwa wananchi ambayo katiba inatakiwa iyaangalie. Mfano sasa kuna kelele za rasilimali. Kwanza lazima katiba itamke wazi kuwa rasilimali zote ni mali ya wa Tanzania wote. Pia kwa wawekezaji ni lazima asilimia 30 ya mavuno ya rasilimali yabaki nchini au thamani yake. Mfano tumekuwa tukivuna tani 50 za dhahabu kila mwaka, katiba inaweza kusema angalau tani 15 lazima zibaki nchini wauziwe Masonara na Benki Kuu. Hii itakuwa na faida kwa masikini wengi kuliko mambo ya mamlaka, maadili, haki na tawala yaliyojaa kwenye rasimu iliyowasilishwa.
- Rasilimali Ardhi: Kuna hatari ya nchi kupoteza ardhi kupitia multinationals na land grabbing via FDIs. Rasimu ya Katiba haioneshi ni kwa jinsi gani ardhi yetu imelindwa. Nivema kusema ni marufuku mtu wa nje kuwa na ardhi Tanzania na kuwa na Land Lease ya zaidi ya miaka 20. Hivi sasa kuna uwekezaji unakuja na kusema land leass ya miaka 50, hii ni sawa tu na kununua ardhi kwani wa Tanzania waliopo sasa baada ya miaka 50 ni wachache sana watakao kuwapo. Hii iingie kweny rasimu.
- Katiba Mpya iende smabamba na Uchumi wa Kisasa: Uchumi wa Tanzania hivi sasa umeshikiliwa na sekta binafsi, informal sector na biashara. Lakini rasimu inaendeleza yale yale ya wakulima na wavuvi kwa mkazo. Hii ibadilike na pia mipango ya maendeleo hasa miaka mitano na 10 iingizwe kwenye katiba ili kuifanya serikali kila mara ilazimike kuwa na mipango. Haya ni muhimu kama vile walivyochukua nafasi kuubwa kuelezea mahakama.
- Idadi ya Wabunge ni Kituko: Katika rasimu idadi ya wabunge inayopendekezwa ni kituko. Labda tume itoe tafsiri mpya ya kazi za wabunge. Inataka kuturudisha miaka 50 nyuma. Tanzania ina wilaya zaidi ya 130 leo hii inasema mbunge mmoja kwenye mkoa mwanamke na mwanaume. Hii wameitoa wapi duniani?? Lengo ni uwakilishi kweli?? Hata suala la elimu siyo vema kuwabana sana watu. Hivi sasa siyo majungu zaidi ya asilimia 70 ya wabunge wa CHADEMA hawana elimu ya chuo kikuu mpaka Mbowe, Mnyika, Lema, Sugu, na wengine wengi. Je TUME imegundua nini kwenye viwango vya elimu.
- Muundo wa Muungano: Muundo wa Serikali tatu utaliangamiza taifa. Utakuwa ndio mwisho wa muungano. Hiyo tusijidanganye maana tumeona Malaysia na Singapore, Senegal na Gambia na mifano mingine. Tuangalie namna ya kuondoa kero za muungano. Tubaki na Serikali zetu mbili maana hapo hawa wanaomuimba Nyerere tuwaambie tunamuenzi kwa yale ambayo mpaka anakufa alikuwa akiyapigania kama ya muundo wa sasa wa muungano na isiwe ni unafiki tu. Kuna uhakika mkubwa hata kama angekuwa hai leo, mambo yote angewaachia kuyajadili na kufanya mtakavyo, lakini hili la muungano asingekubali angekuala na hao vishoka sahani moja mpaka angewateketeza wote bila kumuacha hata mmoja. Na labda hata Jaji Warioba ingekuwa ndio mwisho wake wa kuwepo kwenye medani za siasa za Tanzania. Kwani kwa mapendekezo haya asingemsamehe yeyote aliyehusika. Zanzibar isikilizwe na wanayoyataka na kuyalalamikia yafanyiwe kazi iwe aibu kwa hao mbwa koko wanaosubiri muungano ufe. Wengine ndo wanashabikia Mtwara na Southern States. Labda Tume itumie ujasiri kusema imeangalia kuwa Tume zote zilizopita zilipendekeza serikali tatu kusema kwa nini hazikusikilizwa. Hatuja sahau kwa nini Aboud Jumbe alipelekea kujiuzulu ni kile kitendawili cha 1+1 ni 3 alichoshindwa kumjibu Mwalimu Nyerere akasema 3. Wakaja wale waliojiita G55 hatuna shaka kama kwenye hii tume hawamo nao wakaja na jibu la 3 wakaenda na maji. Vipi wakina Kolimba na Malecela walipoambiwa hawamsaidii Rais. Nini msimamo wa Nyerere katika haya tume iwe wazi pia kuliko kukimbilia taarifa za jaji Kisanga na Nyalali. Nakumbuka msimamo wa CCM wakati Tume inayoongozwa na Mh. Jaji Warioba inakabidhiwa hadidu za rejea ulikuwa Muundo wa sasa wa muungano usijailiwe wala kutafutiwa maswali yeyote. Nia ya CCM ilikuwa Tume ikita ngivu zake kutafutia ufumbuzi juu ya kero za muungano wetu huu mtukufu na si vinginevyo. Msimamo wa CCM ni pamoja na msimamo wa Rais waJamhuri ya Muungano ambaye ni mwana CCM na Mwenyekiti wa Chama. Na ikumbukwe kuwa Jaji Warioba ni mwanaCCM, swali kuu kwake kashindwa kuitetea nafasi ya chama chake, kashindwa vipi kutetea msimamamo wa Mwenyekiti wake ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi? Jaji Warioba na Tume yake wameboronga kuliko ilivyotegemewa kwenye suala hili la mfumo na muundo wa sasa wa Muungano wetu adhimu kabisa. Makosa haya kwa watu wanaopigania muungano wetu hausemeki na wala hausameheki kirahisi. Wangeweza kuhoji U-CCM wa Jaji Warioba na uadilifu wake kwa Chama na Serikali yake.
