Rasimu ya katiba: Uraia wa Nchi mbili

Rasimu ya katiba: Uraia wa Nchi mbili

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
480
Reaction score
644
Naomba msaada kwenye RED hapo. Inamaanisha nini swala kuwa sheria na sio kwenye katiba. Najua hakuna stupid question. Na watu wenye uraia wa Tanzania wa kuzaliwa wakiwa na uraia wa nchi nyingine wataruhusiwa kupiga kura au kugombea nafasi kwenye serekali. Naongelewa mzawa ambaye anauraia wa nchi nyingine.

  • Uraia wa Nchi mbili

Ndugu Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
 
Hayo ni majanga ndani ya katiba
 
Huo ndiyo ukweli,hakuna sababu kwa jambo dogo kama hili kuandikwa ktk Katiba yetu.
 
Mafisadi wote watakuwa na uraia wa nchi nyingine ili wakishaiba na kuweka huko Uswiss waende kuishai huko huko. Mtanzania wa kawaida inamnufaisha nini?
 
Wapo sahihi sana tume. Silipendi kabisa suala la 'dual citizenship' ambalo Membe analipigia debe sana!
 
Naishukuru sana Tume ya Katiba imekuwa makini sana kuepuka kuifanya katiba yetu mpya isiwe na viraka viraka kama hii ya mkoloni. Hata hivyo ikiingizwa kwenye sheria suala la uraia wa nchi mbili sheria itamke wazi kwamba kwa kiongozi yeyote mwandamizi ambaye alikuwa madarakani na uongozi wake umekoma kwa sababu ya kumaliza kipindi chake cha kuwa madarakani, au ameachishwa au amestaafu uongozi wa umma hataruhusiwa kuomba uraia wa nchi mbili hadi amemaliza miaka mitano tangu awe nje ya uongozi. Hii itasaidia kukamilisha uchunguzi wa madudu aliyoyafanya kipindi akiwa madarakani. Baada ya miaka mitano kupita ndipo aruhusiwe kuomba huo uraia wa nchi mbili na asubiri majibu ya kupata au kukosa bila kujali madaraka yake ya awali au protocol aliyonayo.

Hii ni kwa ajili ya kuepusha wizi wa fedha za umma leo hii kuna vigogo wana fedha za nchi yetu nchini Uswiss wametulia kana kwamba hayawahusu sisi Watanzania tumechoka kuishi maisha ambayo Mungu hakutuumba tuyaishi ugumu huu wa maisha ni "MAN MADE STYLE OF LIFE"

Mungu Ibariki Tanzania:
Mungu Ibariki Tanganyika:
Mungu Ibariki Zanzibar:

We are really tired of you leaders!!!
 
Nitofautiane na mtazamo wako. kama alikuwa kiongozi mwandamizi kwanini akimbilie kuwa raia wa nchi nyingine? Uongozi wake ndiyo uliyoifikisha nchi hapo ilipo kwa nini akimbilie uraia mwingine kama siyo kuyafuata mabilioni yetu ya dollar aliyofisadi?!

mimi naona isiruhusiwe kwa kiongozi mwandamizi ama aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi kuwa na uraia wa nchi mbili.
 
Wamependekeza uraia ya nchi mbili uwekwe kwenye sheria badala ya Katiba (Sheria mama) ili iweze kutumika kwa maslahi binafsi kisiasa hapo baadaye.. kama kuzuia mtu asigombee nafasi fulani baadaye-kwani mchakato utakuwa rahisi(kubadilisha sheria siyo katiba). - ndiyo 'loose ends' zenyewe..
 
Naomba msaada kwenye RED hapo. Inamaanisha nini swala kuwa sheria na sio kwenye katiba. Najua hakuna stupid question. Na watu wenye uraia wa Tanzania wa kuzaliwa wakiwa na uraia wa nchi nyingine wataruhusiwa kupiga kura au kugombea nafasi kwenye serekali. Naongelewa mzawa ambaye anauraia wa nchi nyingine.

  • Uraia wa Nchi mbili

Ndugu Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.

Mkuu kwa hili naamini limekaa vzr sana, hii itapunguza ''ukinyonga'' kwa baadhi ya watu haswa wenye nia mbaya au kufanya mabaya na baadae kusepa kiaina. So ikiwa katiba itawaruhusu kuna uwezekano leo ukawa mkenya, na kesho ukawa mzambia ili mradi kukwepa baadhi ya mambo. Lkn ikibaki kwenye sheria itasadia kupunguza ukinyonga huo. Naunga mkono hili katika rasimu ya katiba!
 
Think Twice Guys! Kuna ndugu zetu walizaliwa nje, sasa sijui according to most of you ni kwa makosa! Wanastahili uraia wa huku, origin yao, hebu tupunguze ubinafsi, sio kwamba kwa sababu labda bahati mbaya hujawa na exposure kiasi hichoo! ukaanza kuzuia wengine wasipate Haki zao, please please!

Dual citizenship ni muhimu saana kwa kipindi hichi, Watu wanaague eti mtu anaweza kuwa muovu, hiyo sio point kwani mzungu mwizi hawezi kamatwa na kushtakiwa kwa uizi wake? hebu tusijustify weaknesess zetu, tuwe fair!
 
kwanini kuwa na uraia wa nchi mbili?huo sio uzalendo.uraia wa nchi moja ndiyo unaohitajika.ni utafiti gani umefanyika kama watanzania wanahitaji kitu?uraia wa nchi mbili ni ufisadi mtu anweza kufanya kazi nchi fulani akaharibu na kukimbilia nchi nnyingine ili kukwepa kuwajibishwa.na kwa nni hasa mtu uwe na uraia toka nchi mbili na shida ni nini.
 
Uraia wa nchi mbili mi sioni kama ni muhimu sana hasa kwa watanzania. Kama mtu kazaliwa nje ya nchi na angependa kuishi huko na kuwa raia wa huko basi na atumie uraia wa huko! na kama ataamua kurudi Tanzania basi aukane uraia wake wa awali! Kumbuka huwezi kuwatumikia mabwana wawili ni lazima tu utakuwa mnafiki tena mkubwa kwa bwana mmojawapo! SIONI POINT KABISA YA KUWA NA URAIA WA NCHI MBILI NA WANAHITAJI HILI JAMBO NI WALE WASIO WAZALENDO KABISA ILI AKILIKOROGA HUKU AKIMBILIE UPANDE MWINGINE AMBAKO ATAPANDA KINGA FULANI. MFUMO WETU WA SASA KUHUSU URAIA NI BORA SANA VINGINEVYO TWAJA JUTA HAPO BAADAYE KWA UPUUZI HUU WA DUO CITIZENSHIP! WATAKUJA WAZUNGU HAPA WATATUMIA HUO MWANYA MSIPOKUWA MAKINI NA KUWAFILISI. SASA HIVYO HAWANA URAIA WATANZANIA WANATUIBIA HIVYO WAKIPEWA HUO URAI JE ITAKUWAJE? TUSIJIFANYE TUNAHURUMA SANA KUMBUKA HURUMA BILA MIPAKA NAYO INAUA!
 
Back
Top Bottom