Rasimu ya katiba inaturudisha nyuma miaka 50

Rasimu ya katiba inaturudisha nyuma miaka 50

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Swala la serikali 3 kwa mtazamo wangu lingejadiliwa miaka 50 iliyopita wakati waasisi wa muungano walipokutana kwaajili ya kuunganisha zanzibar na tanganyika.

Lilishajadiliwa na kwa busara zao ikaonekana muundo wa serikali mbili ndio sahihi zaidi...

Kwa sasa kama wakomavu wa Muungano inatakiwa tujadili serikali moja na si 3.

Ubinafsi na uroho wa madaraka umetuleta hapa..hakuna sababu za ziada katika kutetea hili..

Tume ya katiba pamoja na kushikilia msimamo wao kwamba hayo ndio matakwa ya wananchi, hayo ikiwa ni moja wapo ya majukumu yao, wanalo jukumu lingine la kutoa ushauri kwa hao wananchi na kuja na mbadala wa mfumo usioleta kelele toka pande mbili za Muungano.

Kwa sasa zanzibar ina Rais na makamu wawili ( hao hawako mbali na hadhi ya urais).

Tanganyika ina Rais pamoja na makamu wake ( ambaye hayuko mbali na hadhi ya urais)

Hivyo mapaka sasa tuna marais wawili na makamu 3 wenye hadhi ya urais kufanya marais wa sasa kua watano ( tanzania pekee Afrika)

Tukija na mfumo wa serikali tatu ( mnikosoe kama nitakua nimepotosha)

Kutakua na Rais wa Muungano na makamu wake

Rais wa Tanganyika na makamu wake..

Rais wa Zanzibar na makamu wake..

Si ajabu kabisa kuja kua na marais 7 ( tutakua tunaongoza duniani kua nchi moja yenye marais wengi kwa wakati mmoja)

Huu mzigo wa kuendesha serikali ni kwa vyanzo hivi hi vi vya mapato au kuna vingine ambavyo hatuvijui...Ni mzigo kwa wananchi wa tanzania...

Tume ingetumia busara, kutushauri katika mfumo bora zaidi wa muungano kuliko kuongeza matatizo kulingana na mtazamo wangu...Tume imejaa watu makini kabisa wajuvi wa mambo ya kijamii, kisiasa, sheria, uchumi na mengineyo ambayo yangewawezesha kutoa ushauri utakaoleta suluhisho la kudumu badala ya kutuletea mawazo wa wananchi ambayo kama yakitumiwa kama yalivyo yataleta maatatizo zaidi.

Wasomi wetu waliopewa jukumu hilo zito kutuwakilisha katika utunzi wa kanuni za kutuongoza waheshimu wajibu waliopewa na kutuletea katiba bora iliyosuluhisho kwa miaka 50 mbeleni na si katiba ambayo itatulazimu kurudi nyuma miaka 50 na baada ya miaka 2 tuingie gharama upya za kuandika katiba nyingine, itakua aibu ya karne.

Binafsi siafiki serikali 3 kwani ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida na ni kwa manufaa ya wachache tu ukiachana na uhalisia wenyewe.

Serikali moja ndio suluhisho la matatizo yetu kwa sasa, badala ya kutengana tuna wajibu wa kuungana zaidi.
 
Swala la serikali 3 kwa mtazamo wangu lingejadiliwa miaka 50 iliyopita wakati waasisi wa muungano walipokutana kwaajili ya kuunganisha zanzibar na tanganyika.

Lilishajadiliwa na kwa busara zao ikaonekana muundo wa serikali mbili ndio sahihi zaidi...

Kwa sasa kama wakomavu wa Muungano inatakiwa tujadili serikali moja na si 3.

Ubinafsi na uroho wa madaraka umetuleta hapa..hakuna sababu za ziada katika kutetea hili..

Tume ya katiba pamoja na kushikilia msimamo wao kwamba hayo ndio matakwa ya wananchi, hayo ikiwa ni moja wapo ya majukumu yao, wanalo jukumu lingine la kutoa ushauri kwa hao wananchi na kuja na mbadala wa mfumo usioleta kelele toka pande mbili za Muungano.

Kwa sasa zanzibar ina Rais na makamu wawili ( hao hawako mbali na hadhi ya urais).

Tanganyika ina Rais pamoja na makamu wake ( ambaye hayuko mbali na hadhi ya urais)

Hivyo mapaka sasa tuna marais wawili na makamu 3 wenye hadhi ya urais kufanya marais wa sasa kua watano ( tanzania pekee Afrika)

stroke gonjwa baya!!!
 
Back
Top Bottom