Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Sasa nimethibitisha ya kuwa katiba iliyopo ilisiginwa na kutotumika katika kuibadilisha katiba iliyopo kwa sababu ya kumlinda Raisi ambaye atajengewa mazingira ya kila chaguzi zetu atokane na chama tawala cha CCM.
Katika Katiba iliyopo utaratibu wa kuibadilisha katika kwa masuala ya muungano na haya mapendekezo ya tume ya warioba yote ni masuala ya muungano ni shuruti theluthi mbili ya wabunge wote wa bara na theluthi mbili ya wabunge wote wa visiwani waafiki. Utaratibu huo haukufuatwa kwa sababu hakuna mwafaka ndani ya Bunge hili kuhusiana na khoja ya siri ya JK na wenzie ya kumjenga na kumlinda Raisi ajaye ambaye kama rasimu hii itapita lazima ataendelea kutoka ccm na wala siyo vinginevyo.
Swali la kujiuliza JK, Warioba na wapambe wao wanakhofu ya nini baada ya 2015? Ni dhambi zipi wametutendea hadi wajenge mazingira ya kukaza uzi wa kutudhulumu haki zetu za wapigakura hata kuhoji uhalali wa matokeo ya Uraisi na kulazimisha kuyakasimu kwa wagombea kinyume cha katiba hiyohiyo ambayo inasema mamlaka ya dola yanatokana na wananchi wenyewe? Kama wana madhambi ushauri wangu ni watubu tutawasamehe bali wasitegemee kwa kuminya haki za raia ndiyo ufumbuzi wa kudumu wa kulindana utamaduni ambao utapamba moto kama hii rasimu itapita kama ilivyo ..
Kwa JK na wenzie masilahi ya taifa ni kulinda ulaji wao kupitia Raisi ajaye ambaye wathakikisha ni kutoka kwenye chama chao na mazingira anayojengewa ni kama ifuatavyo:
Kuweka mazingira ya kuhakikisha kuwa haki ambazo raia wamepewa zinaporwa papo kwa hapo kwa kujenga mazingira sheria zitaundwa kupora haki hizo:-
1) Ipo ibara inayosema vijana wanayohaki ya kushiriki kwenye Nyanja zote lakini inapokuja uraisi wamewekewa ukomo lazima wazidi miaka 40 na hivyo kuleta ukinzani kwenye katiba hiyo hiyo.
2) Raisi anapoingia madarakani anahitaji zaidi ya asilimia hamsini tena ya wapigakura wote lakini kumngoa inahitajika mapendekezo ya asilimia 75 ya wabunge wote ambao baadhi ya wao ni wateule wake!
3) Raisi hawezi kushitakiwa kwa makosa ya jinai ambayo ameyatenda akiwa madarakani hadi yawe yameidhinishwa na Bunge ambalo ili lifanye hivyo basi robo tatu yao wawe wamekubali ashitakiwe! Huyu Raisi ni Mungu au ni mwanadamu ambaye anapaswa kuwajibishwa kama mwanadamu mwingine? Ikumbukwe katiba iliyopo ni theluthi mbili tu zinahitajika kumwondoa Raisi madarakani na haya mapendekezo yanalirudisha taifa nyuma kwa kuweka masharti magumu ya kumwajibisha Raisi mkorofi kupitia Bunge.
4) Zipo aya zinasema Raisi hana mamlaka ya kuingilia uteuzi na udhibiti wa nidhamu wa taasisi nynginezo lakini wajibu aliopewa Raisi ni kuwaingilia na hivyo kuleta migongano ndani ya katiba hiyohiyo. Yaelekea inapokuja Raisi migongano imeshamiri ili kumfanya awe juu ya sheria.
5) Majaji wakuu ambao siyo sehemu ya Bunge wanapewa kazi za kumdhibiti Raisi kwa kuchunguza tuhuma dhidi yake kazi ambayo ni ya Bunge hivyo kuleta migongano ya mihimili ya serikali ambayo rasimu hiihii imekataza.
6) Majaji wakuu hawahawa ambao hawajachaguliwa na wananchi sasa wanapewa nafasi ya kuwapora wabunge kazi ya kuidhibiti dola na kufanya kazi ya uchunguzi badala ya kufanyakazi ya kuamua kwenye masuala yasiyo ya kisiasa.
7) Mashitaka dhidi ya Raisi yamewekewa muda wa mwaka mmoja bila ya kujali uhalisia wa matukio yenyewe. Khofu ya Tume ya Warioba ni dhahiri kuwa Raisi ajaye hatakuwa na uhalali na ndiyo maana anahitaji kupewa uhalali na katiba.
