Rasimu hii ya katiba inalenga kulinda maovu ya maraisi wastaafu na wajao tusiwawajibishe!

Rasimu hii ya katiba inalenga kulinda maovu ya maraisi wastaafu na wajao tusiwawajibishe!

1) Ibara ya 205 (2) imethibitisha tatizo nililoliona ya kuwa tume ya uteuzi inaiingilia kazi za tume ya utumishi wa umma za kufanya mapendekezo ya uteuzi wa wajumbewa tume ya maadili. Inapokuja masuala ya kinidhamu tume ya utumishi wa umma inabebeshwa majukumu ya kuwathibiti wajumbe wa tume ya maadili wakati tume ya utumishi wa umma haikushirikishwa katika kuwateua. Ninarudia kamati maalumu ya uteuzi iliyofurika na majaji ifutwe na kazi zao zichukuliwe na tume ya utumishi wa umma.

 
1) Ibara ya 208 (2) inarudia uteuzi kufanywa na Raisi kutokana na kamati ya uteuzi. Majaji wakuu hawapaswi kuingilia shughuli za kiutendaji siyo zao ni kuleta migongano ya dola isiyo ya lazima. Vile maspika siyo kazi zao kufanya kazi ya kusaili watumishi wa umma kazi hizo waachiwe tume ya utumishi wa umma izifanye.

 
1) Ibara 212 (2) inathibitisha ya kuwa kazi ya uteuzi wa tume ya haki za binadamu ni kazi ya tumeya utumishi wa umma na ndiyo maana wamepewa majukumu ya kushauri kwenye masuala ya kinidhamu sasa ile tume ya uteuzi mbona isizifanye hizi kazi za kuthibiti nidhamu? Wao tume ya uteuzi ni kujaza nafasi tu lakini uthibiti wa nidhamu wanaingia mitini sasa inakuwaje ajira na nidhamu vitenganishwe kama siyo kuleta vurugu? Tume ya utumishi wa umma itafanyakzai zake vizuri kama itapewa mamlaka ya ajira na nidhamu kwa pamoja siyo kutupia Magana na ndizi iwe imeliwa na kama ya uteuzi ambayo sifa za wajumbe ni ujaji mkuu, uspika na ukamishina tu!

 
1) Ibara 213 (1) inatamba tume ya haki za binadamu itakuwa huru wakati ni majaji wakuu, maspika ndiyo wameiteua! Uhuru utatoka wapi wakati kamati ya uteuzi imeshamiri migongano ya mihimili ya dola?

 
1) Ibara ya 216 inasahihisha mapungufu ya Ibara ya 215 kwa kubainisha Tume ya utumishi wa umma itatoa mapendekezo ya teuzi hizi lakini ilipaswa ionyeshe wazi kuwa tume ya maadili itazitangaza nafazi za ajira zote za umma kutoa fursa sawa kwa watanzania wote wenye sifa kushiriki kwenye zoezi hilo kama watahitaji kufanya hivyo bila ya kubaguliwa.

 
1) Ibara 218 ni mbaya. Yawaje mdhibiti na mkaguzi wa serikali akae madarakani miaka yote saba bila ya kupimwa utendaji wake kama unafaa? Yawaje viongozi wengine wapewe miaka 3 na kupimwa tena? Hii Ibara ni ya kibaguzi na ubaguzi unakatazwa na hii rasimu.

 
1) Ibara ya 231 imekwepa kuzungumzia misamaha ya kodi ni marufuku na hivyo kutoa mianya kwa serikali kuendelza ufisadi wa kutoa misamaha ambayo haina tija kwa serikali bali kwa viongozi na wafadhili wao.

 
1) Ibara ya 231 ina utata kwani wachangiaji wa uendeshaji wa serikali ya muungano ilipaswa kuwa ni nchi shiriki badala ya kuingilia mapato ya nchi shiriki. Utaratibu huu utaiumiza Tanganyika kwa sababu makusanyo yake ni makubwa wakati rasimu hii inasema serikali hizi zina hadhi sawa. Makusanyo yaliyoainishwa humu yataipunguzia sana uwezo serikali ya Tanganyika uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu itakuwa imeachiwa majukumu makubwa bila ya nyenzo za kuyatatua na hivyo kuwa na kewro zisizo za lazima. Ninapendekeza kwa vile majukumu ya uendeshaji wa serikali ni machache basi iendeshwe kwa michango ya washiriki wake ambayo itategemea na bajeti na mahitaji na mgawanyo ambao utaamuliwa na tume ya maridhiano ya muungano.

 
1) Ibara ya 231 iondolewe kipengere cha 231 (1) kwa vile ushuru wa bidhaa ndiyo hutumika kuimarisha miundo mbinu. Kwa mfano kodi za mafuta ndizo zinazojenga barabara sasa ukizinyanganya serikali shirikishi wakati miundo mbinu siyo suala la muungano uwezo wa serikali shiriki kuimairisha miundo mbinu yao itapotea na kuleta misuguano isiyo ya lazima.

 
1) Ibara za 240, 245 na 249 Raisi anapoteua wakuu wa majeshi ya ulinzi, polisi au mkurugenzi wa usalama wa taifa inafaa na ni lazima alishirikishe Bunge siyo kujiteulia tu mtu amtakaye yeye tu.

 
1) Ibara ya 251 (3) iongezewe ya kuwa aliyejiuzulu au kustaafu hapaswi kupokea mafao ya uzeeni kama amaeajiriwa ndani ya utumishi wa umma. Mfano tuna mawaziri wakuu wastaafu wako bungeni wanakula mshahara nab ado wanalipwa pensheni wakati bado wamo kwenye utumishi wa umma. Hayo ni matumizi mabaya ya utumishi wa umma.

 
1) Ibara ya 253 (1) irekebishwe na kuwa watajwa hawataruhusiwa kugombea nafasi za umma siyo baada ya miaka mitatu bali baada ya kalenda ya uchaguzi mmoja kupita.

 
Back
Top Bottom