Rasimu ya Katiba mpya: CHADEMA toeni dira!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Ni dhahiri kuwa CCM imeparaganyika kutokana na rasimu ya katiba iliyotolewa na Warioba! CCM sasa wameadhimia kutumia mabaraza ya wilaya ambayo wana wajumbe wengi na mabaraza ya kitaasisi yatakayoundwa na CCM kuwaburuza wanachama wao waipinge rasimu hii na kuendelea kuwa na serikali mbili!

Hivyo ili kukabiliana na upuuzi huu wa CCM, CHADEMA wanapaswa kutoa dira kwa Watanzania wote ili mbinu hii chafu ya CCM isifanikiwe! Ukweli ni kwamba hata wana- CCM wenyewe wanatofautiana kwa kiwango kikubwa kuhusu suala hili. CHADEMA haina budi kuchukuwa fursa hii ya mparaganyiko ndani ya CCM kuwaongoza Watanzania wote kupata katiba ya kudumu ya nchi hii kwa miaka 100 ijayo!
 
Mkuu cdm haikurupuki vuta subra soon kamati inakutana kwa ajiri ya kuichambua rasimu hii tutegemea mazuri tu
 
Mkuu cdm haikurupuki vuta subra soon kamati inakutana kwa ajiri ya kuichambua rasimu hii tutegemea mazuri tu
​Inatia moyo lakini ni vizuri pia wafuasi wa CHADEMA wakaandaliwa kupambana na mbinu zote chafu ambazo CCM wanaweza kupanga kuzifanya!
 
Mkuu kuandaliwa kwa wafuasi wa cdm kushafanyika kupitia kurugenzi ya mawasiliano chini ya 2maini makene ama hujasoma bandiko lake?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…