diego simeone ameifanya atletico madrid iwe ni timu tishio barani ulaya kwa takribani miaka 8 tokea akabidhiwe madaraka ya kuisimamia klabu hiyo, kabla ya ujio wa diego simeone atletico walishindwa kufikia nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu kwa takribani miaka 10 (2001-2011).
ujio wa diego simeone umepelekea atletico madrid waondokane na laana ya kushindwa kuvuka kwenye hatua ya 16 bora kwenye michuano ya UEFA laana ambayo imedumu tokea mwaka 1997.
ninachowapendea atletico madrid ni tabia yao ya kulipa fedha kwa mujibu wa kiwango cha mchezaji husika, ikitokezea mchezaji ana kiwango cha wastani basi watamnunua kwa fedha ndogo baadae watamtengeneza aendane na mfumo wa uchezaji unaotumiwa na mwalimu ndio maana imekuwa ni vigumu sana kumkuta mchezaji anashidnwa kuendana na style ya uchezaji wa timu na ushahidi wa hilo jaribu kurejea usajili wa savic ambaye alishindwa kuwika man city.
atletico madrid si wabahili kwenye biashara ya kununua wachezaji mahodari vile vile atletico madrid wapo vizuri sana kwenye biashara ya kuwauza wachezaji wao nyota kwa fedha nyingi(aguero, falcao, jackson martinez,curtois, griezman, miranda n.k)
utofauti mkubwa kati ya atletico na benfica unakuja kwenye manunuzi ya wachezaji waliokwisha tengenezwa, mara nyingi benfica wanatengeneza wachezaji wenye wao kwa kuwanunua kwa fedha ndogo na kuwauza baadae kwa hela nyingi ndio maana hawafanyi vizuri barani ulaya ukilinganisha na atletico madrid