8) Kwenye kupinga matokeo ya Uraisi, wapigakura hawana sauti na sauti hiyo imekasimiwa kwa wagombea bila ya kutofautisha haki za wapigakura siyo lazima zioane na za wagombea. Mgombea anaweza kununuliwa lakini wapigakura hakuna anayeweza kuwanunua wote. Isitoshe kwenye rasimu hiyohiyo imebainisha ya kuwa wenye mamlaka ya kuongoza dola ni raia wote lakini inapokuja kupinga uraisi wapigakura ambao ndiyo wamemchagua Raisi wameporwa mamlaka ya kuhimili dola ambayo yamo kwenye hii Rasimu. Migongano hii inaonyesha Tume ya Warioba imejaribu sana kuwalinda maraisi wajao wasiwajibike kwa wananchi. Mpigakura akiona kura yake imeibiwa akae kimya tu huku Rasimu inasema raia wanajukumu la kuilinda na kuitetea katiba hii! Raia wataiteteaje katiba kama hawaruhusiwi kwenda mahakamani kudai haki yao kama wapigakura endapo wanaona kura yao haikuhesabiwa kutokana
9) Haki ya rufani imeporwa kwenye kupinga matokeo ya uraisi lakini kwenye Nyanja nyinginezo zote haki ya rufani ipo. Angalau malalamiko dhidi ya chaguzi za uraisi yangelianzia mahakama ya rufaa na kuweka nafasi ya urani kwenye mahakama ya juu badala ya kuanzia mahakama ya juu bila nafasi ya rufani. Haki ya rufani ndiyo moja ya misingi ya kutoa haki sasa ukiiondoa haki hiyo mlalamikaji ataona kweli katendewa haki pale anapokuwa hakubaliani na maamuzi?
10) Muda wa kuwasilisha malalamiko dhidi ya uraisi umeaachiwa sheria za kawaida lakini muda wa kusoma sababu za uamuzi na kuitisha uchaguzi mwingine umetamkwa. Swali hapo kwanini iwe hivyo kama siyo kujenga mazingira magumu ya anayetaka kulalamika kwa kutegemea sheria za bunge badla ya katiba yenyewe na hivyo kutoa mianya ya mahakama hizi zetu zinazoendeshwa kisiasa kutuchagulia viongozi kwa kudai muda umekwisha wa kulalamika? Walalamikaji wangelipewa muda wa wiki mbili tangia matokeo kutangazwa kudai haki yao mbele ya sheria.
11) Viongozi wa kimahakama kwa maana ya majaji wakuu wamepewa nyadhifa nyingi za kiutendaji kama za kuchunguza malalamiko dhidi ya Raisi kazi ambayo siyo yao ikiwemo ya kuteua viongozi wa ngazi za juu wa Tume huru ya uchaguzi kazi ambayo nayo ni ya kiutendaji kwenye Rasimu ambayo inakataza miingiliano ya dola tatu yaani mahakama, serikali na Bunge. Huu mkorogano unalenga kuhakikisha mahakama zinatumika kutuchagulia viongozi ambao watalindana nao. Ikumbukwe chini ya Rasimu hii Raisi ambaye anawateua nao majaji wakuu wamepewa nafasi ya kumpima utendaji wake kazi ambayo ni ya wabunge na hivyo kudhoofisha uwajibikaji wa Raisi kwa wananchi kupitia Bunge lao.
12) Teuzi za Raisi alizowekewa ndani ya Rasimu hii hazina ushiriki wa wananchi wa kutosha na hivyo kumpa mwanya wa kuteua watu awatakao hata kama hawana sifa bila ya ushiriki wa Raia kupitia Bunge lao!
13) Wakati kuondolewa Raisi madarakani kunatokana na ridhaa ya malalamiko ya wabunge inapokuja kuondolewa Makamu wa Raisi Bunge limeporwa hiyo ridhaa na kukasimiwa kwa Raisin a hivyo makamu wa Raisi kutowajibika Bungeni. Kwa lugha nyingie ni kuwa kama Raisi hamtaki Makamu wa Raisi basi anamshitaki Bungeni lakini kama anamtaka hata kama anatuhuma kibao Bunge ni marufuku kuwajibisha. Swali hilo ni Bunge la kuidhibiti serikali au Bunge jina tu?
14) Ukiondoa uteuzi wa Waziri Mwandamizi, teuzi za Raisi za mawaziri namanaibu wao hawahitaji kuthibitishwa na Bunge. Hili Bunge kama haliwezi kuwathibitisha wabunge linawezaje kuwathibiti utendaji wao? Rasimu hii imefanyakzai ya ziada kuhakikisha Bunge lijalo ni Bunge butu ambalo ukiondoa malipo yao halina meno ya kuithibiti serikali.
15) La ajabu mwanasheria Mkuu atathibitishwa na Bunge lakini mawaziri na manaibu wao hapana. Hii imekaaje maana mwanasheria mkuu aliyethibitishwa na Bunge anakuwa na uhalali mkubwa kuliko hata mawaziri na manaibu wao ambao hawajapitia kwenye tanuru la Bunge kwa kupigiwa kura ya maoni.