- Vipindi vya Urais kati ya Tanzania bara na Zanzibar: Katika kushughulikia kero za Muungano Tume ingejaribu kupendekeza kupitia Rasimu yake kuwa baada ya vipindi vya viwili viwili vya marais wa wawili wa Tanzania bara basi nafasi hiyo iende Zanzibar kwa rais mmoja atakaepatiwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Kwa mfano Kupitia CCM, baada ya Tanzania bara kupata fursa ya kutoa Marais wawili (Rais Mkapa na Rais Kikwete) waliokaa kwa kipindi cha miaka 20, basi Wa Zanzibar wapate nafasi hii baada ya Rais JK watoe Rais atakae kaa kwa miaka 10. Kwa ufupi wa maelezo haya ni kuwa kwenye kipindi cha miaka 30 basi Bara wapate miaka 20 ya kuongoza nchi na 10 iende Zanzibar. Jambo hili lingefanyika na kuwekwa kwenye katiba basi tusingepata tabu leo ya kuona makundi mengi yakigombana kutafuta ujiko ndani ya mitaa yetu kwa minajili ya kupata Urais 2015. Kila mtu angetupa jicho upande wa zanzibari leo kuangalia ni mtu gani miongoni mwetu wana CCM ambaye anaweza kuwa amiri Jeshi Mkuu wa kuchukua kijiti cha Uongozi adhimu wan chi kwa minajili kulinda uhuru, amani na usalama wan chi yetu tukufu iliyoundwa na muungano wa watu wenye mtizamo mmjoja. Tunaomba viongozi wa juu wa Chama na Serikali, wakiungana na wale wa Vyombo vya juu vya Ulinzi na Usalama wan chi hii wamuulize haya kayatoa wapi? Mawazo haya yanamuwakilisha nani? Chadema na CUF hawa ni wasaliti wakubwa waanagaliwe sana. Mapendekezo haya siyo tu yametikisa nguzo za muungano wetu bali yamezivunja nguzo hizi, kwa hiyo Muungano umepwaya na una nyufa nyingi na za hatari kuvunjika.
- Nini hatari ya Kuvunjika Muungano: Tuna mkumbusha Jaji Warioba kuwa siasa za Zanzibari ziko salama kwa kwa ajili ya Muungano ambao umeimarika. Kama Muungano ukivunjika leo basi Zanzibari itanuka damu ya ajabu. Nawaomba wakuu wa Chama na Serikali na wale wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wan chi warejee Mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Zanzibar (Unguja) tarehe 04.11.2012. Kumbukumbu za Mkutano huu ziko kwenye CDs Ambazo sisi tunazo kama hawana sisi tutawapa waone wenyewe. Katika mkutano huo CCM walikuwa wanajibu kauli mbalimabli zilizokuwa zimetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wana CCM hawakuuma maneno kwa kauli za Matusi ambazo haziwezi kutukanika. Katibu wa Vijana wa Wilaya ya Mjini Magharibi aliweza kusema waziwazi kuwa wana Uamsho na viongozi wa CUF hasa maalimu Seif na Jussa wanakazwa au wanatiwa. Matusi haya yalipokuwa yanatolewa kulikuwa na nderemo zikiambatana na shamra shamra na vifijo na kadhalika. Kwa jinsi walivyokuwa wanazidi kutukana ndio furaha za wana CCM ziliwafanya waendelee kuwashangilia wasemaji, hasa huyu kijana Katibu wa Vijana na Mgeni wa heshima wa Mkutano huo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mzee Borafia. Mkutano huo ulifanywa siku mbili kabla Mkutano Mkuu wa CCM taifa wa taerehe 06.11.2012. Ni matumaini yetu kuwa Tume ya Jaji Warioba italiangalia hili kwa makini na kuibadilisha Rasimu kabla haijaenda kwa wananchi kujadiliwa na kutolewa mapendekezo.
