Rasimu ya Katiba na wabunge

Rasimu ya Katiba na wabunge

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ni lazima wakati huu wa kuandaa katiba mpya watanzaniatutambue kuwa bunge ndio kiini cha mabadiliko katika utendaji wa serikaliitakayokuja baada ya katiba mpya.
Ni wakati sasa wa kutengeneza taasisi za kusimamia ustawi wawatanzania.
Moja ya taasisi muhimu katika kuleta ustawi wa watanzania nibunge.
Nimepitia sura ya tisa ya rasimu ya katiba nikajiulizamaswali mengi maana bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania linatakiwa kukidhimambo mawili
1. Kuwa wawakilishi wa wananchi
2. Kuwa na utaalamu wa kufanya majukumu yake kwa mujibu wa ibaraya 115 ya rasimu.
Mambo haya mawili ndio msingi wa kupata sifa za mbunge ziwezipi.
Ni vigumu sana kwa kuangalia jamii ya watanzania kukidhi matakwaya ya vipengele viwili hapo juu kwa pamoja.
Nikiangalia ibara ya 125 ya rasimu inayoainisha sifa za mtu kuchaguliwa kuwa mbunge inakidhi kipengere chakwanza tu cha kuwa wawakilishi wa wananchi.
Lakini je bunge litakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumuyake kama yalivyoainishwa katika ibara ya 115 ya rasimu? Hapa ninaona tunachezakamali maana mcheza kamali huwa hajui bali anabashiri tu.
Tunasema bunge lijadili mikataba ya sheria ya rasilimali zanchi kabla ya kusainiwa na kuipisha swali kwa mujibu wa sifa za 125 za mtu kuwambunge tutegemee nini katika kujadili mikataba hii (ibara 115 h)?
Kwa sifa za 125 tutegemee nini katika kujadili mipango yamda mrefu, kati na mfupi ya maendeleo ya taifa (ibara 115 f)
Kiukweli kwa mujibu wa sifa tulizoainisha katika ibara ya125 bunge halitakuwa na uwezo wa kufanya kazi zake za ibara ya 115 kwa ustadimaana upo uwezekano wa bunge kutakiwa kujadili mkataba wa madini lakini hakunamtu hata mmoja anayeifahamu sekta ya madini na wabunge kuishia kutaja vijijivinavyozunguka maeneo ya madini, kutaja mambo ya kawaida ambayo kila mtuanayajua na mwisho kupitisha bila uchambuzi wa kina kujua triki zilizopo zakimkataba na kuagiza mabadiliko. Hivyo hivyo kwa sekta zote.
Watanzania kama tunataka maendeleo tuwekeze katika kujengataasisi kwa kuzijengea uwezo wa kufanya kazi, kuzipa taasisi uhuru na hapotutegemee mipango inayopangwa kwanza itakuwa na tija na pili itatekelezwa.
Ili kulijengea bunge uwezo wa kufanya kazi zake. Ninapendekezabunge liwe na sura mbili
Sura ya kwanza ni uwakilishi wa wananchi ambao sifa zakezimeanishwa katika ibara ya 125 ya rasimu.
Sura ya pili ni kuweka wabunge wa kisekta.
Tunaweza kuwa na sekta zifuatazo
1. Afya
2. Elimu
3. Sheria
4. Uchumi
5. Kilimo
6. Nishati
7. Usafirishaji
8. Viwanda
9. Ustawi wa jamii
Kila sekta tunaamua iwe na wabunge watano ambaotunachanganya wazoefu wa field work na watafiti katika sekta husika. Hawa bungenikazi zao ziwe ni kuweka input katika mambo yanayohitaji utaalamu lakini piawakati bunge haliendeshi vikao hawa wanaenda kufuatilia utendaji wa sekta zaona kulipatia bunge hoja za kushauri au kuwajibisha serikali. Nilivyozitaja hapojuu sekta hizo zinaongeza wabunge 45 ambao wapo wanaoweza kusema ni wengi ilatujiulize iwapo tutaongeza wabunge 45 au 50 bunge likawa na tija tunawezakudhibiti mapato kiasi gani kwa mwaka na kuwahudumia hawa ni kiasi gani kwamwaka na hapo tuchague kutokea hapo. Kwa muundo wa bunge ulivyo ninawasiwasihatuwezi kupata bunge la kushauri na kusimamia serikali bali chombo hikikinahitaji utaalamu ili kutimiza malengo yake na utaalamu huu hatuwezi kuupatakwa kutegemea kura za wananchi maana unaweza kupata taaluma moja nusu yawabunge na taaluma nyingine hakuna kabisa. Pia hatuwezi kusema kuunda vyombovya kushauri bunge maana hakuna haja ya daktari amfundishe mwalimu mambo yaliyokatika sekta yake alafu mwalimu akajadili muswada wa afya kwa nini daktari mojakwa moja asijadili muswada wa afya kwa mambo ya kitaalamu huku kukiwa na watuwanaotoka katika katika jamii kuleta mrejesho wa kijamii.
Lakini pia kwa wabunge wawakilishi wa wananchi katiba itajemajukumu ya mbunge, wawe ni wakaazi wa majimbo yao wakikusanya takwimu za utendajiwa serikali katika majimbo yao na sio mfumo wa sasa wa mbunge anafanya biasharazake akitoka kwenye biashara zake anatafuta maneno tu ya kwenda bungenikuongea.
 
Back
Top Bottom