Rasmi derby ya kariakoo imekufa, Simba wamekuwa dhaifu kipindi kirefu

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Mechi ya derby ya Leo Yanga tupo kama tumecheza na Namungo

Simba tumewafunga sana, yaani huu mwaka wa 4 mnakuja kwenye mechi kama under dog🐕

Derby hauvutii kabisa, Simba haina wachezaji wazuri

Wazee wa ubaya ubwela mnayumba.
Mara MUKWALA- ni striker mrefu kuliko goli kumbe mbumbumbu mnaibiwa.

Kwa Sasa Yanga vs Azam ndo derby

Simba tengeneza team, mo anawadanganya wale wachezaji wenu marasta hamna kitu
 
Pole
 
Hivi unajua maana ya derby?

Unajua historia ya hivyo vilabu 2 vya Kariakoo?

Azam ana historia gani ya kiushindani kati yake na Yanga mpaka wanapokutana ndio iitwe derby?

Mavi matupu umeandika
 
Wenzako wanatamba huko wana timu 😂
 
Mimi siyo shabiki ila kiukweli Mo ni tatizo na Simba siyo team bali kusanyiko la wachezaji.

Ubaya ubaya!
 
Huelewi maana ya derby. Kwa tafsiri yako, kuna siku itatokea Yanga na Mbeya City utaiita Kariakoo derby
 
Naona kwako Derby ina maana tofauti.
London Derby (Chelsea Vs Arsenal) ipo na haifi.
Catalunya Derby (Barcelona Vs Malorca) haifi hata mmoja akiwa mdebwedo.
Milan Derby (AC vs Inter) hata mmoja alipopokwa point haikuteteleka.
Hiyo ni mifano na iko mingi. Huwezi kuua Derby Kwa unyonge wa mmoja. 2018-2021 kwenye peak ya Simba basi utani ungekufa. 1988/89 Simba alipokuwa anaelekea shimoni utani ungekufa.
 
Nanina wee jamaa hahahaa..eti wale wachezaji wenu marasta..simba chama la wahuni,kuanzia viongozi,mashabiki hadi dimbani.
 
Hivi utopolo mnaweza kukaa bila kuizungumzia simba?
 
Simba si mbaya sana sema chemistry ya wachezaji haijaungana vizuri, tuwape muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…