Rasimu ya Katiba Mpya: Jina "Tanzania Bara" Linakera!

Mh! Hiyo si sababu ya msingi, jina la T/bara linaleta utata, na umoja wa Afrika unaotaka ww ilikuwa iitwe tu Africa bara na Africa Zanzibar ili kudumisha huo umoja wa Africa, namuunga mkono Jaji Bomani kwa 100%, kwani jina Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar, mambo ya kuengeza bara na visiwani hizo ni mbwembwe tu. Labda useme tu Tanganyika ni jina BAYA!
 
Mkuu hapa hakuna mjadala moja kwa moja we need Tanganyika back
 
Serikali tatu hakuna maana yoyote zaidi ya kuliingizia taifa hasara kwa kulipa matumizi yasiyo ya msingi kama salary ya viongozi na wafanya kazi mbalimbali wa serikali hizoo huku nchi ikiwa bado katika. Madeni na bajeti ya kutegemea wahisani tuu. Is from economical point of view wakuu


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 


Mmmhhhh!!!
 


Nashindwa kuelewa, ni mimi ndo sijakuelewa? Kwa maelezo yako uneonekana umeelewa kwamba TANZANIA haitakiwi tena. Ukweli ni kwamba, jina TANZANIA litaendelea kuwepo ktk serikali ya Shirikisho (muungano). Kinachozungumzwa hapa ni serikali hizi mbili, ya Zanzibar na Tanganyika. Kumbuka kabla hizi nchi mbili hazijaungana ziliitwa hivyo, sasa basi tuwe katika majina hayo ktk serikali zetu za nchi washirika, hilo jina TANZANIA tukutane nalo katika MUUNGANO tu. Hii ndo maana ya serikali tatu inayozungumzwa, siyo kwamba jina Tanzania halitakuwepo. Wasiwasi wako nimeuona hapo ulipoanza kuelezea Faida zako za kubaki na jina Tanzania.
 

Lakini jina la tanzania liwepo ktk shirikisho au muungano,nje ya muungano hakuna jina tanzania kuna jina tanganyika na zanzibar,kwanini wakwepe jina tanganyika na kutaka liwepo tanzania bara??huu ni wizi wa majina ya pamoja jina tz bara liondoke na tusiliogope tanganyika,hili ndio jina halisi
 
labda walihisi watakuwa wanamfagilia mtikila

hebu tushupalie hili jina libadilishwe wakuu! vinginevyo na zanzibar nayo isomeke tanzania visiwani ndo itakuwa imebalansi

Hah ha ha ha ahh Mtikila
 
Wana JF natumaini hamjambo.
Nategemea JF ni fursa nzuri ya kutoa maoni yetu na kueleza yale tunayodhani ni muhimu kwa mustakhabari wa nchi yetu. Nirejee kwenye Rasimu ya Katiba hapa hatuna haja ya kuwa na jazba wala kuzunguka. Kweli, Tume ya Katiba chini ya Mhe. Jaji Warioba imefanya kazi nzuri lakini kimantiki wamepotoka kwa kuandika neno Tanzania bara badala ya Tanganyika. Historia inaonesha nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaa Tanzania. Ukiuita upande mmoja wa muungano Tanzania bara upande wa pili unakuwa Tanzania visiwani. Hizi siyo nchi wala serikali bali ni vielezi tu. Nchi na serikali zao zitabakia kuwa Tanganyika na Zanzibar. Hapa ni suala la marekebisho na yawezekana wakadai kuwa ni typing error. Muundo wa serikali tatu unatakiwa uwe Tanganyika, Zanzibar na Tanzania. Naomba kutoa hoja
 

1. Mpaka hapo tupo pamoja

2. & 3. Hapa tunaanza kupishan;kwanza msimamo wangu kama raia wa nchi hii ni kuwa ama ziwepo serikali mbili ama serikali moja. Sasa kama wazanzibar watatutenga (God forbid) wakawa na serikali yao sisi tuendelee kutumia jina hilo la Tanzania kwa sababu na faida nilizozitaja kwenye post za mwazo za uzi huu. Nia ni njema kabisa ya mimi kutetea tuendelee kutumia jina hili. Nakuhakikishieni tukiweza kuendelea kutumia jina hili tutaepuka mtego ambao wazanzibar wanataka kuingia vile vile tutaweza kukwepa matatizo ambayo Mwl. Nyerere aliwahi kututaadharisha. Lakini kama wazanzibar watakubali ku 'dissolve' serikali yao tukawa na serikali moja basi itakuwa "well and Good" kutumia jina Tanziania maana jambo lilokuwa limeasisiwa na wazalendo wa awali wa nchi hii itakuwa imetimia.

N.B

Kuna jambo moja ambalo nimeligudua kuna wanasiasa ambao wanaotoka eneo la bara la JMT ambao kwa udi na uvumba wanataka wazanzibar watutenge. Wanasiasa hawa utawajua kwa hila yao hii chafu kupitia kauli wanazozitoa... mfano utawasikia wakisema " mfumo wa kuwa na serikali moja hauwezekani kwa sababu wazanzibar hawatakubali ". Nashindwa kuelewa ina maana wanasiasa hawa ndio wanavipimo vya kujua mawazo ya wazanzibar wote ?

Sote kwa pamoja tuhimizane tuwe na serikali moja ....tuachane na mambo ya mashirikisho.
 

Ni kweli nje ya mfumo wa muungano tulionao kuna majina hayo uliyoyataja....lakini pia na kudokeza Hao wazanzibar wanaowalazimisha wenzao wajitenge na sisi hawawezi kuisimamisha serikali ya Zanzibar kwa muda mrefu. Sababu kubwa ya hawa jamaa kushindwa ni kuwa kuna wazanzibar wengi sana ,ambao wako kimya, hawataki kujitenga na sisi. Hivyo, wingi na weledi wao utawasaidia kurudisha kisiwa cha Unguja (chenye ikulu ya zanzabar) katika JMT. Kwa kuzingatia hili, nashauri tuendelee kuwaunga mkono hawa wazazibar waliokaa kimya kwa sasa kwa kutorejea tena matumizi ya jina la Tanganyika. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaelekea kuwa kielelezo bora kuelekea muungano wa maana wa waafrika.
 
Safari hii watanganyika kaunganeni na kenya muitwe tankenyan.

mmmh....we una akili sana! halaf pakitokea taflani kwenye hiyo tankenyan tunaachana nao tunahamia zambia tuitwe tambia au unaonaje hapo.
 

Tukiweza kubaki na serikali moja ya Tanzania ni vema sana. Na ninashindwa kuelewa ni kwanini waasisi wetu waliamua kuwepo na serikali mbili, yaani ya Tanzania (Muungano) na ile ya Zanzibar. Hii inaonyesha Zanzibar haiku-desolve completely kuingia kwenye Muungano (ilibaki na jina lake na serikali yake, WHY???)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…