Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kocha Miguel Gamondi leo Februari 16, 2026 amesaini mkataba rasmi wa kuinoa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameongoza tukio la utiaji saini mkataba wa kocha Gamondi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaki Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa pamoja na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzanía (TFF) Walace Karia.
Gamondi ataiongoza Taifa Stars kuelekea michuano ya AFCON 2027 itakayofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Ikumbukwe Gamondi aliiongoza Tanzania Katika michuano ya AFCON 2025, ambapo timu ya taifa ya soka ya Tanzania ilitinga hatua ya 16 bora.