Chadema Diaspora
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 480
- 644
Naomba msaada kwenye RED hapo. Inamaanisha nini swala kuwa sheria na sio kwenye katiba. Najua hakuna stupid question. Na watu wenye uraia wa Tanzania wa kuzaliwa wakiwa na uraia wa nchi nyingine wataruhusiwa kupiga kura au kugombea nafasi kwenye serekali. Naongelewa mzawa ambaye anauraia wa nchi nyingine.
Ndugu Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
- Uraia wa Nchi mbili