Rasmi: Atletico Madrid ndio klabu inayoongoza kwa kuingiza mapato makubwa zaidi kwenye mauzo ya wachezaji

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Kutokana na Mauzo ya Mshambuliaji Antoine Griezmann jana mchana kwa kiasi cha €120 Million hivyo kufikisha mapato ya Atletico Madrid kwenye mauzo ya wachezaji wao ndani ya miaka 10 hii ni €1,080 Million yaani €1.08 Billion. Hivyo kuvunja rekodi ilioshikiliwa na Benfica huko nyuma kwa mbali sana.


Hii ni takwimu kabla ya mauzo ya Griezmann jana

NB: dirisha hili tu wameingiza tayari €300 Million kwa mauzo ya wachezaji watatu tu yaani Lucas hernandez €80 M, Rodri Hernandez €70, Griezmann €120 M.

Je klabu zingine zina lipi la kujifunza?
 
diego simeone ameifanya atletico madrid iwe ni timu tishio barani ulaya kwa takribani miaka 8 tokea akabidhiwe madaraka ya kuisimamia klabu hiyo, kabla ya ujio wa diego simeone atletico walishindwa kufikia nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu kwa takribani miaka 10 (2001-2011).

ujio wa diego simeone umepelekea atletico madrid waondokane na laana ya kushindwa kuvuka kwenye hatua ya 16 bora kwenye michuano ya UEFA laana ambayo imedumu tokea mwaka 1997.

ninachowapendea atletico madrid ni tabia yao ya kulipa fedha kwa mujibu wa kiwango cha mchezaji husika, ikitokezea mchezaji ana kiwango cha wastani basi watamnunua kwa fedha ndogo baadae watamtengeneza aendane na mfumo wa uchezaji unaotumiwa na mwalimu ndio maana imekuwa ni vigumu sana kumkuta mchezaji anashidnwa kuendana na style ya uchezaji wa timu na ushahidi wa hilo jaribu kurejea usajili wa savic ambaye alishindwa kuwika man city.

atletico madrid si wabahili kwenye biashara ya kununua wachezaji mahodari vile vile atletico madrid wapo vizuri sana kwenye biashara ya kuwauza wachezaji wao nyota kwa fedha nyingi(aguero, falcao, jackson martinez,curtois, griezman, miranda n.k)

utofauti mkubwa kati ya atletico na benfica unakuja kwenye manunuzi ya wachezaji waliokwisha tengenezwa, mara nyingi benfica wanatengeneza wachezaji wenye wao kwa kuwanunua kwa fedha ndogo na kuwauza baadae kwa hela nyingi ndio maana hawafanyi vizuri barani ulaya ukilinganisha na atletico madrid
 
FC Porto nao huwa wanajitahidi sana kuna kipindi walitoa wachezaji wengi sana, sishangai kuwa katika nafasi iliyopo, vipi vilabu vya Olyimpique Lyon kumbe ni wakawaida sana katika kuuza na kununua
 
Realmadrid wanamtaka Mbape, kwa Neymar ni media na agent wake wanacheza mchezo ili kuongeza thamani yake, Neimar wakati anataka kuhama Santos alionywa sana kuhusu kwenda kuwa kivuli cha Messi angekuja Madrid leo hii ndo angekuwa icon ya timu ishatoka hiyo, Madrid wanajua after Hazard ni Vicinious au Mbape.
Uuzaji na ununuzi bado unaendelea. Real Madrid wanamsarandia Neymar sijui kama watampata na tayari wameshatumia pesa ndefu sana. BARCA wakidengua usishangae akitua Real Madrid.
 
Man u for the best 10 years haijauza mchezaji yoyote kwa pesa ya maana kivipi haijaguswa na FFP rules ?
 
Hzo data mbona zinanipa ukakasi .

Cost of purchasing player
Less- Revenue of selling player
= Profit or loss Obtained by the Club.
Sasa kama ni hvyo hapo kwa Atletico naona wana negative balance alafu mnasema wametengeneza faida kubwa?
 

Hakuna cha kujifunza hapo

Saabu purchase yao ni kubwa kuliko mauzo yao,mwisho wanafanya kuwa na balance ya -Ve
 
Benfica ndo wanapata faida,hao wengine ni hasara tupu
Benfica wana faida kwenye mauzo kweli ila nje ya hapo hawana faida kuzidi timu yeyote hapo..... Atletico kwenye mikataba tu ya Tv, masoko,Viwanja n.k kutokana na usajili inaofanya hao Benfica hawafikii hata 15% ya Faida ya Atletico.

Unless Benfica ingekua inawatunza hao wachezaji angalau misimu miwili kama Atletico ili waifikishe mbali UEFA... Wapate coverage kubwa iongeze washabiki, wauze jezi,wapanue uwanja, Tv rights wapewe hela nyingi n.k kuliko kuambilia hizo faida za kuuza mtu mmoja mmoja huku mapato mengi hayakuwi ni biashara kichaa

NB: -7 Ni kabla Griezmann hajauzwa kwenda Barca hivyo isomeke + €113 Million
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…