Nashindwa kuelewa, ni mimi ndo sijakuelewa? Kwa maelezo yako uneonekana umeelewa kwamba TANZANIA haitakiwi tena. Ukweli ni kwamba, jina TANZANIA litaendelea kuwepo ktk serikali ya Shirikisho (muungano). Kinachozungumzwa hapa ni serikali hizi mbili, ya Zanzibar na Tanganyika. Kumbuka kabla hizi nchi mbili hazijaungana ziliitwa hivyo, sasa basi tuwe katika majina hayo ktk serikali zetu za nchi washirika, hilo jina TANZANIA tukutane nalo katika MUUNGANO tu. Hii ndo maana ya serikali tatu inayozungumzwa, siyo kwamba jina Tanzania halitakuwepo. Wasiwasi wako nimeuona hapo ulipoanza kuelezea Faida zako za kubaki na jina Tanzania.