16) Inapokuja umiliki wa akaunti nje kwa watumishi wa umma, katiba inakataza lakini inatoa mwanya wa Bunge kuunda sheria za kuruhusu watumishi wa umma kuwa na akaunti nje. Tatizo hapa ni kuwa anayetuhumiwa kuwa na akaunti nene nje ya nchi ni rahisi na wasaidizi wake kutokana na misamaha ya kodi ambao haijaidhinishwa na Bunge sasa kuliruhusu Bunge kupitia katiba kuendeleza wizi na uporaji wa mali za taifa hili ni kubariki dhuluma dhidi ya raia. Nilitarajia kutokana na tuhuma za viongozi wengi kutajwa kuwa wanamiliki akaunti kule Uswizi basi Tume isingetelekeka kwenye hili kumbe ndiyo wamejenga mazingira mabaya ya kuisigina hata hii rasimu kupitia sheria ndogondgo za Bunge! Kiburi hiki kimeongezeka hasa baada ya tume kupewa kibali ya kuisigina katiba iliyopo kwa kutumia sheria za kawaida ambazo kupitishwa kwake kunahitaji koramu ya wabunge wasiopungua 30 tu!
17) Inapokuja uthibiti wa misamaha ya kodi ambayo hushinikizwa na Raisi na kupitishwa na baraza la mawaziri hii inayoitwa katiba mpya ipo kimya ikimaanisha ya kuwa business as usual! Yaani hakuna mabadiliko nah ii ni katiba mpya jina tu siyo kimantiki hata chembe.
18) Bunge na mahakama zimenyanganywa haki ya kujua kama Raisi alishauriwa vyema na kupuuzilia mbali ushauri wa baraza la mawaziri lakini bunge hilohilo likisaidiwa na watendaji wakuu wa mahakama kwa maana ya majaji wakuu wamepewa mamlaka ya kumchunguza Raisi. Hivi watamchunguzaje Raisi ambaye ushauri aliopewa wanakatazwa kuuchunguza? Hicho ni kiini macho na bila ya Bunge kuwa na mamlaka ya kuzisoma nyaraka mbalimbali za maamuzi ya vikao vya baraza la mawaziri pale ambapo kuna malalamiko yanayohusu utendaji wa Raisi na mawaziri sasa Bunge litawezaji kutekeleza majukumu yake yta kikatiba kama siyo ubabaishaji tu huu?
19) Makosa ya jinai ambayo yamegundulika baada ya Raisi kustaafu Bunge au mahakama kamwe haziwezi kuyachunguza jambo ambalo linaashiria ni jitihada za kulinda maovu yoyote ambayo Raisi ameyatenda na kumpa kinga ya kijumla ambayo itampa kiburi cha kufanya anavyoona inafaa kwa kuwa yuko juu ya sheria. Hii ni karne ya 21 au tunarudi karne ya 19?
20) Raisi kuteua manaibu mawaziri ambayo majukumu yao yanagongana na ya katibu mkuu ni kupunguza idadi ya wizara bila ya kupunguza matumizi.
21) Kazi za Waziri mwandamizi zinaingiliana na za Makamu wa Raisin a mawziri na hana uhaja zaidi ya kuleta migongano ya kiutendaji. Tume hii ambayo tangia tupate uhuru wamezoea kuwa na Waziri Mkuu wameshindwa kuona na kuwa na uelewa ya kuwa Waziri mwandamizi ni mzigo tu ambao inabidi tuukatae. Waziri mwandamizi kama alivyo waziri mkuu kwenye mfumo uliopo kawekwa pale ili kumlina Raisi kwa kubeba lawama pale mambo yanapokwenda kombo na ndiyo maana zimewekwa ibara za kuthibitishwa na Bunge bila kuwekwa utaratibu wa kuwajibika Bungeni. Bunge halina mamlaka ya kumchunguza chini ya mapendekezo haya. Bunge ni kuthibitisha uteuzi khalafu hawana mamlaka ya kumchunguza utendaji wake!
22) Mawaziri na manaibu wao hawahitaji kuthibitishwa na Bunge lakini katibu mkuu kiongozi uteuzi wake kuthibitishwa na Bunge. Hapa uhalali wa kisiasa wa mawaziri na manaibu wao umefifilishwa na wa katibu mkuu kiongozi ambao anawajibika kwa mawaziri na manaibu wao umeimarishwa lengo haliko wazi hata chembe.
23) Makatibu wakuu hawahitaji kuthibitishwa na Bunge kwa hiy0o matatizo ya kimfumo ya watendaji waandamizi serikalini kutowajibika bungeni rasimu hii inahimiza uendelee!