- Kupoteza Legacy ya Utwala Bora wa Rais JK: Muungano ukija kuvunjika kwa ajili Muundo mpya wa Muungano unaopendekezwa na Rasimu itakuwa na athari kwa utawala wa mpendwa wetu Mh. JK . Tunawashauri wasaidizi wa karibu wa Mh. JK wasishindwe kumshawishi ili atumie kila linalowezekana aipige chini hii Rasimu ili kama watu wanataka muundo huo wa Muungano ambao ni hatarishi kwa uhuru, usalama na uhai wa taifa letu tukufu wasubiri rais mwingine asiye yeye. Kwani huo sio msahafu lakini kwa sisi ni wapenzi na wanachama wa CCM hatutopenda hili litokee kwa Kiongozi yeyote wa CCM anayeongoza nchi hii. Naogopa kuwa legacy ya mpendwa Rais wetu JK kuja kufananishwa na ile ya Rais Gorbachev wa USSR ya zamani iliyosambaratika.
- Tume ipewe muda irekebishe rasimu kabla haijaenda kwa wananchi. Hii ni kwa Mh Rais aliyewakabidhi kazi atengeneze jopo la wataalamu makini na waadilifu kutoka Bara na visiwani waipitie Rasimu na kwarudishia mapendekezo wana TUME ili warekebishe hasa yale mambo ambayo yanweza kuhatarisha amani, usalama na uhai wa Taifa hili lilioundwa na Muungano mtukufu wa Serikali tukufu za Zanzibar na Tanganyika KABLA YA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KWENYE MJADALA wa rasimu ya kupata Katiba Mpya.
- Articles of Union: TUME IKUMBUSHWE KUWA HAINA UWEZO WA KUGUSA NAKUBADILISHA MAMBO YALIYOKWENYE MUUNGANO. IMEYAPUNGUZA NA KUBAKI SABA KWA KUTUMIA KIGEZO KIPI? KWA RUHUSA YA NANI?? HAYA YANAONDOAJE KERO ZA MUUNGANO??
- Kwa sasa kuna umuhimu wa kufuatilia kwa karibu nyendo za Tume, watu wanao-infulence na mitazamo yao huwezi kumuamini kila mtu tuna wakina GORBACHEVU wanataka tuingie kwenye historia ya kuibadili Tanzania mwelekeo. Inashangaza MCT kupewa kipaumbele kwenye maoni ya Katiba kuwemo kwenye Mabaraza ya Katiba. Ni wazushi na wasaliti wanaodunduliza pesa za wafadhili kuja ku BRAIN WASH WATANZANIA. Kimsingi MCT si chombo cha kubeza. Kina watu wachache wanaoweza kuwa hatarishi kwa namna moja au nyingine. Baadhi ya wajumbe wa bodi zao wanaandika makala katika magazeti tata kama vile Mawio au Mwanahalisi ambalo kwa kiburi limeamua kurudi mitaani kwa kubadilisha jina. Wananchi wa kawaida tunajiuliza nani anawapa kiburi magazeti kama haya?? Kuna kila dalili kuwa haya magazeti ni miradi ya watu wenye nafasi katika nchi ambao labda vyombo vilivyopewa mamlaka kusimamia habari ikiwemo wizara wanawaogopa. Kama si kweli inashangaza kuona wanaandika habari ambazo haziwezi kuvumiliwa na mtu yeyote Yule kwa sababu yeyote. Ushauri kwa Waziri husika ni kufungia haya magazeti na kuwafanya waandishi wa habari wajue kuwa hawako juu ya sheria. Ikisuburiwa mpaka 2015 haitawezekana kuwanyamazisha kwanza watakuja na dharau kubwa kwa serikali hivyo maamuzi YOTE yafanyike sasa. Kwa mawaziri wanaokwenda mwendo wa kinyonga ni wa kati wa kuwapumzisha na kutafuta wakina Magufuli, Muhongo, Mwakyembe, Kagasheki na Tibaijuka wengine wapo wengi tu CCM kina Hazina kubwa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
Ahsanteni Sana
[/TR]
[/TABLE]